Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Abdallah Said alishafariki miaka mingi iliyopita kwa sasa wamebaki watoto wake...Yule tajiri Abdala Said wa pale Mwanga yupo.
Akili za kuambiwa changanya na zako,kuna watu humu wanauchafua mkoa wa Kigoma kwa chuki zao binafsi tu na kuwakatisha watu tamaa hata wasiende kutembea na kujionea mkoa wa Kigoma ulivyo.
Mimi ni mwenyeji wa Kigoma Mjini kabisa hivyo huwa nachukizwa na wapuuzi wachache wanaotuchafulia mkoa wetu kwa maneno ya kipumbavu yasio na ukweli wowote.
Kigoma kwa sasa imepiga hatua kubwa sana kwenye nyanja karibu zote, Elimu,Afya,miundombinu,Makazi,Biashara n.k ukilinganisha na zamani...ambapo tulitengwa na serikali kimaendeleo,Tumuombee mema bwana Kikwete kwa kuwa wakwanza kukumbuka kigoma na kutuweka kwenye ramani mpaka waliokuja baada yake kutupa kile alichokiandaa tukipate...maana tulikuwa mayatima tuliokosa faraja kutoka kwa walezi wetu.
Kwa mtu ambaye hajafika Mkoani Kigoma afike mwenyewe ajionee jinsi uasili wa mazingira ya Kigoma yalivyo naamini atapenda sana maisha ya mkoa huu yasiyokuwa na changamoto nyingi kwa mtu mwenye kipato cha wastani....mkoa huu ni sehemu nzuri ya kuishi kwa mtu yeyote yule aliyeamua kuishi hapa,binafsi nimeishi na wageni wengi kutoka mikoa mpaka nchi mbalimbali katika mkoa wa Kigoma tena miaka kumi nyuma na waliishi kwa furaha na amani tele wakiyafurahia maisha ya mkoa huu...japokuwa kwa sasa mkoa unaanza kufunguka kimaendeleo hii inatia moyo kwa wageni kukaribia hapa na kujionea yaliyomo yamo.
Kuna vitu ambavyo Kigoma vipo lakini kuna mikoa baadhi hakuna tena ni mjini kati kabisa...
Watu wa Kigoma ni watu wanaokwenda na wakati na ni wajanja....ukifika Kigoma usishangae kuona gari za kutembelea Jijini Dar au Mwanza ndio zinatumika kubeba abiria(Tax)..hii inaonyesha usiriasi wa watu wa Kigoma katika kufanya biashara zao,watu wanajituma kuwekeza katika kile wanachokifanya japo kuwa Mazingira yalikuwa hayaridhishi..
Wageni ni wengi sana Kigoma na wamehamia kabisa wanafanya harakati zao na wamehamia kabisa wamejenga huwaambia kitu kuhusu Kigoma ingekuwa ni sehemu mbaya kuna wachawi,Vumbi,wizi basi watu wasingetoka Moshi,Arusha,Dar,Morogoro,Mwanza,Dodoma,Mbeya,Mtwara,Zanzibar,Tanga wakaja kuishi Kigoma wanaongea kama wamekatwa vichwa waache mihemko isiyokuwa na tija....Kigoma ni mahali salama kwa yeyote kuishi na akapiga mishe zake kizawa kabisa.
Japokuwa huwezi kufananisha na majiji au miji mikubwa kutoka na naendelea kuchelewa lakini huku mambo yanaenda kama kawaida Biashara zipo(Kigoma-China),Mijengo mikali ya kishua ipo ya watu binafsi,sehemu za starehe zipo Beach kali,Hotel za maana,sijui Bar,Migahawa classic,Club zipo,vijana wadogo kumiliki pesa sijui magari wapo kama huko kwenu....karibu kila aina ya gari linalotoka Kigoma lipo watu wazito wapo...hivyo usipotoshwe au kupotosha wenzako.
Karibuni Kigoma mle samaki watamu,mafuta mazuri ya Mawese,mjifunike mashuka ya kufumwa,pia muone ukarimu na utu wa mkoa huu.
😂🤣😅😆😁😄😃😃Nyie watu wa kigoma mbona wachafu sana!fanya mkae mmalize tofauti yenu na maji kwanza ndio mtushauri tuje kutembea kigoma
Umepiga kwenye mshonoNyie watu wa kigoma mbona wachafu sana!fanya mkae mmalize tofauti yenu na maji kwanza ndio mtushauri tuje kutembea kigoma
Punguza kashfa.Nyie watu wa kigoma mbona wachafu sana!fanya mkae mmalize tofauti yenu na maji kwanza ndio mtushauri tuje kutembea kigoma
Uko sahihi Mamndenyi.Punguza kashfa.
Mikoa ya pembezoni imechelewa kwenye maendeleo ila siyo upaze sauti kipuuzi hivi.
Ni muda tu nao watatoboa ukizingatia Makamu katoka huko.