Hapa jirani yangu pana nyumba haijawahi kukaliwa na watu tokea ikamilike kujengwa. Ni mwaka wa 10 huu, mpaka geti linaanza kuoza. Nijitwalie?

Yaani hivyo tu ukamiliki ardhi?
Hii scenario nimeiona sio mbali sana na nilipo, jamaa amekuwa akilima hicho kiwanja, anapanda mihogo nk na vile amepakana na hicho kiwanja, naona kabisa akikimiliki kiulaini kabisa.
 
Kuna nyumba moja ilikua kando ya barabara mitaa fulani ambayo tulikua tukipita tukiwa wadogo. Kipindi hicho hiyo nyumba ilikua ina milango, madirisha ya vioo na kila kitu kama vile kuna watu wanaishi humo, ila hakukua na mtu. Sisi tulikua tukiambiwa nyumba hiyo ina majini, na enzi hizo tulikua tukipita hiyo njia tunarusha mawe juu ya bati na kukimbia!

Juzi nimepita hiyo mitaa, nikakuta ile nyumba imechakaa kabisa, nyasi ndefu zimeota, bati zimeezuliwa, vioo na madirisha yamevunjikavunjika, hakuna milango yaani zimebaki kuta tu zimesimama.. Kwakweli mpaka leo sijajua hii nyumba ilikua ya nani?
 
Unajifunza utapeli! Acha hizo, tafuta hela kijana wangu! Acha tamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…