Tanzania hii hasa Tanganyika hali ni tete kwa sasa nipo Morogoro, nashuhudia mashindan ya kupandisha nauli kwa vyombo vya usafirishaji huku wakida EWURA imepandisha bei ya mafuta, wapo waliopandisha hadi mara mbili ya bei ya zamani.
Wapo ambao walikuwa wanabeba abiria kwa 500 leo ni 1000 kwa eneo lilelile na huku wengine wakipandisha kutoka 1000 mpaka 1500 ikiwa ni ongezeko la nusu ya bei ya awali kwa baadhi ya maeneo kama kutoka hapa kwa Sanya kwenda mjini leo bajaji 1500 kutoka 1000 huku daladala zikipandisha mpaka 1000.
Hali hiyo ipo mpaka kwa bodaboda na daladala mji mzima.
Vipi huko kwenu nauli zinasomaje au madereva wa huko kwenu bado wana hofu ya Mungu?
Pia soma: