Kuna nyumba moja ilikua kando ya barabara mitaa fulani ambayo tulikua tukipita tukiwa wadogo. Kipindi hicho hiyo nyumba ilikua ina milango, madirisha ya vioo na kila kitu kama vile kuna watu wanaishi humo, ila hakukua na mtu. Sisi tulikua tukiambiwa nyumba hiyo ina majini, na enzi hizo tulikua tukipita hiyo njia tunarusha mawe juu ya bati na kukimbia!
Juzi nimepita hiyo mitaa, nikakuta ile nyumba imechakaa kabisa, nyasi ndefu zimeota, bati zimeezuliwa, vioo na madirisha yamevunjikavunjika, hakuna milango yaani zimebaki kuta tu zimesimama.. Kwakweli mpaka leo sijajua hii nyumba ilikua ya nani?