Happy birthday to me, Taikon wa Fasihi

Happy birthday to me, Taikon wa Fasihi

Ishi sana Mtibeli-Taikoni wa mapenzi kwa sasa Kihesa ,Iringa.
 
Kumbe ndio unaendelea kukua.. nitakuwa nakuvumilia pale unapoweka nyuzi zenye utoto, ignorance na immaturity.

Heri ya siku ya kuzaliwa.

Mwanadamu haishi Kukua, ukuaji hauna mwisho.
Halikadhalika ujinga hauna mwisho, ndio maana kwenye Maisha kuvumiliana ni Jambo la hekima na Busara.

Nimeishi na watu wenye umri mkubwa lakini wanaweza kufanya Jambo lolote ambalo linaweza kubeba tafsiri ya ujinga au Akili, upumbavu au hekima.

Hata hivyo Wakati mwingine MTU huweza kuamua kuwa mjinga ilhali anaakili, Maisha ni uchaguzi.

Mtu anahukumiwa Kwa dhamiri hiyo ndio hukumu ya Haki.

Shukrani Sana Mkuu, barikiwa.
 
Kwema Wakuu!

Ninafuraha kubwa katika siku hii ya leo.
Hii ndio siku ambayo nilizaliwa. Ndimi Taikon wa Fasihi, Mnyanyembe wa Tabora.

Nawashukuru wote mliokuwa baraka kwangu, lakini pia nawashukuru wale mliogeuka changamoto kwangu,
Mnisamehe wale wote niliowakosea Kwa namna moja ama nyingine.
Mimi kila Siku ninawasamehe wanikoseao, kamwe jua halitozama bila kusamehe walionikwaza. Hivyo sina kinyongo.

Tuishi Kwa upendo, tukifundishana, tukionyana na kukemeana pale tunapokosea. Lakini pia tukisaidiana, iwe ni kimawazo, kiuchumi, kijamii na Kiroho.

Hivyo ndivyo Maisha yetu yatakavyokuwa mazuri na Furaha.

Happy birthday to me, Taikon wa Fasihi, Mnyanyembe.

Sabato NJEMA.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Hbd boss
 
Kama uko na afadhali mfukoni jaribu kuita watoto uwapatie zawadi.wanapofurahi na mambo yako yanafunguliwa
 
Back
Top Bottom