Hans Poppe wa TATOA amchambua Magufuli

Hans Poppe wa TATOA amchambua Magufuli

Mhazini wa TATOA ambacho ni chama cha wenye malori Tanzania amemwita Magufuli ni mtu asiyejua na ambaye ana chuki kubwa kwa transporters na angeweza angewaondoa wote nchini kwa tuhuma za kufikirika kuwa wanaharibu barabara.

Amekwenda mbali zaidi kwa kusema anafikiria kuwa Magufuli anafanya makusudi ili apate mgao wake wa rushwa. Hii ni kwa sababu amewaagiza wafanyakazi wa mizani ya Iringa wawatoze faini wenye malori na kuuliza kwanini faini zinapungua. Hans Poppe anasema faini zinapungua kwa sababu transporters wamekuwa compliant so hawatakiwi kutozwa faini ovyo.

Amesema Magufuli ndio Waziri wa ovyo kuliko wote kwa kuendesha uongozi wa vitisho na amri za ovyo na kwamba mainjia wote wanamwogopa sana na wanasema hivyo.

Anasema ingawa Magufuli si injinia lakini elimu yake inatosha kutoa mwongozo mzuri ila anafanya makusudi.

Amesema amri ya Magufuli kuondoa tolerance ya 5% katika uzito wa mizigo ni kinyume cha sheria kwani hiyo ni sheria au taratibu iliyowekwa tokea zamani wakati Magufuli bado anasoma.

Kwa hitimisho wameamua kusimamisha malori yote kutofanyakazi kuanzia kesho.

Hii imetoka katika mahojiano na ITV 5 minutes ago. Ipo kazi!
sio waziri tena mkuu
 
Huyo HANS POPE ni -------- tu, kama wakigoma wagome wao, hata hivyo malori kutoka nje yanaendelea na safari. Na nyinyi munompa kichwa na kumsifia HANS POPE ni wapuuzi tu, inawezekana hamumujui magufuli. Ngoja niwape mfano mdogo wa mjinga mmoja aliyekuwa na kiburi na dharau kama HANS POPE jinsi magufuli alivyo mfanya kitu mbaya.....

Kuna jamaa mwarabu mmoja anaitwa Zakheimu alikuwa mkandarasi mkubwa sana hapa nchini, siku moja wakandarasi wakaandaa mkutano na magufuli akaalikwa kama mgeni, kilichotokea ni kwamba MAGUFULI alichelewa kufika kwenye mkutano, MAGUFULI alipofika kwenye mkutano yule ZAKHEIMU akamfuata MAGUFULI na kuanza kumtukana nanukuu "yaani waziri mzima unachelewa kwenye mkutano sikutegemea kama waziri unaweza kuwa na akili ya ajabu kiasi hiki na hatukutaki tena kwenye mkutano" Magufuli akamjibu ZAKHEIMU nanukuu "wewe mwarabu unatoa wapi jeuri ya kunitukana mimi waziri tena wewe ni mgeni ndani ya hii nchi, sasa tutaona, nahakikisha kuanzia leo kampuni yako haipati kandarasi au tender yoyote labda ya kutengeneza bara bara za mtaa, labda mimi sio magufuli nakuapia" tokea hapo mpaka leo kampuni ya ZAKHEIMU imekufa na nasikia siku hizi ZAKHEIMU ameamua kuokoka. Zamu ya huyo kibaraka HANS POPE inakuja, kumbukeni magufuli haonei mtu bali anasimamia sheria na ndicho kinachotakiwa kwa kiongozi bora "utawala wa sheria"
Hatimaye zamu ya Hanspope imefika Mkuu.
 
Mimi simuungi mkono Magufuli hata kidogo kwani hata yeye anadharau sana na amri zake za kiimla.Umedharau utadharaulika pia this is principle kwani yeye nani.Mizani zinapima tofauti na watu wanapigwa faini ilo analisemeaje.Walitoka watu wa wizara,Tatoa na wa mizani wakaondoka na magari yakapima tofauti kibaha,Chalinze,Msata na makambako gari iloilo hii imekaajae.Lori la mafuta linapima kila mizani huu si uhuni na kuwatesa kwa foleni bila sababu ya msingi.
Kumbe jamaa kaamza uu-IMLA kitambo sana.
 
