Uchaguzi 2020 Hapa ndipo anapokosea Dkt. John P. Magufuli. Kwasasa yeye ni 'mgombea zaidi' kuliko Rais

Uchaguzi 2020 Hapa ndipo anapokosea Dkt. John P. Magufuli. Kwasasa yeye ni 'mgombea zaidi' kuliko Rais

Anajua na uhakika atasaidiwa kura ziibiwe ili atangazwe! Safari hii asijaribu.Aaanze kuchimba makaburi ya halaiki yatusubiri.Na asisahahau wale jamaa ICC toka The Hague wapo
mjini wakicompile datas!
 
Kwa mfano alisema eti (Lissu) anagombea Urais ambao hatashinda! Yeye, kama mgombea, anajuaje kama Lissu hatashinda? Yeye, kama mgombea, anamjua mshindi wa uchaguzi huu tayari? Amejuaje?
Mkuu huyu jamaa anajua kabisa kwamba hatashinda ktk sanduku la kura. Hivyo anategemea zaidi magumashi ya wakurugenzi na vyombo vya dola.
 
Rais wa Tanzania ni Mhe. Dr. Magufuli.

VUTA-NKUVUTE , Kama huelewi hilo rudi tu shule ukasome upya tena.
 
Acha kukariri bali fikiria kabla ya kuandika ngonjera zako hapa. Sasa kama unasema shughuli za Rais zinasimamishwa hapo kuna Rais? Narudia tena kwa Mujibu wa Katiba yetu hakuna hata sekunde moja ambapo Rais anakuwa hayupo katika nchi. Shughuli zake zinaendelea kama kawaida. Katibu Mkuu Kiongozi hawezi kufanyakazi kama Rais hata siku moja. Kuhusu CDF mambo ya kijeshi achana nayo huyajui kabisa hangaika na siasa uchwara tu.
Naomba unionyeshe wapi nimeandika neno zinasimamishwa?.
 
Acheni kudanganyika na mikusanyiko mnayoiona.. Katika jiji kama Mza lenye wakazi milioni mbili, watu wazima wakiwa takrabin 1.5M, CHADEMA ikikusanya watu elfu 20, hao ni sawa sawa na 1.5%. Kwa hiyo huwezi isemea 98.5% ambayo haijafika kwenye mkutano wa Lissu ina maamuzi gani.
Wakiwa watu ni wachache mnasema ooh hawako tayari kitawala nchi pakitokea nyomi la Nguvu oooh msidanganyike na mafuriko yani mpo Kama mwanamke aliyetungwa mimba nje ya mfuko wa uzazi...nyambafu tulieni mlisema upinzani umekufa Sasa Nini kulia
 
Watumishi wa Tume ya UCHAGUZI wote ni WATEULE WAKE.

Wasimamizi wa Uchaguzi wote ni WATEULE WAKE.

Viongozi wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, wote ni Wateule wake.

Mishahara anawalipa yeye, magari mazuri amewapa yeye.

Halafu wawatangazie WAPINZANI ushindi!!!!!!!!!!!!.

AMEJIHAKIKISHIA USHINDI.
Kama akishinda kihalali tutavumilia miaka mingine mi-5 ya msoto, ila akishindwa akubali tuu, asije akamwaga damu kwa kung'ang'ania madaraka sababu hata Lissu naye ni kama mbogo aliyejeruhiwa, simuoni akikubali kudhulumiwa kirahisi ushindi.
 
Mkuu, opinion polls zinaonesha CCM (Magu) itashinda kwa kishindo uchaguzi huu.. Makadirio yakiwa ni ushindi wa zaidi ya 90%.
Wanaofanya real opinions polls walishashughulikiwa zamani, wa mwisho kula kibano walikuwa TWAWEZA, sasa sijui wewe umeota wapi?
 
Acheni kudanganyika na mikusanyiko mnayoiona.. Katika jiji kama Mza lenye wakazi milioni mbili, watu wazima wakiwa takrabin 1.5M, CHADEMA ikikusanya watu elfu 20, hao ni sawa sawa na 1.5%. Kwa hiyo huwezi isemea 98.5% ambayo haijafika kwenye mkutano wa Lissu ina maamuzi gani.
Ukisema jiji lina watu 1.5m it means watoto, wazee na vijana. Watoto, under 18 years unaweza kukuta ni 45 to 50 %, hivyo wanaozungumzuwa hapa ni watu wazima above 18 yrs, so hiyo % ni ya hao wenye uwezo wa kuja mikutanoni.
 
