Hapa ni Gbadolite, Kijijini kwa dikiteta Mobutu Sesseko Kuku Wazabanga, nyumba zimegeuka Magofu na mahame


Unachosema ni kweli, kua Chato inazdiwa na sehemu kadhaa kwa vivutio na fursa mbalimbali.

Je, tatzo ni Chato kupendelewa na sio sehemu zingne? Na kwa nn sehemu duni kama Chato kujengwa miundombinu mikubwa kama miji mingine?

Lkn kwenye hoja za msingi za maendeleo ya kiuchumi lazma maeneo duni kuimarishwa ili kuleta unafuu wa maisha na kuondoa uchumi kutoka kutegmea sekta moja"economic diversification"

Sasa basi kama tutaendelea kujenga tu Dar, Mwanza, Mbeya n.k ni lini basi maeneo maskini kama Chato, Songea, Rukwa n.k nayo yataboreshwa?

Je ww wasemaje kwa hili?
 
Jana kuna mtu alizungumzia habari kama yako.

Walielezea Nyerere alivyokataa kujenga barabara ya lami kwenda Butiama, kwa kuuliza "Butiama kuna zao gani?".

Uchumi ni somo la kujua kupanga mambo ili kutumia rasilimali vizuri kabisa.

Kila sehemu ya Tanzania inastahili kuendelezwa.

Lakini, kuna sehemu nyingine zinastahili kupewa kipaumbele kwanza, kwa sababu, ukiziendeleza hizo, zinaleta kitu kinaitwa "multiplier effect".

Kwa mfano, ukiwa na sehemu ina machimbo ya dhahabu, na sehemu nyingine ina mihogo tu, under ceteris paribus, ina make sense kuanza kujenga barabara ya lami kwenda kwenye machimbo ya dhahabu.

Ukipeleka lami kwanza kwenye machimbo ya dhahabu, hiyo lami inaweza kuzalisha na kukuwezesha kuweka lami sehemu kumi zinazolima mihogo.

Ukijenga kwanza kwenye mihogo, ukaacha kwenye dhahabu, hiyo hela haitarudishwa, mihogo haina multiplier effect.

Wananchi wote wanastahili kupelekewa maendeleo. Tatizo, kwa nchi yenye bajeti finyu na macho mengi yanayoiangalia bajeti hiyo finyu, utaanza kujenga wapi ili ujenzi wako uwe na manufaa mengi zaidi kwa watu wengi zaidi? This is the utilitarianism I was talking about. The greater good for the greater number of people.

Ndiyo maana Nyerere alipoambiwa apeleke lami Butiama, aliyliza, Butiama kuna zao gani?

Ukikubali kwamba Chato haipo nafasi ya kwanza kiuchumi kujenga airport, umekubali kwamba kujenga airport hapo si uamuzi mzuri kiuchumi.
 
Charity begins at home! Uzuri ni kuwa chato ipo Tanzania! Kama malalamiko yanayoelekezwa kwa Mkuu yanalenga kutuaminisha kuwa Chato hapana hadhi katika Tanzania, ama basi yaliyofanywa huko yalipaswa kufanyika kaskazini tu itakuwa ni kumuonea mkuu.
Usitetee ujinga Angeliona aibu kidogo akafanya hayo Geita makao makuu ya mkoa
Kiserikali
 
Usimfananishe Mtukufu Rais na mambo yako yakipumbavu..

Hii ni Tanzania sio kongo wewe kilaza, kama unapapenda kongo hamia huko
Mtukufu ni Mungu Mwenyezi pekee magufuli ni wakala wa shetani na nyie ndo misukule yake iliyokatwa ulimi
 
Siungi mkono any kind ya fraud ila nnauliza hivi Chato sio Tanzania? Inamaana mtu akishakua kiongozi haruhusiwi hata kuchimba choo kwao?
Kwani magufuli kachimba choo au kajenga uwanja wa ndege?
 
Haina shida nyumbani kwanza ata mimi naanza nyumbani hili hiwe mfano nyote mkipata mkumbuke kwenu ndio nchi itaendelea
Kwahiyo kwa kujenga uwanja wa ndege kijijini chato ndo nchi imeendelea?
 
Wa Afrika mnalana akili Zero kwanini wasingeigeuza kuwa hotel na uyo uwanja ukatumiwa kwa Mambo mengine kama Mali ya selikari
 
Ukabila ndio umasikini wako.
 
Charity begins at home! Uzuri ni kuwa chato ipo Tanzania! Kama malalamiko yanayoelekezwa kwa Mkuu yanalenga kutuaminisha kuwa Chato hapana hadhi katika Tanzania, ama basi yaliyofanywa huko yalipaswa kufanyika kaskazini tu itakuwa ni kumuonea mkuu.

