Hapa bongo kuna watu wanaishi kama Ulaya

Hapa bongo kuna watu wanaishi kama Ulaya

We bana kila mtu aenjoy alichonacho, nini Buza kuna siku nilikua masaki ya Chanika ndanindani huko kuna kakijiji kana nyumba kama tano tu lakini masela wapo nje kwenye viti vya magogo wamekaa wanapiga gongo yao kiroho safi tu halafu wamefurahi sana hadi nikawaonea wivu hilo life lao
👍👍🤣🤣
 
Usiumie sana ukasahau "Kuishi" endelea kufurahia maisha yako huku ukitafuta,


Usihuzunike sana coz humo ndani ya hizo nyumba hujui nao pia kuna matatizo yao wanayoyapitia,inaweza kua ni matatizo ya kiafya,kifamilia au matatizo mengine yeyote yale,

Usisubiri mpaka utimize jambo fulani ndio uwe na furaha,unaweza kutimiza jambo hilo kisha ukawa na furaha ila baadae ukaja kuona kua jambo hilo ni la kawaida tu,Siku zote omba afya njema na uzima huku ukiendelea kutafuta.
Awesome 👍
 
Kuna Mzee mmoja alikuwa anafanya kazi serikalini. Alikuwa mtu mkubwa kicheo.

Akawa kapandishwa cheo kikubwa kabisa kazini kwake.

Akapewa nyumba nzuri sana Oysterbay.

Karibu kabisa na ubalozi wa Marekani.

Watoto wake wakafurahi sana. Wakaona wanaenda kuhamia Oysterbay, tena karibu kabisa na Ubalozi wa Marekani.

Lakini, yule Mzee hakuwa mtu wa kupenda makuu.

Alisema anapapenda pale alipokuwa anaishi, maana pana sehemu kubwa, tena amezoeana sana na majirani. Wanaishi vizuri.

Zaidi, hakuona sababu za kuhamahama nyumba za serikali kwani alikuwa anakaribia kustaafu.

Watoto wake wakakasirika sana.

Wakasema Baba unaacha nafasi ya kuhamia Oysterbay, tena mtaa wa Laibon ukae jirani na rais Mwinyi na ubalozi wa Marekani?

Baba yao akasema ameshaamua.

Basi muda kidogo tu, ubalozi wa Marekani ukapigwa bomu. Ile nyumba ikapasukapasuka vibaya sana kwa sababu ilikuwa karibu sana na ubalozi wa Marekani.

Kama yule Mzee angehamia pale, familia yake ingeweza kuumia vibaya sana.

Watoto wale wakamuona yule mzee kama alikuwa na uwezo wa kuona yajayo.

Unaweza kutamani kitu kizuri, ukasononeka kukikosa.

Kumbe, usalama wako unakuja unapokikosa hicho kitu.

Ukikipata unapata balaa.
Exquisite 👍
 
Kawaida ya binadamu tuna hulka ya kutamani tusichokuwa nacho.

Umasikini ni kitu kibaya sana kakini kwenye maisha Amani ya Nafsi ni bora kuliko chochote.

Magufuli alikuwa anapenda kwenda kwake CHATO mara kibao ingawa angeweza kuishi Osterbay, Ikulu.

Prod Mwandosya kaamua kukaa kwake huko Mbeya ingawa anaweza kuishi Masaki.

Jambo la msingi ni kuishi sehemu inayokupa Amani.

Na watu wengine pia wanapenda kuishi na watu wanaofahamiana nao ( kijamaa ) maana wanasema zimwi likujualo halikuli likakwisha, siyo kama Osterbay kila mtu ndani ya geti zito lenye umeme.

Leo kina Akon wametafuta pesa US lakini wamerudi Senegal ambako wanaheshimika zaidi.
👍
 
Mimi nakumbuka wakati niko O-level mwanzoni nilikuwa nakaa na masela, msosi wa kugombania fujo nyingiii.

Sasa, kuna Mkuu mmoja wa Magereza akapenda sana nikaishi kwake: Kwanza kuna kuku wa mayai, mayai kila muda, baiskeli za gia kibao nikapewa za kuendea shule.

Lakini imagine, nilikuwa sina amani moyoni just from within ( for no reason) kabisa ikabidi nirudi kwa masela🤣
🤣
 
Kawaida ya binadamu tuna hulka ya kutamani tusichokuwa nacho.

Umasikini ni kitu kibaya sana kakini kwenye maisha Amani ya Nafsi ni bora kuliko chochote.

Magufuli alikuwa anapenda kwenda kwake CHATO mara kibao ingawa angeweza kuishi Osterbay, Ikulu.

Prod Mwandosya kaamua kukaa kwake huko Mbeya ingawa anaweza kuishi Masaki.

Jambo la msingi ni kuishi sehemu inayokupa Amani.

Na watu wengine pia wanapenda kuishi na watu wanaofahamiana nao ( kijamaa ) maana wanasema zimwi likujualo halikuli likakwisha, siyo kama Osterbay kila mtu ndani ya geti zito lenye umeme.

Leo kina Akon wametafuta pesa US lakini wamerudi Senegal ambako wanaheshimika zaidi.
Sahihi kabisa Mkuu.

Home is where the heart is,home is the feeling not a place.
 
Hahaha uliza wewe mkuu..hahaha hua nacheka sana aisee ukikutana na waliokata tamaa ya maisha au walioamua kua maskini ukikuta wanachoongea unaweza kuaga haraka na kuondoka kwa kasi, mtu anachamba na makaratasi anasema ameridhika na maisha, mtu mtoto wake kafa sababu alikosa shilingi elfu 10 ya kununua dawa anasema karidhika na maisha ya kifukara kwamba anashukuru kwa kila jambo, na ukikuta ni wamekaa kinyonge na nyimbo ni za dini za kulilia mateso shida, majonzi, machozi, n.k
Kwa hiyo matajiri hawaridhiki?!!

Kuridhika ndio utajiri mkubwa....
 
kule mbezi kwa zena kuna gari za kawaida kila aina bwana huyo asitutishe [emoji2][emoji2]
Sehemu ambapo kuna gari kali kali ni upanga tena ule mtaa wa Mindu kwenye Gorofa za minduplace nikiwa pale naenjoy sana.

Kwingine huku Toure Dr Masaki ukikaa hapa Cliffside Residence unaona Kwanzia gari kali/Sea Cliff Sea view safi kabisa
 
Back
Top Bottom