Kwani leo? Ni kitambo sana. Si kwa kesi ya Simba ni issue tofauti. Jiwe alipoingia tu jumba jeupe akaanza kumsulubu nadhani partly kuna uhusiano na issue ya huu uzi. Kuna malori ya jamaa zaidi ya 20 kuna wakati yalikaa border ya Tunduma zaidi ya mwezi eti kodi gani sijui haijalipwa. In the end jamaa akajiongeza akakumbuka ni issue ya makaburi so ikabidi ayauze yote na kampuni yote kwa ujumla akaishia zake. Ila mimi sielewi, hivi hapa duniani tunaishi milele? Vitabu vya dini tunavyoviamini (ninaamini tunaviamini ndio maana kutwa kucha tunaomba tuombewe) vinasema kuna maisha baada ya kifo. Sasa kwanini tunaishi tofauti as if tutaishi milele? Chuki zinatusaidia nini na sisi ni wacha Mungu (sina hakika hii ni kwa mujibu wa yale tuyasemayo majukwaani).