Hapa jirani yangu pana nyumba haijawahi kukaliwa na watu tokea ikamilike kujengwa. Ni mwaka wa 10 huu, mpaka geti linaanza kuoza. Nijitwalie?

Hapa jirani yangu pana nyumba haijawahi kukaliwa na watu tokea ikamilike kujengwa. Ni mwaka wa 10 huu, mpaka geti linaanza kuoza. Nijitwalie?

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Kuna nadharia mbili hapa.

1. Yawezekana mmiliki alikuwa anamjengea mchepuko. Ili siku moja aje amfanyie surprise. Lkn kabla ya surprise jamaa akapata ugonjwa ama ajali na kufariki. Kwahiyo si mchepuko wala familia waijuao nyumba hii.

2. Mmiliki alipoikamilisha alipigwa kifungo cha miaka 30 au zaidi jela.

Je, nijitwale hii nyumba? Vipi kama nadharia ya 2 ndiyo sahihi? Akitoka jela na kurudi uraiani itakuwaje? Ingawa kuna usemi wa kiswahili unanipa moyo "cha kuokota siyo cha kuiba, mwenye mali mpumbavu".
 
Ngoja niwape kisa kimoja

Kuna jamaa zangu Mzee wao alifariki akawa amewaachia nyumba za urithi, sasa baada ya miaka mingi kupita Kuna nyumba walikua wanaiuza. Katika kupekua mafaili wakampa mnunuzi document ili ajiridhishe. Yule mnunuzi kaenda ardhi anakuta ile document ni ya nyumba nyingine kabisa tofauti na ile aliyopanga kununua

Akajulisha jamaa wakamtaftia document sahihi wakafanya biashara. Sasa jamaa wakaanza kujiuliza hii document ya mara ya kwanza ni ya wapi mbona hii nyumba hatuijui. Wakafatilia kushirikiana na ardhi mpaka kwenye Hio nyumba, wakamkuta Mzee mmoja anaishi hapo baada ya kumhoji Mzee akadai alipewa Hio nyumba Aishi na Mzee mmoja ila ana miaka mingi hawajawasiliana na hajui hata yupo wapi.

Jamaa wakawa wamepata nyumba nyingine kilaini kabisa na hakuna aliyekua anaijua.
 
Mimi Nina nyumba miaka 5 sijawahi kwenda na ilikamilika haishi mtu yeyote!

Kwanini hujafikiria kuwa Mwenye nyumba yupo nje ya inchi? Umefikiria kuwa kafariki au yupo jela?
 
Utashangaa kuna watu wanaishi humo ila wewe huwaoni. Jichanganye
Hizi nyumba zione hivi! Hakuna kitu kinachotengenezwa kwa hela ndefu mpaka kukamilika kama nyumba! Ubora na mwonekano wa nyumba na mahali ilipo ndo thamani ya hela iliyotumika kuijenga.

Kwasababu hiyo nyumba haiwezi kukaa tupu! Kama sio watu wanaishi, basi ziko roho zinaishi mule! Mashetani nayo yanataka kuishi kwenye nyumba nzuri! Roho iliyokuwa nyuma ya upatikanaji wa hela na ujenzi wa hiyo nyumba ndo zinaishi mule! Jichanganye uingie uone mziki wake!
 
Hizi nyumba zione hivi! Hakuna kitu kinachotengenezwa kwa hela ndefu mpaka kukamilika kama nyumba! Ubora na mwonekano wa nyumba na mahali ilipo ndo thamani ya hela iliyotumika kuijenga! Kwasababu hiyo nyumba haiwezi kukaa tupu! Kama sio watu wanaishi, basi ziko roho zinaishi mule! Mashetani nayo yanataka kuishi kwenye nyumba nzuri! Roho iliyokuwa nyuma ya upatikanaji wa hela na ujenzi wa hiyo nyumba ndo zinaishi mule! Jichanganye uingie uone mziki wake!
Ni kweli kabisa mkuu
 
Back
Top Bottom