Hapa ndio Mwanga Kaskazini mkoani Kigoma

Hapa ndio Mwanga Kaskazini mkoani Kigoma

hii nchi inawatu wa hovyo sana,kumbe Kigoma iko vizuri namna hii na hamsemi,mmekazania kuitajataja Dodoma wee wakati Dodoma ni vumbi tupu!
 
Sasa unabishia tafiti!!!
Endelea kupiga kampeni upate maji




Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Sio kweli, kwasababu nyinyi mnachukua ukabila kana kwamba ndio utaifa. Waha sio Warundi wala Wamanyema sio wa Kongo. Wamanyema ni watu wa ujiji na kigoma mjini mkoani kigoma Tanzania ila wana asili ya Kongo
Mf. Wangoni watu wa Songea & Malawi ila wana asili ya Afrika ya kusini na Uswazi. Pia Wamasai wa Tanzania wana Asili ya Kenya, pia Wajaluo kabila la Tanzania pia wana asili ya Kenya. Hivyo ndivyo yalivyo na makabila ya Kigoma.
Leo Muha anaitwa Mrundi kisa tu ana ndugu Burundi, Leo Mmanyema anaitwa Mkongomani kisa tu ana ndugu Congo. hivi ni makabila mangapi yapo mpakani mwa Tanzania na wala hayabaguliwi kama haya ya kwetu Kigoma?

''Wadigo'' ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Tanga, pia wako Kenya wanapoishi upande wa Kusini wa mji wa Mombasa. Hawajawahi kusumbuliwa wala kuambiwa sio watanzania japokuwa wanazo familia huko Kenya.

''Wajaluo'' ni kabila hasa la Kenya. Wako pia Uganda ya mashariki na wachache wanaishi nchini Tanzania katika Mkoa wa Mara. Hawajawahi kusumbuliwa wala kuambiwa sio watanzania japokuwa wanazo familia huko Kenya.

''Wamasai'' ni kabila wazawa wa Afrika la watu wahamaji wanaopatikana Kenya na kaskazini mwa Tanzania. Hawajawahi kusumbuliwa wala kuambiwa sio watanzania japokuwa wanazo familia huko Kenya.

''Wamakonde'' ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Mtwara. Pia wako Msumbiji. Lugha yao ni Kimakonde. Hawajawahi kusumbuliwa wala kuambiwa sio watanzania japokuwa wanazo familia huko Msumbiji.

''Wanyakyusa'' ni jina kwa ajili ya watu wanaoishi kwenye wilaya ya Rungwe katika sehemu za kusini za Mkoa wa Mbeya (Tanzania) upande wa kaskazini ya Ziwa Nyasa. Lugha yao ni Kinyakyusa pia hupatikana Malawi huhesabiwa pamoja nao katika kundi lilelile. Hawajawahi kusumbuliwa wala kuambiwa sio watanzania japokuwa wanazo familia huko Malawi. Ila sisi huku Kigoma ndio mnaendelea kutubagua. Dhambi ya Ubaguzi ni mbaya itawarejea siku moja
Mkuu shukrani sana kwa ufafanuzi huu murua kabisa[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Endelea kupiga kampeni upate maji




Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Unahisi hii mada ina justify kutokuwepo warundi na wakongo Kigoma? Unahisi hii mada ina justify uhalali wa wewe kupinga tafiti?
 
Mwanga Kaskazini ni jina la kata ya Manisipaa ya Kigoma Ujiji katika Mkoa wa Kigoma, Tanzania

View attachment 2363747

Mandhari katika Kata ya Mwanga Kaskazini, Kigoma-Ujiji

View attachment 2363752

Mini mart katika Kata ya Mwanga Kaskazini, Kigoma-Ujiji

View attachment 2363753

Shule ya msingi Katubuka, Mwanga Kaskazini, wilaya Kigoma Mjini, mkoa Kigoma, Tanzania,
Katubuka, Mwanga kaskazini

View attachment 2363788

Kata zingine za Manisipaa ya Kigoma Ujiji - hapa Mkoani Kigoma ni pamoja na Bangwe | Buhanda | Businde | Buzebazeba | Gungu | Kagera | Kasimbu | Kasingirima | Katubuka | Kibirizi | Kigoma Mjini | Kipampa | Kitongoji | Machinjioni | Majengo | Mwanga Kusini | Rubuga | Rusimbi.
Karibuni Kigoma
Karibuni Maghararibi mwa Tanzania

View attachment 2363764
Jiji la Kigoma
 
Mwanga Kaskazini ni jina la kata ya Manisipaa ya Kigoma Ujiji katika Mkoa wa Kigoma, Tanzania

View attachment 2363747

Mandhari katika Kata ya Mwanga Kaskazini, Kigoma-Ujiji

View attachment 2363752

Mini mart katika Kata ya Mwanga Kaskazini, Kigoma-Ujiji

View attachment 2363753

Shule ya msingi Katubuka, Mwanga Kaskazini, wilaya Kigoma Mjini, mkoa Kigoma, Tanzania,
Katubuka, Mwanga kaskazini

View attachment 2363788

Kata zingine za Manisipaa ya Kigoma Ujiji - hapa Mkoani Kigoma ni pamoja na Bangwe | Buhanda | Businde | Buzebazeba | Gungu | Kagera | Kasimbu | Kasingirima | Katubuka | Kibirizi | Kigoma Mjini | Kipampa | Kitongoji | Machinjioni | Majengo | Mwanga Kusini | Rubuga | Rusimbi.
Karibuni Kigoma
Karibuni Maghararibi mwa Tanzania

View attachment 2363764
Kazura Mimba kwa kina Mwijaku sijasikia mbona
 
Wadada wa kigoma wamejaaliwa ngozi nzuri na nywele nzuri, sema tu wakapewa ufupi.
 
Mkuu, nchi hii haijafikia hatua hiyo, nchi hii inavyombo imara vya usalama na ukaguzi imara zaidi ya ujuavyo. Kigoma sio mkoa wenye mipaka peke yake, ipo mikoa mingi imepakana na nchi za jirani Tunduru kuna mpaka na nchi ya Malawi na Mozambique, Namanga imepakana na Kenya, Mutukula imepakana na Uganda, na Kigoma imepakana na Burundi na Congo kupitia ziwa Tanganyika kama ilivyo Zanzibar imepakana na Mombasa kupitia Bahari ya hindi, kama ilivyo mtwara imepaka na Comoro kupitia bahari ya hindi. Kwa hiyo kauli yako ya kusema kwamba Kigoma kuna wakimbizi haramu ni batili.
huko kote napajua vizuri sana ila mpaka wa Kigoma unao pakakana na nchi za Burundi na Kongo unaongoza kupitisha wahamiaji haramu zaidi na wengi wao wanaishi Kigoma bila kuwa na vibali.
Ukienda kibirizi utakutana na wavuvi wa kikongo kibao wanaishi hapo, waendesha bajaji wengi ni warundi, wakulima wa mashamba wengi ni warundi wote hao wanaishi kinyume kabisa.
 
Daah Kigoma bado sana labda fukwe za ziwa victoria na Gombe pekee.
Miji yao kuanzia kigoma mjini na wilaya zake hakuna mvuto kabisa.
Uvinza, Kasulu nk hakuna mvuto kabisa


Mvuto wa nini, wewe unataka Kigoma iwe na mvuto kama demu??!😏
 
Back
Top Bottom