DOKEZO Hapa Morogoro kuna baadhi ya maeneo bei ya nauli ya bajaji imepanda mara 2 na maeneo mengine kwa nusu bei

DOKEZO Hapa Morogoro kuna baadhi ya maeneo bei ya nauli ya bajaji imepanda mara 2 na maeneo mengine kwa nusu bei

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Tanzania hii hasa Tanganyika hali ni tete kwa sasa nipo Morogoro, nashuhudia mashindan ya kupandisha nauli kwa vyombo vya usafirishaji huku wakida EWURA imepandisha bei ya mafuta, wapo waliopandisha hadi mara mbili ya bei ya zamani.

Wapo ambao walikuwa wanabeba abiria kwa 500 leo ni 1000 kwa eneo lilelile na huku wengine wakipandisha kutoka 1000 mpaka 1500 ikiwa ni ongezeko la nusu ya bei ya awali kwa baadhi ya maeneo kama kutoka hapa kwa Sanya kwenda mjini leo bajaji 1500 kutoka 1000 huku daladala zikipandisha mpaka 1000.

Hali hiyo ipo mpaka kwa bodaboda na daladala mji mzima.

Vipi huko kwenu nauli zinasomaje au madereva wa huko kwenu bado wana hofu ya Mungu?

Pia soma:
 
U.S na Israel ni superpower na zipo kwa ajili ya kupigania maslahi ya nchi masikini Ili ziishi kwa raha,ndio maana kabla ya wao kuanzisha vita,bei ya mafuta ilikua kubwa kuliko hii
 
Strait of Hormz effect. Vita vipambe moto japo kwa miezi 10 mbele ili tuone nchi zipi zitatepete kiuchumi na kuchochochea maandamano kutokana na kupanda ama kukosekana kwa mafuta.

Btw TIPPER bado wapo?
 
Mashabiki WA taifa teule SI WA mwombe Mungu WA israel alete mafuta ,hata hivyo tusijali mwamposa yupo ataombea Kila kitu kitakaa shwari. Wakati huo sisi wakatholiki tunaiombea Dunia amani ,Mungu awabariki sana wakatoliki Kwa kusimamia haki na amani
 
Kama umechoka kuona faida ya biashara yako ikiteketea kwenye vituo vya mafuta kila bei ya EWURA ikipanda, sasa ni wakati wa kuachana na mazoea na kuhamia OASIS Electric ambapo kwa Unit 3 tu za umeme (Tsh 1,100) unapata uwezo wa kutembea kilomita 130 bila hitaji la oil wala service za injini; karibu tukufanyie uchanganuzi wa bure wa jinsi unavyoweza kuokoa zaidi ya Tsh milioni 3.5 kwa mwaka kwa kila pikipiki moja na kuanza kumiliki faida yako halisi leo.

0685665582
 
Back
Top Bottom