Hongoreni kwakuyatoa maisha yenu kwaajili yetu.
Mnapambana sana kuhakikisha familia Iko sawa.
HERI YA SIKU YA BABA DUNIANI!!
Wewe ni muhimu sana kwenye haya maisha.
Wewe ni nguvu ya watoto wako.
Kuna vitu mama hata apambane vipi, hawezi kumpatia mtoto. Wazazi wote ni muhimu kwa nafasi zao ila, baba ni mhimili kwenye maisha ya mtoto wake.
BABA;
Jina hili ni kofia ya moto yenye misumari inayokuchoma kichwani kila ukiwawazia wana wako. Naomba nikukumbushe.....
Kulea ni jukumu la wazazi wote. Malezi ya watoto hayasimami kwenye nafasi ya matunzo. Kuwatunza ni kuwapa chakula, mavazi; malazi na elimu. Kulea ni kuutoa muda wako wa thamani kujenga mawasiliano na watoto. Kuwaonyesha unawapenda hata kama wako mbali nawe kimazingira.
Kuna nafasi kubwa moyoni mwa mtoto ambayo hujazwa na upendo wa baba tu. Watoto ambao hawajawahi kuamini kuwa wanapendwa na baba zao, ujasiri wao ni nusu ya ule walionao watoto waliooonyeshwa upendo na baba zao.
Wakati mwingine upendo, kueleweka, kuthaminika, kuaminika, kupewa nafasi na mambo mfanano wa hayo...ni hitaji kubwa zaidi na la thamani likipatikana kwa mtoto kutoka kwa babaye; kuliko hizo bidhaa zinazoweza kununulika.
Kauli zenu kwa watoto wenu wa kike na wakiume, zitatengeneza ama zitaharibu maisha yao huko mbeleni.
Mabinti zenu wanatamani kusikia mkiwaambia ni wazuri, werevu, wa maana, wanaojitosheleza na wa muhimu.
Vidume vyenu, vinataka kusikia mkiwaambia namna ni werevu na wenye nguvu na uwezo wa kufanikisha chochote maishani.
Inatangulia kauli ya Muumbaji inafuata kauli ya Baba. Hizi kauli ni muhimu sana kwenye maisha ya mwanadamu yoyote mwenye moyo udundao kwa mpigo wa sekunde.
Kila mtoto mwenye uhakika wa uwepo wa baba kwenye maisha yake, anataka sana kumuona akiwajibika kama kiongozi na kama mzazi.
NOTE: Wamama ambao mmetengana na wababa wa watoto, kwa sababu yoyote isiyohusisha uhai na kifo, wapeni hao wababa nafasi ya kuwalea watoto kwa nguvu na uwezo waliojaaliwa. Vita vya mapenzi visiingilie na kuharibu maisha ya mtoto.
Kama baba yuko hai, na anaihitaji hiyo nafasi ya kuwajibika, usimnyime. Mtoto wako anamhitaji sana. Usitamani kufanyika fahari kwa kutambulishwa kama 'super women' hali ya kuwa huyo unayetamani aje akutambulishe unamharibia njia kwakumtenga na baba yake.
Malezi yanahitaji akili na kusakanya maarifa kila siku, hayataki hisia. Kumpenda mtoto tu hakutoshi, mfundishe, muelekeze, mpe sababu na wakati fulani mpe njia. Kwenye hili, Baba ni muhimu sana.
Hongera kwakuwa baba mzuri.
Hongera kwa kuwa baba bora.
MUSTAKABALI WA KIZAZI KIJACHO UNAKUHITAJI SANA BABA AMBAYE UNAIJUA NA KUIISHI NAFASI YAKO.