sengobad
JF-Expert Member
- Aug 13, 2017
- 9,008
- 8,788
Migebuka kwa jina la kiswahili wanaitwajeKwasasa ni Migebuka 5-6-7 kwa Tsh 2,000/= Kutegemea na ukubwa wa Migebuka.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Migebuka kwa jina la kiswahili wanaitwajeKwasasa ni Migebuka 5-6-7 kwa Tsh 2,000/= Kutegemea na ukubwa wa Migebuka.
Yaani kwa ubishi na ujuwaji aise hao jamaa Ni kibokoKatubuka manguruweni..kibirizi..hakika kigoma pako vizuri nikipata nafasi nitarudi kuwasalimu ndugu zangu..ila punguzeni ujuaji na ubishi.
#MaendeleoHayanaChama
Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Daah Kigoma bado sana labda fukwe za ziwa victoria na Gombe pekee.Utalii upoje mtu akija kuzurura from Dar mfano 3 days.
Huwa wanaibishia hata saa hao jamaaYaani kwa ubishi na ujuwaji aise hao jamaa Ni kiboko
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Ni kweli kabisa kama kuna mkoa ambao umevamiwa na wahamiaji haramu basi Kigoma inongoza.Nilifanya tafiti kwa jamaa zangu 46 wanaoishi Kigoma, nikagundua 2 tu ndo walikuwa watanzania, 34 walikuwa warundi, na waliobaki walikuwa wakongo.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Kila baada ya nyumba 2 Kuna Mchawi
Nahitaji mke wa kuoa huko mkuu binti asizidi 27Mabinti wa huku ni wavumilivu, wachapakazi na wapole.
View attachment 2363913
Karibu ndugu, usisite kunitafuta nikupatie binti mzuri kwa ajili ya kuoa. Mwenye nidhamu na heshima
Niliwahi kusikia hadi VP wetu naye anatoka Burundi.Nilifanya tafiti kwa jamaa zangu 46 wanaoishi Kigoma, nikagundua 2 tu ndo walikuwa watanzania, 34 walikuwa warundi, na waliobaki walikuwa wakongo.
Kutoka kabila gani na mwenye sifa zipi unahitaji?Nahitaji mke wa kuoa huko mkuu binti asizidi 27
Bidhaa zote za kilimo zinapatikana huku ikiongozwa na mafuta ya mawese. Pia tunazo bidhaa za uvuvi ikiwemo dagaa wa Kigoma na samaki aina ya Migebuka.Ni bidhaa gani kubwa inayopatikana kigoma mkuu?????
Mkuu, nchi hii haijafikia hatua hiyo, nchi hii inavyombo imara vya usalama na ukaguzi imara zaidi ya ujuavyo. Kigoma sio mkoa wenye mipaka peke yake, ipo mikoa mingi imepakana na nchi za jirani Tunduru kuna mpaka na nchi ya Malawi na Mozambique, Namanga imepakana na Kenya, Mutukula imepakana na Uganda, na Kigoma imepakana na Burundi na Congo kupitia ziwa Tanganyika kama ilivyo Zanzibar imepakana na Mombasa kupitia Bahari ya hindi, kama ilivyo mtwara imepaka na Comoro kupitia bahari ya hindi. Kwa hiyo kauli yako ya kusema kwamba Kigoma kuna wakimbizi haramu ni batili.Ni kweli kabisa kama kuna mkoa ambao umevamiwa na wahamiaji haramu basi Kigoma inongoza.
Wakongo na waburundi wanaishi kigoma bila hata kuwa na vibali jambo ambalo linahatarisha usalama wa wananchi na nchi kwa ujumla.
Sio kweli, kwasababu nyinyi mnachukua ukabila kana kwamba ndio utaifa. Waha sio Warundi wala Wamanyema sio wa Kongo. Wamanyema ni watu wa ujiji na kigoma mjini mkoani kigoma Tanzania ila wana asili ya KongoNilifanya tafiti kwa jamaa zangu 46 wanaoishi Kigoma, nikagundua 2 tu ndo walikuwa watanzania, 34 walikuwa warundi, na waliobaki walikuwa wakongo.
Vipi hapo Ugweno takwimu zinasomajeKila baada ya nyumba 2 Kuna Mchawi
Sasa unabishia tafiti!!!Sio kweli, kwasababu nyinyi mnachukua ukabila kana kwamba ndio utaifa. Waha sio Warundi wala Wamanyema sio wa Kongo. Wamanyema ni watu wa ujiji na kigoma mjini mkoani kigoma Tanzania ila wana asili ya Kongo
Mf. Wangoni watu wa Songea & Malawi ila wana asili ya Afrika ya kusini na Uswazi. Pia Wamasai wa Tanzania wana Asili ya Kenya, pia Wajaluo kabila la Tanzania pia wana asili ya Kenya. Hivyo ndivyo yalivyo na makabila ya Kigoma.
Leo Muha anaitwa Mrundi kisa tu ana ndugu Burundi, Leo Mmanyema anaitwa Mkongomani kisa tu ana ndugu Congo. hivi ni makabila mangapi yapo mpakani mwa Tanzania na wala hayabaguliwi kama haya ya kwetu Kigoma?
''Wadigo'' ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Tanga, pia wako Kenya wanapoishi upande wa Kusini wa mji wa Mombasa. Hawajawahi kusumbuliwa wala kuambiwa sio watanzania japokuwa wanazo familia huko Kenya.
''Wajaluo'' ni kabila hasa la Kenya. Wako pia Uganda ya mashariki na wachache wanaishi nchini Tanzania katika Mkoa wa Mara. Hawajawahi kusumbuliwa wala kuambiwa sio watanzania japokuwa wanazo familia huko Kenya.
''Wamasai'' ni kabila wazawa wa Afrika la watu wahamaji wanaopatikana Kenya na kaskazini mwa Tanzania. Hawajawahi kusumbuliwa wala kuambiwa sio watanzania japokuwa wanazo familia huko Kenya.
''Wamakonde'' ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Mtwara. Pia wako Msumbiji. Lugha yao ni Kimakonde. Hawajawahi kusumbuliwa wala kuambiwa sio watanzania japokuwa wanazo familia huko Msumbiji.
''Wanyakyusa'' ni jina kwa ajili ya watu wanaoishi kwenye wilaya ya Rungwe katika sehemu za kusini za Mkoa wa Mbeya (Tanzania) upande wa kaskazini ya Ziwa Nyasa. Lugha yao ni Kinyakyusa pia hupatikana Malawi huhesabiwa pamoja nao katika kundi lilelile. Hawajawahi kusumbuliwa wala kuambiwa sio watanzania japokuwa wanazo familia huko Malawi. Ila sisi huku Kigoma ndio mnaendelea kutubagua. Dhambi ya Ubaguzi ni mbaya itawarejea siku moja
Tuwekee na msikiti wa wakristoNimeitaja Boss, sema nimeandika Kitongoji badala ya Kitongoni. Huu ndio msikiti wa Waislamu Kitongoni - Ujiji
View attachment 2363865