Uchaguzi 2020 Hapa ndipo anapokosea Dkt. John P. Magufuli. Kwasasa yeye ni 'mgombea zaidi' kuliko Rais

Mshamba tu

Ccm Zanzibar inatia huruma .
Mgombea Urais Wanapewa
Wabunge wanapewa
Hata wawakilishi wanapewa kutoka Dodoma.

Tukumbuke ASP+TANU =CCM
Lakini Zanzibar hawezi kutoa M/Kiti wala SG

Kuna Makamu Wenyeviti 2

Akifa M/Kiti wao wa taifa anachukua nafasia Makamu wa Bara Ccm
Kwa ufupi Ccm Zanzibar Kama Tawi la Ccm Mtwara.

Wanzazibar hamkeni.
 
Hivi unafikiri Kuna mtu hapo ? Tanzania hatuna tiss Mpaka jiwe kawa presidaa ,ukipewa stori zake huna hamu .
 
Mkuu, opinion polls zinaonesha CCM (Magu) itashinda kwa kishindo uchaguzi huu.. Makadirio yakiwa ni ushindi wa zaidi ya 90%.

Hakuna opinion polls zinazoruhusiwa Tanzania, wewe uliona wapi?

Eeh?

Uliona wapi?????
 
Watumishi wa Tume ya UCHAGUZI wote ni WATEULE WAKE.

Wasimamizi wa Uchaguzi wote ni WATEULE WAKE.

Viongozi wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, wote ni Wateule wake.

Mishahara anawalipa yeye, magari mazuri amewapa yeye.

Halafu wawatangazie WAPINZANI ushindi!!!!!!!!!!!!.

AMEJIHAKIKISHIA USHINDI.

Sio ‘YEYE’.. yote hayo anayafanya kwa kodi zetu sisi. Hatoi hizo gari na hela huko mfukoni kwake. Ajue kuwa yuko pale kwa sababu yetu sisi wananchi. Na anatoka huyu October.. tushachoka kumuelewesha mtu kila siku kuwa yeye ni muwakilishi wetu tu pale kwenye kile kiti, sio ‘master’ wetu. Kila kitu anajivika nacho uhusika.. ‘changu’, ‘mimi’.. Amejisahau sana kama ni mtumishi tu. Aende akapumzike sasa huko Chato.
 
Kila anapopita, hujieleza. Tena ni mambo yale yale aliyoyahubiri na kuyatajataja kwa miaka yake yote mitano madarakani: ujenzi wa reli, ujenzi wa bwawa la umeme, barabara, zahanati, madaraja na kufuta ada za shule za msingi hadi kidato cha nne. Hana jipya katika sera zake. Hana mipango mipya kuelekea 2025. Ndiyo maana ametamka kuwa miaka mitano hii iliyopita ilikuwa ni onjaonja tu, yenyewe inakuja. Nani, mwenye utimamu wa akili na mwili, ataitaka hali iliyopo iendelee?

Katika kauli zake (mfano ya jana kule Ikungi, Singida), Dr. Magufuli amekuwa akizungumza kana kwamba yeye si mgombea wa Urais ila Rais 'anayeendelea' bila kuzingatia matokeo ya mwisho ya kura za Urais zitakazopigwa Oktoba 28. Kwa mfano alisema eti (Lissu) anagombea Urais ambao hatashinda! Yeye, kama mgombea, anajuaje kama Lissu hatashinda? Yeye, kama mgombea, anamjua mshindi wa uchaguzi huu tayari? Amejuaje?

Dkt. Magufuli anapaswa kuuvaa 'ugombea' zaidi ya Urais. Anapaswa, pamoja na kuwa bado yuko madarakani, kusema amefanya nini; amefanikiwa katika nini; ameshindwa katika nini na atarekebishaje aliposhindwa. Si sawa hata kidogo kuongea kana kwamba LAZIMA ASHINDE. Watanzania wanaweza kumchagua mgombea mwingine kwa kura zao. Wanaweza kuvutiwa na mwingine katika sera hata kama hakuna hela.

Mgombea ajinadi kwa sera zake na si mikwara yake!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kasulu, Kigoma)
Lumumba imejaa watu wa aina gani?
 
Jana katoa amri zahanati ijengwe Singida na ataenda kuzindua mwezi wa 11 sasa kama nayeye nimgombea unatoaje ahadi kuwa kianze kujengwa katikati ya kampeni hio sirushwa?.
Ataendelea kuwa Rais mpaka hapo Rais mwingine ataapishwa
 
Kila anapopita, hujieleza. Tena ni mambo yale yale aliyoyahubiri na kuyatajataja kwa miaka yake yote mitano madarakani: ujenzi wa reli, ujenzi wa bwawa la umeme, barabara, zahanati, madaraja na kufuta ada za shule za msingi hadi kidato cha nne. Hana jipya katika sera zake. Hana mipango mipya kuelekea 2025. Ndiyo maana ametamka kuwa miaka mitano hii iliyopita ilikuwa ni onjaonja tu, yenyewe inakuja. Nani, mwenye utimamu wa akili na mwili, ataitaka hali iliyopo iendelee?

Katika kauli zake (mfano ya jana kule Ikungi, Singida), Dr. Magufuli amekuwa akizungumza kana kwamba yeye si mgombea wa Urais ila Rais 'anayeendelea' bila kuzingatia matokeo ya mwisho ya kura za Urais zitakazopigwa Oktoba 28. Kwa mfano alisema eti (Lissu) anagombea Urais ambao hatashinda! Yeye, kama mgombea, anajuaje kama Lissu hatashinda? Yeye, kama mgombea, anamjua mshindi wa uchaguzi huu tayari? Amejuaje?

Dkt. Magufuli anapaswa kuuvaa 'ugombea' zaidi ya Urais. Anapaswa, pamoja na kuwa bado yuko madarakani, kusema amefanya nini; amefanikiwa katika nini; ameshindwa katika nini na atarekebishaje aliposhindwa. Si sawa hata kidogo kuongea kana kwamba LAZIMA ASHINDE. Watanzania wanaweza kumchagua mgombea mwingine kwa kura zao. Wanaweza kuvutiwa na mwingine katika sera hata kama hakuna hela.

Mgombea ajinadi kwa sera zake na si mikwara yake!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kasulu, Kigoma)

Tusishangae katumbua mtu kwenye mikutano yake ya kampeni.

Huku si kuchanganyikiwa peke yake.

Kale kaukichaa alikokasema mwenyewe kanaweza si ka kufumbia macho.
 
Back
Top Bottom