Happy Father's Day kwa akina baba wote JF na Dunia kwa ujumla. Una ujumbe gani kwa Baba yako leo?

Happy Father's Day kwa akina baba wote JF na Dunia kwa ujumla. Una ujumbe gani kwa Baba yako leo?

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu salama?

SIKU YA BABA.jpg

Leo 16/6/2024 ni Siku ya akina Baba Duniani/Father's Day (ambayo husheherekewa kila Jumapili ya tatu ya Mwezi Juni). Kwa maoni siku hii hatuwasherekei tu wanaume wenye watoto/wanaoitwa baba na wenye upendo kwa watoto wao bali pia tunawasherekea:

- Wale wote wanaotamani kuwa baba kwa muda mrefu lakini bado hawajafanikiwa (Mungu atawasaidia msikate tamaa),

- Baba zetu waliotangulia mbele za haki (Mungu awalaze pema)

- Kina baba wa kesho (Mjipange kwa malezi, msije kutekeleza watoto wenu)

- Single father's ambao wanahakikisha watoto wao hawakosi kitu katika maisha yao na wanapata upendo wote

- Baba ambao uhusiano na watoto wao una changamoto za hapa na pale (endelea kupambana mambo yatakaa sawa)

images - 2024-06-16T082139.111.jpeg

- Wanaume waliosimama/wanaosimama kama baba kwenye maisha yetu (Mungu awabariki mmekuwa nguzo kubwa kwetu)

- Wanaume ambao wamepoteza watoto wao (Mungu awatie nguvu na faraja).

Katika siku ya leo, una ujumbe gani kwa baba yako?
 
Happy daddies' Day!!

Jah azidi kumuweka na aishi maisha marefu mnoo, ili nizidi kufurahia uwepo wake kwenye maisha yangu, huwa nawaza nisingekua na baba yeye ingekuajee?

Yeye amevuka viwango vya baba Bora, azidi kubarikiwa na kujaliwa zaidi ya pale anapohitaji.

[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Yaani Baada ya siku ya akinamama duniani kushika hatamu, watu wameona waje na siku ya wanaume! Sisi wanaume hatuhitaji haya mambo!! Ili iweje kwa mfano?? Tuacheni tuishi maisha yetu ya kawaida siku zote ni sawa na tuwajibika kila kukicha!!
 
Wakuu salama?

Leo 16/6/2024 ni Siku ya akina Baba Duniani/Father's Day. Kwa maoni siku hii hatuwasherekei tu wanaume wenye watoto/wanaoitwa baba na wenye upendo kwa watoto wao bali pia tunawasherekea:

- Wale wote wanaotamani kuwa baba kwa muda mrefu lakini bado hawajafanikiwa (Mungu atawasaidia msikate tamaa),

- Baba zetu waliotangulia mbele za haki (Mungu awalaze pema)

- Kina baba wa kesho (Mjipange kwa malezi, msije kutekeleza watoto wenu)

- Single father's ambao wanahakikisha watoto wao hawakosi kitu katika maisha yao na wanapata upendo wote

- Baba ambao uhusiano na watoto wao una changamoto za hapa na pale (endelea kupambana mambo yatakaa sawa)

- Wanaume waliosimama/wanaosimama kama baba kwenye maisha yetu (Mungu awabariki mmekuwa nguzo kubwa kwetu)

- Wanaume ambao wamepoteza watoto wao (Mungu awatie nguvu na faraja).

Katika siku ya leo, una ujumbe gani kwa baba yako?
Baba nakupenda
 
Yaani Baada ya siku ya akinamama duniani kushika hatamu, watu wameona waje na siku ya wanaume! Sisi wanaume hatuhitaji haya mambo!! Ili iweje kwa mfano?? Tuacheni tuishi maisha yetu ya kawaida siku zote ni sawa na tuwajibika kila kukicha!!
Kama wewe huhitaji ni sawa, baki na mtazamo wako Mkuu, acha wengine tusherekee sababu tunaheshimu uwepo wenu, bila akina baba kwenye maisha wengine tungepoteza ramani, wengine tusingefika hapa tumefika, wengine tusingekuwa presentable kama tulivyo, tusingekuwa na uthubutu kama tuliyonayo.... hivyo acha tuwasherekeee✨️✨️✨️

Afu leo ni Siku ya akina Baba sio Wanaume.
 