Sawa sawa kabisa ni kweli Rais Magufuli ndiye Rais wa JMT hadi hapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi itakapotangaza mshindi wa kinyan'ganyiro hiki, hapo baada ya 28/10/2010. Kwa mantiki hiyo anafanya na kusema yote kama Rais wa JMT na kwa kofia ya sasa ya Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, ndiyo maana unamsikia akiomba kura kutoka kwa wananchi. Hukumsikia akifanya kazi ya kura siku za nyuma before 29/08/2020. Hebu nieleze kwa nini CHADEMA wanamuita Lissu "rais" pale wanapomkaribisha kuhutubia na kuomba kura kwa wananchi? Hili analifanya sana Freeman Mbowe. Kwa nini? Naomba kuelimishwa.
 
Hana washauri wa kumpangia hoja nzito za kampeni? Toa majibu mazuri juu ya malaalmiko ya wananchi ambayo ni KEY.
1. Hali ngumu ya Maisha,
2. Watu kupotea potea na kutishwa tishwa
3. Ajira kwa Vijana hasa kwa hawa graduates wanaozagaa mabarabarani.
4. Nini hatima ya Rasimu ya Katiba iliyopo kabatini.

Haya ndiyo mambo ambayo unawaambia watu in next 5 years what will be a way forward.
 
Hahaha Hapa ni TANZANIA sio lazima Wa USA na WARUSSIA wasemee wao ya kwaooo THIS IS BLACK NATION Tnakwenda na Yetu
Yaani hata swali langu hujaliona!? Kweli vilaza hamtaisha JF.
Hizo polls zimeendeshwa na taasisi gani?
 
Mkuu, opinion polls zinaonesha CCM (Magu) itashinda kwa kishindo uchaguzi huu.. Makadirio yakiwa ni ushindi wa zaidi ya 90%.
Opinion poll ya mwisho ya Twaweza miaka 3 iliyopita aliporomoka mpaka 65% mpaka yule Mkuu Bw. Eyakuze akajikuta matatani na kunyang'anywa Hati yake ya Kusafiria kungojea kukamilika uchunguzi wa Uraia wake. Matokeo ya uchunguzi ule hadi leo hayajawekwa wazi na hatma ya Twaweza na alipo Eyakuze hakuna habari yoyote. Taasisi iliyoendesha Opinion Poll iliyopandisha makadirio kufika 90% ingetajwa usije na wewe ukanyang'anywa Passport yako kama unayo na Uraia wako kuhojiwa kwa sababu CCM Mara nyingi wamesema mgombea wao atapita kwa asilimia 99%. Kaa chonjo hata kama wewe ni CCM!
 
Opinion polls zimefanywa na nani?
Hapa Russia tuna the Levada Center,wao wana reputation nzuri kuhusu researches & polls.
USA kuna Gallup,YouGov na wengine wanaotambulika.
Hao waliofanya opinion polls ya 90% ni nani?
Nadhani ni Umoja wa Vijana bila Marinda bila Vaseline lumumba gov
 
Mkuu, opinion polls zinaonesha CCM (Magu) itashinda kwa kishindo uchaguzi huu.. Makadirio yakiwa ni ushindi wa zaidi ya 90%.
Opinion polls za wapi? Tuna sheria ya takwimu, zimeidhinishwa wapi hizo poll? JPM yuko kwenye wakati mgumu sana uchaguzi huu...he is going to be a first president with only first term in Tanzania amini au usiamini!
 
Jana katoa amri zahanati ijengwe Singida na ataenda kuzindua mwezi wa 11 sasa kama nayeye nimgombea unatoaje ahadi kuwa kianze kujengwa katikati ya kampeni hio sirushwa?.

Hiyo ni RUSHWA TU. Takukuruuuuuu![emoji79][emoji79]
 
Back
Top Bottom