Hata huo uwanja wa ndege kijijini kwa Mobutu ilikuwa ni Zaire pia.
 

Kwani hicho kitendo cha wabunge kutumia pesa za umma kwenda kushangilia timu ya taifa kimesifiwa, mpaka uone hicho kitendo cha ubinafsi wa rais ndio kinapigiwa kelele tu?
 

Hua naamini waafrika tukibebwa kama tulivyo tukapelekwa US na US wakabebwa kama walivyo wakaletwa africa haitapita mwezi tutakuja kuomba msaada Africa tena msaada wa tech mpya kutoka Africa manake hizo za tutakazokuta kule tutaua ndani ya mwezi
 
Heshima kwako mkuu.

Umechambua vizuri sana. Na hivi ndivyo twapaswa kuelezea mambo kuonesha pros and cons za miradi, na sio kishabiki kam wengi tunavyokua tunafanya. Kwamba kisa mm nimezaliwa Mbeya nikijenga Mbeya nimepapendelea.


Walielezea Nyerere alivyokataa kujenga barabara ya lami kwenda Butiama, kwa kuuliza "Butiama kuna zao gani?".

Nyerere katika kipindi chake na mazingira ya nchi yetu ilikua tofauti sana.
1. Miundombinu ilikua mibovu na duni sana i.e barabara za mikoa na miko, wilaya na wilaya n.k, umeme, maji, hospital.

2. Elimu kwa watz; majority walikua hawana elimu. Ndo maana Nyerere alijikita sana kueneza elimu kufuta ujinga.
3. Uwezekaji ulikua mdogo sana na wengi walikua kwenye "Subsistence economy"

Kwa hiyo ni vigumu sana kufananisha mazingira ya nyerere na hali ya sasa.
Lakini, kuna sehemu nyingine zinastahili kupewa kipaumbele kwanza, kwa sababu, ukiziendeleza hizo, zinaleta kitu kinaitwa "multiplier effect".

Miji kama Mwanza, Geita na nchi ya Rwanda ni fursa kubwa kwa maeneo mingine ya jiran kibiashara. Hiyo miji ina watu wengi na ili kuendeleza biashara ndani ya hii miji inahitajika iwepo miji mingine maeneo jirani ya kibiashara ili uchumi wa ukanda husika uweze kua na "Multiplier effect....la sivyo biashara itajikuta ni Mwanza na Dsm,Mbeya, n.k
Ingawa mhe.alitakiwa pia aiangalie miji kama Musoma, Ngara, Biharamulo, Sirari, Shinyanga, Nyamongo, n.k ili kuhamasisha biashara na mji wake wa chato.

Mfano mji wa nyamongo, Geita, n.k una madini mengi sana angeboresha miundombinu na viwanja vya ndege ili kuleta ushindani ktk huo ukanda.




Kuna mdau humu ndani aliwahi kuleta mada kuhusu maendeleo kikanda akishauri ukanda flani ujitegemee wenyewe kimaendeleo kulingana na maliasili za ukanda husika. Yaani ukusanyaji kodi, allocation of resources etc visimamiwe na mamlaka (halimashauri) za ukanda huo.
Mfano Mwnza, Mara, Kagera, Geita (Ukanda wa ziwa) viwe na mamlaka ya ukusanyaji wa kodimgawanyo wake. Vivyo Hivyo kwa kanda zingne, pia kuwe na fungu la kwenda serikali kuu. serikali kuu ikiwa ni mshauri na pengme kuingila pale panapostahili.

Lkn hili kwa sasa naona linafanyika indirectly kwan kama maeneo duni katka ukanda flan yanajengwa na kuimarisha ni hatua nzuri ya kuelekea point ya maendeleoya ushindani kikanda.

Wito tu sheria na taratibu zifuatwe ktk allocation of Scarce resources we have, na haki itendeke.
 
Mleta mada naona unaendana na ule msemo wa dua la kuku halimpati mwewe.

Huwezi kumlinganisha Mobutu na JPM, ni watu wawili tofauti kabisa katika suala la maono yao.

Andika vitu kwa facts sio unaongea kama upo kijiweni. Huyu mtoa mada ameweka mpaka vielelezo vya picha. Na wewe tupe facts zako
 
Pale mwz ile airport ni kichekesho aiseee.
Mi najiuliza hizi pesa kwanini zisingepelekwa kuboresha uwanja wa ndege wa Mwanza,uwanja wa ndege wa Mwanza hauna hata jengo la Abiria yaaani ni kubanana tu
 
Neutral observers kwa kiswahili fasaha tunawaita ni 'wanafiki daraja la kwanza'.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…