VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Kila anapopita, hujieleza. Tena ni mambo yaleyale aliyoyahubiri na kuyatajataja kwa miaka yake yote mitano madarakani: ujenzi wa reli, ujenzi wa bwawa la umeme, barabara, zahanati, madaraja na kufuta ada za shule za msingi hadi kidato cha nne. Hana jipya katika sera zake. Hana mipango mipya kuelekea 2025. Ndiyo maana ametamka kuwa miaka mitano hii iliyopita ilikuwa ni onjaonja tu, yenyewe inakuja. Nani, mwenye utimamu wa akili na mwili, ataitaka hali iliyopo iendelee?
Katika kauli zake (mfano ya jana kule Ikungi, Singida), Dr. Magufuli amekuwa akizungumza kana kwamba yeye si mgombea wa Urais ila Rais 'anayeendelea' bila kuzingatia matokeo ya mwisho ya kura za Urais zitakazopigwa Oktoba 28. Kwa mfano alisema eti (Lissu) anagombea Urais ambao hatashinda! Yeye, kama mgombea, anajuaje kama Lissu hatashinda? Yeye, kama mgombea, anamjua mshindi wa uchaguzi huu tayari? Amejuaje?
Dkt. Magufuli anapaswa kuuvaa 'ugombea' zaidi ya Urais. Anapaswa, pamoja na kuwa bado yuko madarakani, kusema amefanya nini; amefanikiwa katika nini; ameshindwa katika nini na atarekebishaje aliposhindwa. Si sawa hata kidogo kuongea kana kwamba LAZIMA ASHINDE. Watanzania wanaweza kumchagua mgombea mwingine kwa kura zao. Wanaweza kuvutiwa na mwingine katika sera hata kama hakuna hela.
Mgombea ajinadi kwa sera zake na si mikwara yake!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kasulu, Kigoma)