Happy daddies' Day!!

Jah azidi kumuweka na aishi maisha marefu mnoo, ili nizidi kufurahia uwepo wake kwenye maisha yangu, huwa nawaza nisingekua na baba yeye ingekuajee?

Yeye amevuka viwango vya baba Bora, azidi kubarikiwa na kujaliwa zaidi ya pale anapohitaji.

[emoji120][emoji120][emoji120]
Mungu azidi kumbariki✨️✨️
 
R.I.P mzee Swai. Ulinifundisha kuwa Mwanaume halisi wa kimachame. Do and don't zako zimenifanya niendelee kupambana humu duniani.

Tuonane asubuhi ile, katika pambazuko lile. Katika karamu ya mwanakondoo.
Mungu aendelee kumpumzisha pema✨️
 
Yaani Baada ya siku ya akinamama duniani kushika hatamu, watu wameona waje na siku ya wanaume! Sisi wanaume hatuhitaji haya mambo!! Ili iweje kwa mfano?? Tuacheni tuishi maisha yetu ya kawaida siku zote ni sawa na tuwajibika kila kukicha!!
Kuna kitu muhimu inaonekana Hauna. Attention to details. Hii ni siku ya kina baba (wazazi wa kiume), sio siku ya wanaume. Kuna tofauti hapo maana sio kila mwanaume ni baba. Asante
 
" Lakini mimi na nyumba yangu , tutamtumikia Mwenyezi-Mungu. "- Joshua 24:15

# Happy Father's Day
# Mungu atuwezeshe akina-Baba tuendelee kujipata . Tuzipambe nyumba zetu kwa vicheko na tabasamu kila wakati.
 
Baba yako anajua kuwa yule mwanaye aliyezaliwa kidume, akajivunia kuwa na dume. Aliyemlea na kumkuza kama shujaa na mrithi wake siku hizi amekuwa nyanya ntole. Inaumiza sana wazazi. Akijua ataumia sana ila nafasi bado unayo coca ya kubadilika na kuwa alfa male tena. Kuwa coca ambaye baba yake alijivunia alipoambiwa amepata mtoto wa kiume.

Ni bora ubgekuwa teja, mwizi na mvuta bangi. Ungeendelea kuwa shujaa na baba yako angejivunia ila sio kuvuliwa ubingwa. Inauma na kufedhehesha sana wazazi. Mungu akusaidie
Niliposema baba yangu amevuka viwango vya baba bora, nilimaanisha na anastahili wala sikukosea.

Baba yangu sio mbaguzi wa watoto, kwamba ajivunie wa kiume tyuu na wa kike asijivunie hilo kwake halipo, alinilea kwa mapenzi, maadili na makuzi yenye kumpendeza yeye na umma kwa ujumla tena kwa msingi thabiti wa imani na dini ya kikristo na kupitia baadhi ya hatua na sakramenti.

Yess anajua wazi uhalisia wa mwanae, huenda ananaumia km unavyosema but hakuna kilichobadilika kwake juu yangu, kuhusu mabadiliko ya kutoka nilivyo na kuwa utakavyo, hayo ni maamuzi na matakwa yangu, na yatafanywa kwa ridhaa yangu pale nitakapohitaji.

Umesema ni kheri ningekua jambazi, mlevi, mwizi, au mvuta bangi kwani ningekua mrithi na shujaa wake bado, sijui unalenga nn hasa, ila hayo yote ni ubatili sio ktk tamaduni wala maadili.

Baba yangu ana amini ktk uhuru binfasi hasa kwa mtu mzima aliye na umri wa kufanya maamuzi juu yake, hivyo hana shida kabisaa.

Aishi sana baba yanguu. [emoji482][emoji482]
 
Back
Top Bottom