Happy B'daY Carleen

Happy B'daY Carleen

Mdogo wangu Carleen. Niko kwenye quarantine + curfew ya Korona; na nilikuwa nimeamua kupumzika kidogo na JF lakini kwa hili nimeshindwa kujizuia. Nami naungana na wote kukutakia kila lililo la heri unaposherehekea siku yako hii ya muhimu. Hebu yote yaliyosemwa na kipenzi chako (na wapendwa wengineo) hapo juu na yakatimie kwako saba mara sabini katika mwaka huu mpya unaouanza; na mingine mingi ijayo. Mungu na Akakushike mkono na kukuimarisha zaidi na zaidi ewe binti wa ajabu.

Mimi huwa nakufananisha na Esta wa kwenye Biblia - yule binti jasiri wa Kiebrania aliyesimama imara mbele ya maadui wenye nguvu mpaka akaweza kujiokoa yeye mwenyewe, familia ya mjomba wake pamoja na watu wake wote. Wewe ni lulu ya thamani kabisa kabisa; na dunia ni bora zaidi kutokana na uwepo wako ndanimwe. U nyota ing'aayo sana ili kuwaonyesha njia wasafiri waliopotea na hata kupondeka mioyo katika kizazi hiki kinachohangaika huku na huko kikipapasa njia ya mkato kuelekea katika ufanisi (hasi) wa maisha. Naamini kuwa Mungu Analo kusudi kubwa sana na maisha yako. Mshukuru Yeye kwa yote. Mkabidhi Yeye njia zako na mshirikishe sana katika maamuzi yako yote. This big bro of yours is extremely happy for you; and I hope that your friendship with your Coco will last forever. Hebu na ikawe hivyo !!!
 
Happy Womb Escape Day Twinnie!

You are important and you matter. Remember to always be happy, It's the cheapest gift ever.
Stay strong, accept the challenge and move on to higher pedestal.
Live it up Carleen and know you are worth the world!! Have a fantastic year ahead.

I love you.
Twinnie wa watu. Najua nina kesi ya kujibu; tena kubwa ajabu. Kwa leo naomba tu nikusalimie. Sherehekea salama kuzaliwa kwa Twinnie wako; na nyote mbarikiwe sana !!!
 
Asante Paula. Yangu ni December 12...ila huwa ina mixed feelings kwa sababu mamangu kipenzi pia alifariki December 12...
Pole sana kwa kumpoteza mama.
Mama yangu alifariki December 19.

Sasa itabidi ya kwako usherekee kwa kupeleka maua kwenye kaburi. Na keki ukalie huko huko.
[emoji17][emoji17][emoji17][emoji17] I feel so sorry for you guys, Mungu azidi kuwapumzisha kwa amani hao mama zetu na azidi kuwafariji wapendwa wao. Amen
 
Back
Top Bottom