Hans Poppe wa TATOA amchambua Magufuli

Hans Poppe wa TATOA amchambua Magufuli

Nilidhani hii ni post ya awamu hii, ningeshangaa.
 
Ila zamani watu walikua jeuri jaman, haswa wafanyabiashara walikua na nyodo mnoo, angalia huyu jamaa alivyothubutu kumtukana Waziri mzima tena mbele ya kamera, ukitaka kujua utam na karaha ya dunia mjibu tu Mkuu wa Wilaya shit sasahivi ndio utaita maji mma
 
Hans Poppe alikuwa na lugha chafu sana kwa msiomfahamu alikuwa anawatukana mpaka mawaziri kwenye serikali ya JK huku akisema kuwa nchi hii Hakuna wa kumfanya lolote......

Alikuwa analalamikiwa na Tanroads kwa kuzidisha uzito kwenye maroli yake na yeye akawa anawajibu watu kuwa yeye haongei na mbwa......

Kwa mhuni fulani mwenye majibu ya kihuni na kejeli iliyochanganyikana na dharau....watu wengi tulijiuliza hii jeuri anaitoa wapi....!!
Mkuu ukitaka kujua alikua na jeur na kibri angalia alivyomnanga Waziri tena mbele ya kamera asee acha anyooke
 
Ila zamani watu walikua jeuri jaman, haswa wafanyabiashara walikua na nyodo mnoo, angalia huyu jamaa alivyothubutu kumtukana Waziri mzima tena mbele ya kamera, ukitaka kujua utam na karaha ya dunia mjibu tu Mkuu wa Wilaya shit sasahivi ndio utaita maji mma
Na wewe acha kuish kama dedere....... kwahiyo unaona Hao watu ni Miungu yako... haya nenda kaiabudu
 
inasemekana alikaa sehemu kwenye mazungumzo akamponda Mtukufu malaika toka chato kumbe kulikuwa na mpambe akamrecord akampelekea kila kitu ndipo Mtukufu magufuli akasema tafuta upenyo lazimisha foji hata sahihi yake aingizwe kwenye hiyo kesi kwa nguvu, kisha akiwa jela wamuongezee kesi zingine nyingi zaidi, Visasi vya namna hii havina tija kwa Taifa na havileti maendeleo kamwe.
Mmbea wewe
 
Kama kuna mambo huyu Magu kayashughulikia kikamilifu na kwa 100% basi haya:

1. Kuwashughulikia kikamilifu wabaya wake wote a.k.a kulipiza kisasi kikamilifu

2. Kuwadhibiti kikamilifu wakosoaji wake wote, ikiwemo kuwaua na kuwatupa jela

3. Kukusanya kudhibiti PESA zote, na kuzigawa yeye binafsi ATAKAVYOJISIKIA
Bado kukidhibiti wewe
 
Mhazini wa TATOA ambacho ni chama cha wenye malori Tanzania amemwita Magufuli ni mtu asiyejua na ambaye ana chuki kubwa kwa transporters na angeweza angewaondoa wote nchini kwa tuhuma za kufikirika kuwa wanaharibu barabara.

Amekwenda mbali zaidi kwa kusema anafikiria kuwa Magufuli anafanya makusudi ili apate mgao wake wa rushwa. Hii ni kwa sababu amewaagiza wafanyakazi wa mizani ya Iringa wawatoze faini wenye malori na kuuliza kwanini faini zinapungua. Hans Poppe anasema faini zinapungua kwa sababu transporters wamekuwa compliant so hawatakiwi kutozwa faini ovyo.

Amesema Magufuli ndio Waziri wa ovyo kuliko wote kwa kuendesha uongozi wa vitisho na amri za ovyo na kwamba mainjia wote wanamwogopa sana na wanasema hivyo.

Anasema ingawa Magufuli si injinia lakini elimu yake inatosha kutoa mwongozo mzuri ila anafanya makusudi.

Amesema amri ya Magufuli kuondoa tolerance ya 5% katika uzito wa mizigo ni kinyume cha sheria kwani hiyo ni sheria au taratibu iliyowekwa tokea zamani wakati Magufuli bado anasoma.

Kwa hitimisho wameamua kusimamisha malori yote kutofanyakazi kuanzia kesho.

Hii imetoka katika mahojiano na ITV 5 minutes ago. Ipo kazi!
Hana lolote huyu,anatapatapa tu.Wenye malori ikiwa ni pamoja na yeye wamechangia sana kuua reli zetu ili wa-monopolize usafirishaji wa mizigo kwa kutumia malori yao.Zipo taarifa kwamba wame-collude na viongozi wasio waaminifu wa serikali ili kufanikisha adhma yao hiyo ovu.Ni wazi kwa hiyo kwamba ujenzi wa SGR ni mkuki moyoni kwao and hence the hate!
 
Si ilikuwaje ccm wakampitisha huyu mtu.........
 
Ndo sasa Baba Bashite ajue aina ya mtu anayepambana naye...huyu ni retired Military officer aliyewahi kuwaza kumpindua Rais wa nchi, tena Nyerere, na almanusura afanikiwe...he can still do it....tena kwa huyu kiberenge ni rahisi tu!
Dah!! eti kiberenge. nimecheka sana, sijui umewaza nini! hahahaaa
 
Mkuu Visasi Visasi vimewatafuna wengi hata Yusuph Manji alipigwa kwa Visasi vya zamani na sasa anawasaka Risasi rostam Aziz na wenzake kwa bidii ili awakomoe ni hatari na Aibu kufanya kazi kwa Visasi.
mkuu hapo kwa rostam itakuwa ndoto kwake
 
Nilidhani hii ni post ya awamu hii, ningeshangaa.
Historia ni mwalimu mzuri. Alichoongea Zakaria Hans Poppe miaka mitano iliyopita kinaendelea leo.
 
Mkuu ukitaka kujua alikua na jeur na kibri angalia alivyomnanga Waziri tena mbele ya kamera asee acha anyooke
Sasa mtu asijibiwe? kwani kuna sheria kavunja? mtu kutoa maoni yake imekuwa taabu. Huko USA kila siku Trump ana tukanwa na mambo yanaenda.
 
Back
Top Bottom