Hapa ni Gbadolite, Kijijini kwa dikiteta Mobutu Sesseko Kuku Wazabanga, nyumba zimegeuka Magofu na mahame

Hapa ni Gbadolite, Kijijini kwa dikiteta Mobutu Sesseko Kuku Wazabanga, nyumba zimegeuka Magofu na mahame

Mobutu Sesseko Kuku ngendu Wazabanga baada ya kuingia madarakani kimabavu akaanza utawala wa kidikteta

Akajenga ikulu/kasri kubwa kijijini kwao Gbadolite ,akajenga uwanja mkubwa wa kutua ndege tena zilikua zile Concord ,uwanja huu alijenga kijijini kwao

Mobutu alipandisha hadhi kijiji cha kwao na kuwa jiji yani jiji la Gbadolite

Mobutu baada ya kufurumushwa madarakani kijiji kimebaki gofu malisho ya mbuzi na ng'ombe

Ikulu imabaki magofu na makazi ya popo

Uwanja wa ndege umebaki kutua ndege john na wengine walio umbwa na Mungu

Mobutu alikula sana hela za Nchi ya Zaire kujitajirisha na kujenga kwao

Leo hii kwao kumebaki magofu

Magufuli soma historia.

Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Gbadolite
IkuluView attachment 1147267View attachment 1147269View attachment 1147270View attachment 1147271View attachment 1147272
Chattel ya miaka ya baadae
 
Dah aisee. Ni roho ngumu sana tena kuvaa uso wa mbuzi kupora mali za watu na kujenga mahekalu porini.

Mbinguni Waafrica hawaendi. Wallah kabisa.

Naanza kuamini ile inayosemwa kua sisi ni kizazi cha laana.

Africa kua kama ulaya ni ndoto za mchana.

Lkn wakongoman walishindwa nn kuendeleza hayo makazi ?

Ufafanuzi mwenye kufahamu plz.
 
July 6,2019
Magari ya waheshimiwa yakiwasili ktk uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Chato International uliopo ktk kijiji kimoja wilayani Chato mkoa wa Geita, Tanzania.
 
Tatizo ni huyo nduli na dikteta wa Ikulu kukiuka taratibu husika za nchi za kujichotea hazina zaidi ya bilioni 50 bila idhini ya Bunge. Hiyo si sawa na ni ubadhirifu mkubwa wa pesa wa walipa kodi unaostahili kukemewa na Watanzania wote. Nduli hayuko juu ya sheria na taratibu za nchi za kufanya vile atakavyo. Hayo ndiyo mambo ya akina nduli Idi Amin, dikteta Mobutu, Bokassa na wengineo.

Charity begins at home! Uzuri ni kuwa chato ipo Tanzania! Kama malalamiko yanayoelekezwa kwa Mkuu yanalenga kutuaminisha kuwa Chato hapana hadhi katika Tanzania, ama basi yaliyofanywa huko yalipaswa kufanyika kaskazini tu itakuwa ni kumuonea mkuu.
 
Muonekano wa chato airport in 15 years.

Mobutu Sesseko Kuku ngendu Wazabanga baada ya kuingia madarakani kimabavu akaanza utawala wa kidikteta

Akajenga ikulu/kasri kubwa kijijini kwao Gbadolite ,akajenga uwanja mkubwa wa kutua ndege tena zilikua zile Concord ,uwanja huu alijenga kijijini kwao

Mobutu alipandisha hadhi kijiji cha kwao na kuwa jiji yani jiji la Gbadolite

Mobutu baada ya kufurumushwa madarakani kijiji kimebaki gofu malisho ya mbuzi na ng'ombe

Ikulu imabaki magofu na makazi ya popo

Uwanja wa ndege umebaki kutua ndege john na wengine walio umbwa na Mungu

Mobutu alikula sana hela za Nchi ya Zaire kujitajirisha na kujenga kwao

Leo hii kwao kumebaki magofu

Magufuli soma historia.

Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Gbadolite
IkuluView attachment 1147267View attachment 1147269View attachment 1147270View attachment 1147271View attachment 1147272
 
July 6,2019
Magari ya waheshimiwa yakiwasili ktk uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Chato International uliopo ktk kijiji kimoja wilayani Chato mkoa wa Geita, Tanzania.
Duuuh kama nyumbu wanavuka mto Mara
 
Kabla ya Dikteta Mobutu kufa waliokuwa nae Rabbat Morocco aliyatamka haya,"msiwaibie wananchi fedha zao,heshimumi kodi za wananchi "Alikuja gundua yote ni kuukimbiza upepo. Dikteta Mobutu alikuwa na jeshi imara kamati ya ufundi waganga wote magwiji ni wake Lkn wakati ni ukuta ndumba ziliexpire wala dola haikumuokoa na kuteleza Kwa miti.Salama yake ilikuwa ni kukimbia ukimbizini.Mwisho wa dikteta yeyeto lzm uwe mbaya.
 
Huu ndio ujinga na upumbavu uliopitiliza
Kuna nini chato cha kuweza kuimarisha uchumi
Kwa hivi akija Rais mwingine toka Peramiho naye akajenga airport au mabenki huko kwao nayo itakuwa sawa?
Chazo cha mapato kiko wapi? Hawalimi hawafugi ardhi mbovu watu wenyewe ni primitive baiskeli tu hawana halafu unawapelekea ndege like seriously!
Angekarabati uwanja wa Mwanza uwe wa kimataifa
Time will tell

Ubinafsi ni silka ya Blackman,sababu ya ukosefu wa exposure na elimu,wenzetu utanguliza jamii kwanza.
 