Yeye anasema Magufuli ana chuki binafsi na transporters, mimi nasema yeye ana chuki binafsi na Magufuli.

Miezi kadhaa iliyopita alikuwa akihojiwa na kipindi cha television (sikumbuki kituo gani), jamaa aliyaongea hayahaya, tena kwa dharau na kebehi kubwa kwa magufuli utafikiri anamuongelea mtoto wake. Nilijiuliza sana huyu jamaa anapata wapi kiburi hiki? Nikahisi kuna nguvu nyuma yake na si bure!

Inawezekana jamaa ana hoja, lakini jinsi anavyowakilisha hoja zake inaudhi.

Simuungi mkono Magufuli, lakini si vema pia mtu kuwasilisha hoja kwa dharau kwa waziri mwenye dhamana!
Sasa hivi yamemtokea puani. Jiwe hua hasahau wabaya wake
 
In a nutshell: Magufuli anaonekana na watanzania kama mtu hodari na mchapakazi, kiuhalisia mimi naona kinyume chake.

Binafsi si msafiishaji wala sina uhusiano wowote na sekta hiyo , lakini ninasafiri sana kwa barabara nchi karibu zote za SADC, Suala la mizani na sheria zake zinazidi Kuwa tight hapa kwetu pengine kuliko nchi nyingine za sadc, na pengine ndo tunaongoza kwa rate ya uharibifu wa barabara kuliko wenzetu kwa sababu ya ubabe wa mtu mmoja tu, MAGUFULI !!!

Uharibifu wa barabara kwa kiasi kikubwa unatokana na sheria mbovu zilizowekwa na kusimamiwa na viongozi husika, kulalamkikia wasafirishaji ni sawa na kuficha ukweli wa tatizo, si kweli kuwa tunabeba mizigo mizito sana. Bali tuna utaratibu mbaya wa kubeba mizigo ndo maana barabara zetu hazidumu.

Kuna mawili huwa nafikiri dhidi ya wizara hii na watendaji wake: Either wananufaika na rushwa kutoka kwa wasafirishaji hivyo wanaopt njia ambazo hazitatui tatizo bali kuiongezea mzigo serikali na mtu wa kawaida au hawajui na hawako serious kuboresha pengne kuondoa kabisa sheria kandamizi zinazopelekea watu kutocomply.

Mfano: Botswana idadi ya juu ya axle ni 9 urefu mwanzo hadi mwisho ni mita 22, hapa kwetu ni axle 7 na urefu hautakiwi kuzidi mita 17!!! Put it simple: napokuwa na axle nyingi ndio unavyozidi kutetea barabara na the opposite is also true,

Ningekuwa mimi ndo Magufuli ningejiuliza swali moja -kwanini South Africa wanabeba mizigo mizito yet road network zao zina lifespan kubwa kuliko zetu na pia hawana idadi kubwa ya mizani kama sisi. Na bado wakifika Tunduma wanaona ni afadhali ku-offload mizigo na kupakia kwenye malori yetu??

Hivi kuna hasara gani TANROADS ikiruhusu axle 9 na urefu ukawa 22 metre! !! Kwanini Trailers za Interlink ambazo zinatuika karibu Africa nzima hapa kwetu ni marufuku? Remember: Australia wanabeba mpaka tani 80 kwa kuongeza idadi ya axle na kuto limit urefu! Na bado barabara zao zinadumu.
Ingekuwa hii post in ya siku hizi ungeitwa Chadema na mchochezi.
Kumbe watu walisha muona siku nyingi ni MTU was aina gani
 
Tuombe Mungu tuu Hans Pope asije pata mawazo yale ya 1981/82 alipokuwa na wenzake kina Kadego, Komando, Maganga nk.
Maana ile timu ingekuwa kwa sasa ambapo wale jamaa wa kwa Zakaria weledi wao unatia mashaka habari yaweza kuwa ya kuogofya
 
Nimesikia msemaji wa TAKUKURU redion jioni hii anasema huyo Hans Poppe anasakwa kwa tuhuma cjui ya nyasi za TFF na hajapatikana..
 
Back
Top Bottom