Hapa ni Gbadolite, Kijijini kwa dikiteta Mobutu Sesseko Kuku Wazabanga, nyumba zimegeuka Magofu na mahame

Hapa ni Gbadolite, Kijijini kwa dikiteta Mobutu Sesseko Kuku Wazabanga, nyumba zimegeuka Magofu na mahame

Ukweli ni kuwa Chato haikustahili uwanja wa ndege wa hadhi hiyo, ni matumizi mabaya ya raslimali na madaraka. Namuunga mkono JPM ktk mengine lkn si katika hili.

Ingekuwa heri kama huo uwanja ungejengwa makao makuu ya mkoa-Geita, sio wilayani. Kwa kuujienga huo uwanja Chato, maana yake ni kwamba Geita Halmashauri, haitakaa ipate uwanja wa ndege wa maana. Ni heri makao makuu ya Geita yahamie Chato. BTW, baada ya huo uwanja, sasa wawajengee Bandari.

Vv
Kwani KIA ipo mjini Arusha ama Mjini Moshi? Vuta taswira wakati ikijengwa yale maeneo yalikuwaje!! Lakini kwa nini tusitazame uwepo wa Burundi, Congo, Rwanda, Uganda nk kama maeneo muhimu yanayoweza kutengenezewa linkage nzuri na uwanja huu. Kwani ni lazima kila kitu kilete faida leo leo? Kabla ya Chato si kulikuwa na mpango wa kujenga uwanja kama huo kule Misenyi, Kajunguti!! Wakati huo mbunge wa jimbo la Nkege akiwa Waziri wa A. Mashariki aliupigania uwanja huo, wakazi wa eneo lililopangiwa wakalipwa na fidia ila akazidiwa kete na faza house. Tatizo sio Chato, tatizo ni chuki binafsi kwa JPM. Watanzania tunapenda kulalama tu. Vitendo ziro kabisa.
 
Charity should reflect our nationhood//jifunzeni kutoka kwa baba wa Taifa ,aliyoyanena aliyaishi mwenyewe.Hopeless kabisa
Wewe ndo hopeful?! Unapoongelea nationalhood taswira yako inaitenga chato?! Kupinga tu hakusaidii. wakati analeta midege mikubwa watu wakaponda sana, ungedhani labda hakuna atakayepanda hizo ndege, sasa zinajaa na safari za nje zinazidi kuibuliwa! Jf ikekuwa sehemu ya kupumulia na ku-release tension za maisha. Acheni hizo.
 
Sisi wengine huwa tunapenda kuwa 'neutral observers' muda mwingi. Nakuomba tu, kwa uzi huu 'specifically', jaribu kulinganisha Gbadolite na Chato ukizingatia 'ACCESSIBILITY', 'POTENTIAL' ya utalii na uchumi kwa ujumla wake, POPULATION ...... etc etc!
Chato haina kitu !!. Pamoja na sarakasi za kuito Biharamulo, na kule kulazimisha iwe makao makuu ya mkoa wa Geita bila mafanikio. Chato haina kitu, bora Muganza & Katoro ziko kiuchumi kidogo
 
Hadi ikulu ya Chato inafanana na ile ya Gbadolite tofauti ni rangi tu na rangi ni mapenzi ya muhusika
 
Sasa shida ni ya Mobutu ama wacongo wenyewe! Kwa nini hawakupataifisha wakaibua mradi wa maana kama chuo, nk. Nachokiona katika wanaowalalamika sio kuwa wao wana mtazamo uliobora dhidi ya viongozi walalamikiwa bali wanaongozwa na chuki chuki chuki tu. Huo ndo uafrika.
Tatizo kukosa uoni wa vipaumbele.

Jenga kiwanda cha pamba Shinyanga na si Mtwara ambako wanalima korosho.
 
Charity begins at home! Uzuri ni kuwa chato ipo Tanzania! Kama malalamiko yanayoelekezwa kwa Mkuu yanalenga kutuaminisha kuwa Chato hapana hadhi katika Tanzania, ama basi yaliyofanywa huko yalipaswa kufanyika kaskazini tu itakuwa ni kumuonea mkuu.
Wakati mwingine sio lazima u comment kila uzi,uwe unapita tu kimya kimya
 
Komedi ya kumbukumbu ya Marshall Kamaradi Mobutu Sese Seko Kuku Wazabanga pia itakuwepo kupitia yale wananchi wanayofikiri juu ya maamuzi ya kulazimisha
 
Mzee baba mimi ni mtetezi wake ila kwa haya ya airport na mataa na mabenki yasiyo jengwa kwa kuangalia wingi wa wateja na fursa halisi simuungi mkono hata kidogo.

Hii ni 'precedent' mbaya sana kwa viongozi watakaomfuatia.
Mtu huyo anaonyesha dhahiri alivyo mbinafsi hatari.
Spika Sitta alifanya haya ya Mobutu, Eti kujenga ofisi ya Spika Urambo, baadaye alivyoutaka Uspika wenzake wakamwambia abadili jinsia awe mwanamke. Ofisi ile sijui amepewa nani!!!?
 
Charity begins at home! Uzuri ni kuwa chato ipo Tanzania! Kama malalamiko yanayoelekezwa kwa Mkuu yanalenga kutuaminisha kuwa Chato hapana hadhi katika Tanzania, ama basi yaliyofanywa huko yalipaswa kufanyika kaskazini tu itakuwa ni kumuonea mkuu.
Iwapo tuna haki ya kupinga ubinafsi wa wenye madaraka, basi ni lazima tuanze na Rais Magufuli. Anaachaje kuijenga Geita, makao makuu ya mkoa, anahangaika na Chato, kama siyo ubinafsi ni nini!!?
 
Kwa hiyo nyie kazi yenu ni kuwakabidhi watu tu nchi ili waongoze ,halafu nyie mnabaki kuwa mashabiki siyo? ,haaaa haaaa,
Ukaangalia comments nyingi kwa umakini utagundua wachangiaji ni watu kutoka kasikazini,,,,, imagine rais angetoka kaskazini nini kingetokea???? Na hatuna mpango wa kuwakabidhi nchi nyie watu mpaka baadaye sana kwasababu tunawajua vizuri, nani asiyewajua??
 
KWA MAUMBILE, MAZINGIRA NA MIUNDOMBINU ILIYOPO, CHATO INA 'POTENTIAL' YA KUKUA ZAIDI YA SHINYANGA, BUKOBA NA MUSOMA!
JADILI!
 
Back
Top Bottom