Criteria yako ya kukua mji ni ipi?

Maana hata mji unaokua kwa mtu mmoja kwa mwaka unakua.

Kwenye human settlement, demography and economic development mara nyingi hua tunaangalia available natural resources, human resources, technology, infrastructure, inter relationship (trade) with surrounding or distant communities (centers, towns, cities etc)

Sasa kwa case ya Chato,

Utaona wana..
1. Ardhi nzuri ya kilimo
2. Misitu
3. Mbuga ya wanyama
4. Ziwa (Victoria)
5. Watu (human resources)
6. Miji iliyowazunguka ie Mwanza, Geita, Rwanda, Ngara etc
Na vingine viingi.

Je Chato ni kweli inaweza kugeuka kua magofu kama mleta mada anavyodai? Au utazidi kukua zaidi?

Uchambuzi wako mkuu kwa hili.
 
Nashukuru kwa kuwa umekuwa mkarimu, namna hii tunaweza kujadiliana na kuafikiana. Nikwambie Mkuu demokrasia si jambo jepesi kivile kama ambavyo uongozi si kila mmoja anauweza. Hata huko Marekani kuliibuka tuhuma za Trump kusaidiwa na Urusi katika kuupata urais, hapa Afrika demokrasia ni ndoto kabisaa. Lakini pia yapo mazingira ambayo udikteta ni bora kuliko demokrasia, sisi tumekaririshwa tu na mifumo yetu ya elimu.

Watu wakiona mambo hayako sawa waseme, na wapaze sauti! Ila wajenge hoja za msingi, kama hawasikilizwi wachukue hatua zinazoeleweka. Sio kujibanza kwenye keyboard na kulilia ndani. Afrika demokrasia bado sana.
Afrika inaharibiwa na watu wanaoingia madarakani kwa njia za demokrasia, lakini mara wanapoingia Ikulu hujigeuza madikteta kwa kuziteka nyara taasisi za kidemokrasia ili watawale bila kuulizwa. Matokeo yake ni kama haya yanayofanyika Chato.
Lakini nikukumbushe tu kuwa hoja huanzia kwenye keyboard na siku watu wakizichoka hizo keyboard hugeuka vichaa na hakuna wa kuwazuia. Mifano ya hivi karibuni ni Zimbabwe na Sudan.
Therefore, it is our Noble duty through our keyboard buttons, to remind our rulers not to take the people for granted!!!
 
Kwenye human settlement, demography and economic development mara nyingi hua tunaangalia available natural resources, human resources, technology, infrastructure, inter relationship (trade) with surrounding or distant communities (centers, towns, cities etc)

Sasa kwa case ya Chato,

Utaona wana..
1. Ardhi nzuri ya kilimo
2. Misitu
3. Mbuga ya wanyama
4. Ziwa (Victoria)
5. Watu (human resources)
6. Miji iliyowazunguka ie Mwanza, Geita, Rwanda, Ngara etc
Na vingine viingi.

Je Chato ni kweli inaweza kugeuka kua magofu kama mleta mada anavyodai? Au utazidi kukua zaidi?

Uchambuzi wako mkuu kwa hili.
Sehemu kama Chato ziko ngapi nchini, ngapi zimeizidi Chato kwa vivutio na kuweza kuwa na uchumi mkubwa zaidi, na kwa nini Chato ipewe kipaumbele (kiasi cha kujengewa uwanja wa ndege unaowezesha ndege kubwa kutua) zaidi ya pengine panapoweza kuwa na ukuaji mkubwa zaidi wa kiuchumi?

Tuangalie kanuni za uchumi za utilitarianism.
 
Unepaniki
Fizibiliti study bongo hii!! Rejea lile bwawa la DART jangwani, kulihitajika PhD kujua pale hapafai! Nachokuhakikishia hapa bongo wanaopinga progress za JPM nao wakipata nafasi watakuwa na madudu Yale yale tu! Sisi ni wabinafsi kwa hulka tu, lakini pia yeye sio mtakatifu hadi tuseme hautendei wema utakatifu huo. Hujawasikia wabunge pamoja na vipato vilivyonona bado walishindwa kutoa pesa binafsi kwenda kushangilia Taifa Stars, wakaomba pesa za umma!! Mpumzisheni Mkuu asee.
Hizi hoja zako za kujidharau hazifai. Ni aina ya mawazo yanayokubaliana na ile hoja ya Wazungu kuwa sisi Watu Weusi tu nusu watu. Ni dhana mfu. Kwamba mtu mweusi hawezi kufanya mambo kama binadamu kamili, Inasikitisha sana iwapo yanatoka kichwani kwa mtu mweusi.
Pia sisi Watanzania tunasahau kuhusu suala la ubinafsi na kujilimbikizia mali. Kwamba tuwaache waliopo madarakani waendelee na ubinafsi wao kwa kuwa wanaotaka uongozi nao watakuwa wabinafsi vilevile. Ni mawazo yaleyale ya "Mwafrika ni nusu mtu." Tunasahau kuwa hapa Tanzania tulikuwa na Kiongozi "role model." Julius K. Nyerere aliyeshinda ubinafsi, unawezaje kusema wengine wote wanafanana kama si mawazo ya kutetea udhaifu kwa kuwa unafaidi katika mfumo huo!!!?
 
Back
Top Bottom