Hapa jirani yangu pana nyumba haijawahi kukaliwa na watu tokea ikamilike kujengwa. Ni mwaka wa 10 huu, mpaka geti linaanza kuoza. Nijitwalie?

Hapa jirani yangu pana nyumba haijawahi kukaliwa na watu tokea ikamilike kujengwa. Ni mwaka wa 10 huu, mpaka geti linaanza kuoza. Nijitwalie?

Mkuu,

Fanya uokote tu hiyo nyumba, mbona hata Mzee Magu naye aliwahi kuokota ambulance pamoja na vichwa cha treni pale bandarini.

Bahati haiji mara mbili, fanya maamuzi usije ukajuta pale mwingine akaja kuokota.
 
Nyumba za namna hiyo zipo nyingi mno hasa jijini Dar es salaam.

Mahali ninapoishi,kuna nyumba zimejengwa kwa mfuatano zikiwa 3,inasemekana Mzee anao watoto 3 aliamua kuwajengea hizo nyumba,mzee alifariki ila madogo wapo wanaishi nje ya nchi!

Walikuja kipindi fulani( Zaidi ya mika 10 iliyopita) wakaangalia zile nyumba na mahali zilipo wakasema hawazihitaji!.

Kuna Sheikh mmoja ameamua kujimegea moja anaishi na familia yake,zile nyingine 2 zinazidi kuota nyasi tu na nyoka kujazana huko ndani!.

Nyumba ni nzuri na naza kisasa mno!,lakini madogo walisema hawawezi kuja kuishi Tanzania.

Sasa wenyeji kila mmoja anaogopa na kusema wanaweza kushitakiwa,lakini ukweli ni kwamba hakuna mtu wa kukushitaki wala nini!.

Ngoja nivute muda,mwakani nasafisha moja naingia,mdogo mdogo hadi inakuwa yangu!

Maana kwa dalili zilizopo hakuna wa kuhoji zaidi ya kuendelea kuchakaa!,Siku watu wa Ardhi wakishituka zitakwenda na maji!.

Mwakani najimilikisha moja!

Ina maana wameshindwa hata kuzipangisha
 
Kwa nyumba sijui ipoje ila kwa kiwanja afadhali
Mi nilijipatia kiwanja kwa namna hiyo
Kilikuwa ubavuni kwangu na mwenyewe hakuwahi kuonekana
Nikaenda ardhi nikawaeleza wakaniambia kasafishe kwanza ukiona kimya weka msingi tulia

Nilifanya hivyo na hakutokea mtu lakini palikuwa ma tofali 12 pale chini
Baada ya mwaka nikaenda ardhi nikawaeleza wakanipa offer/hati na hadi leo napamiliki
Dah Watu wanadhulumiwa Sana..
 
Dah Watu wanadhulumiwa Sana..
Kuna mahali nilienda kuangalia shamba. Sasa unakuta kichaka ukiuliza hapa vipi, unaambiwa pameuzwa. Sasa najiuliza hawa watu wakipokonywa watalalamika?

Kumiliki ardhi bila kufanya chochote ni makosa sana. Jitahidi hata upande miti ambayo haihitaji uangalizi
 
Kuna mahali nilienda kuangalia shamba. Sasa unakuta kichaka ukiuliza hapa vipi, unaambiwa pameuzwa. Sasa najiuliza hawa watu wakipokonywa watalalamika?

Kumiliki ardhi bila kufanya chochote ni makosa sana. Jitahidi hata upande miti ambayo haihitaji uangalizi
Ila muhimu kama shamba likatie Rizi tulia zako nyumbni watakuja wakitaka kumega we unawaacha tu
 
Mwaka 2009 tulienda na rafiki yangu Bunju kununua Viwanja,tukaanza kujenga mdogomdogo lakini rafiki yangu (RIP)alijenga fasta ikabaki kupaua tu(kumbuka wote tulikuwa mabachela). Siku moja anatoka site akapata ajali Tegeta(aligongana na Lori),alifariki palepale. Huyu rafiki yangu tulikuwa tumepanga nyumba moja Sinza(yeye Chumba chake,mimi changu lakini sebule,jiko nk tunashea. Tangu tunanunua Viwanja mpaka anafariki hakuna aliyewahi kumpeleka site ndugu,rafiki wala jamaa. Hivyo nyumba niliiokota kwa style hiyo,niliipaua,nikaifanyia finishing na sasa nakula Kodi. Lakini kwa kuwa tulikuwa tumeshibana sana hivyo huwa najitajidi kuwatumia Pesa Wazazi wake Moshi kila mwezi,na wamekuwa kama Wazazi wangu na wananiita mwanao.
SWALI KWA NINI SIKUIPA TAARIFA FAMILIA HIYO?huyu Marehemu rafiki yangu ndie aliyekuwa amesoma kwao,Kaka na Dada zake wote ni wale waleviwalevi waliojichokea tu,hivyo kama ningetoa taarifa naamini wangeshauri nyumba iuzwe tu wapate Pesa ya kunywea pombe. Tangu niikamilishe mwaka 2011 mpaka leo nakula Kodi tu,Hati nilishaipata kwa jina langu na maisha yanasonga.
Ndugu tambua marehemu huwa hadhurumiwi. Huyo rafiki yako anawazazi. Handover hiyo nyumba kwa wazazi ili ujitoe kwenye kalma. Kuna siku huyo marehemu rafiki yako atakuja kukuuliza kuhusu mali zake. Kuikamilisha bado hakukupi justification ya kuwa owner under that circumstance.
 
Back
Top Bottom