Happy birthday to me, Taikon wa Fasihi

Happy birthday to me, Taikon wa Fasihi

Happy birthday Bob, uzidi kupata hekima mkuu. Still young sana, strive kuyafikia malengo yako ili ufaidi ya dunia huku ukisubiri ya mbinguni.
 
Mwanaume unasheherekeaje birthday wewe?
Kwa hiyo tukuletee keki upulize mishumaa [emoji849]
🤣🤣🤣shangaa nawewe mwanamke.mimi nimeuliza baazi ya wanaume wakaja kumtetea
Hawa ndio wanatamani kuwa Kama dada zao.mikazo hawawezi.
 
Celebraties wote wanasherehekea dunia nzima lakini watu wasiojielewa ndio wanajifanya wagumu, siku ya kuzaliwa si kwa ajili ya kupuliza mishumaa, unawatembelea wagonjwa, watoto yatima, wazee na kujipa muda wa tafakari za maisha yako, na legacy gani utaacha
Celebrities wanapaka mikorogo, wanatoboa pua na masikio, wanavaa milegezo na nusu uchi, wanajichora matattoo..... vipi ushaiga na hayo?
 
Kwema Wakuu!

Ninafuraha kubwa katika siku hii ya leo.
Hii ndio siku ambayo nilizaliwa. Ndimi Taikon wa Fasihi, Mnyanyembe wa Tabora.

Nawashukuru wote mliokuwa baraka kwangu, lakini pia nawashukuru wale mliogeuka changamoto kwangu,
Mnisamehe wale wote niliowakosea Kwa namna moja ama nyingine.
Mimi kila Siku ninawasamehe wanikoseao, kamwe jua halitozama bila kusamehe walionikwaza. Hivyo sina kinyongo.

Tuishi Kwa upendo, tukifundishana, tukionyana na kukemeana pale tunapokosea. Lakini pia tukisaidiana, iwe ni kimawazo, kiuchumi, kijamii na Kiroho.

Hivyo ndivyo Maisha yetu yatakavyokuwa mazuri na Furaha.

Happy birthday to me, Taikon wa Fasihi, Mnyanyembe.

Sabato NJEMA.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Happy birthday bwana Herieri. Uwepo wako unatuweka active muda mwingi sie wapenda kusoma na hatuna hela
 
Weka location nikuletee keki upulize mishumaa huku tunakuimbia "na kapicha kako nitakapost, wasokupenda itawacost"
Kukumbuka siku ya kuzaliwa hakuna ubaya mkuu, kusherehekea pia, kila mtu na mtazamo wake. Maisha yetu mafupi sana, dogo yupo 20s, soon tu anaanza kuwa mtu mzima na ana miaka michache sana ya kuitwa kijana.

Mkuu mimi na uzee huu unibless na keki na black&white moja tu, soon nazidi kutimiza uzee[emoji12]
 
Happy birthday bwana Herieri. Uwepo wako unatuweka active muda mwingi sie wapenda kusoma na hatuna hela

Shukrani Sana Mkuu.
Usijali Kwa kutokuwa na Pesa, Mungu ameumba Watu wengi ambao wanatoa vitu Kwa gharama nafuu Sawa na Bure.
Kutaka vya gharama ni MTU mwenyewe kutaka kujihangaisha.

Barikiwa Sana
 
Kuna watu ni wajinga mno,birthday yako unakuja kutuambia ili sisi tufanye nn?
 
Kheri ya siku ya kuzaliwa boss.
Ila mwanamume kuandika “happy birthday to me” inaleta zesheni kidogo
 
Celebrities wanapaka mikorogo, wanatoboa pua na masikio, wanavaa milegezo na nusu uchi, wanajichora matattoo..... vipi ushaiga na hayo?

Ikiwa Jambo lolote linavunja asili, Mila na desturi, pamoja na sheria za nchi Jambo Hilo ni Baya, Kwa Lugha ya kisheria huitwa Uhalifu, Kwa Lugha za kiimani huitwa Dhambi.

Ikiwa Mila na desturi zinakataza Watu wasitoboe masikio au kujichora miili yao hasa Kwa wanaume basi wanaofanya hivyo wanakosea.
Ingawaje, yapo makabila kama Kabila la maasai Mila na desturi zao zinaruhusu mwanaume kusuka Rasta Aina Fulani na kutoboa masikio.

Ni ishu ya maadili.
Na unaposema maadil "Moral" kwenye jamii moja inaweza kuwa kosa alafu jamii nyingine ikawa sio kosa.

Zingatia Dunia inajamii nyingi mno
 
Back
Top Bottom