Happy Father's Day kwa akina baba wote JF na Dunia kwa ujumla. Una ujumbe gani kwa Baba yako leo?

Happy Father's Day kwa akina baba wote JF na Dunia kwa ujumla. Una ujumbe gani kwa Baba yako leo?

Baba anabariki ugay??? Ye hataki kizazi chake kiendelee[emoji849]

Kosugi haya leo kaandika mwenyewe njoo uone
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Eve bhana, kwan wasiondekeza kizazi wote ni GAYS? unafahamu kuna GAYS wanaendeleza kizazi km kawaidaa?

Hebu m Relaaaaaxxxx!!! Life fupii hilii bhanaaa.
 
”Happy fathers day” ndiyo kitu gani hicho?

Hivi vi-wishes vya ajabu ajabu ndiyo vinasababisha wanaume wa Kiafrika kujisahau na kuanza kulia lia kutunzwa na wake zao,hayo ni mambo ya wazungu hayatuhusu waafrika.
Kabisa.....
Ndio tumefikia wanaume kupost "my birthday loading....."
 
Mhhh!

Hivi waafrika ni lini tutaacha kuwalaumu wazungu hata kwa vitu visivyoeleweka? Hasa uvivu wa akili zetu. Watu wenyewe kila siku na mabakuli yetu tunawafuata kwao kuwasumbua, tukiwategemea hadi kwa kondomu, na neti!

Wao wakianzisha hizo siku kwa malengo ya kibiashara mbona ni mawazo mazuri ya kukuza uchumi. Na si kwamba maadhimisho na biashara hizo hufanyika Afrika pekee, hata kwao pia. Zaidi, hizo biashara za kuuziana vyakula na maua na zawadi nyinginezo sisi hatuzuiwi kufanya, maana hawasafiri na bidhaa zao kuja kuuza wenyewe. Kwa kiasi kikubwa tunauziana wenyewe huku hivyo hawatupangii vya kuuziana, hata tukiamua tuuziane gongo na wanzuki hawatuzuii. Badala tushukuru wametupa fursa za biashara akili zetu zilikuwa zimeganda zinawaza uzinzi, uchawi na siasa chafu, tunawalaani tena! Kweli shukrani ya punda ni mateke.
Mimi sajawalaumu wazungu bali nimewalaumu Waafrika kwa kuiga. Ulichoandika ndicho nilichomaanisha, Kwamba sisi Waafrika tunaishi on dependency kwa hao wenzetu. Hizi siku zote wao ndio waasisi ama waanzilishi. Sisi tunapokea na kutekeleza.

Hayo ni mawazo yangu tu ila kila mtu yupo huru kutekeleza na kufurahia kile akipendacho maadam havunji sheria za nchi.
 
Basi huyo ni baba wa hovyp zaidi duniani anayebariki mwanaye wa kiume apakuliwe mavi na wanaume wenzake. Hakuma baba hapo ila kuna kituko cha Baba. 😀😃😄😁
Hamna kitu humo bro,wewe alichokiandika umesoma ukakimaliza?

Dizain hiyo ndiyo walivyo hayo maneno amemsingizia baba yake akitafuta faraja ya nafsi yake hakuna mwanaume wa Kiafrika atakubali huo upuuzi labda awe na huyo baba yake huo ndiyo ulikuwa mchezo wake
 
Coca unanichota mimi ndugu yako! Siku ile ulimuweka mwingine nikakuuliza ukasema ni wewe akati yule na huyu ni watu wawili tofauti
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yupiii huyoo kwa avatar au? Ambaye ulimuona na nilisema ndo mie?
 
HERI YA SIKU YA BABA DUNIANI!

Wewe ni muhimu sana kwenye haya maisha. Wewe ni nguvu ya watoto wako. Kuna vitu mama hata apambane vipi, hawezi kumpatia mtoto. Wazazi wote ni muhimu kwa nafasi zao ila, baba ni mhimili kwenye maisha ya mtoto wake.

BABA;
Jina hili ni kofia ya moto yenye misumari inayokuchoma kichwani kila ukiwawazia wana wako. Naomba nikukumbushe.

Kulea ni jukumu la wazazi wote. Malezi ya watoto hayasimami kwenye nafasi ya matunzo. Kuwatunza ni kuwapa chakula, mavazi; malazi na elimu. Kulea ni kuutoa muda wako wa thamani kujenga mawasiliano na watoto. Kuwaonyesha unawapenda hata kama wako mbali nawe kimazingira.

Kuna nafasi kubwa moyoni mwa mtoto ambayo hujazwa na upendo wa baba tu. Watoto ambao hawajawahi kuamini kuwa wanapendwa na baba zao, ujasiri wao ni nusu ya ule walionao watoto waliooonyeshwa upendo na baba zao.

Wakati mwingine upendo, kueleweka, kuthaminika, kuaminika, kupewa nafasi na mambo mfanano wa hayo...ni hitaji kubwa zaidi na la thamani likipatikana kwa mtoto kutoka kwa babaye; kuliko hizo bidhaa zinazoweza kununulika.

Kauli zenu kwa watoto wenu wa kike na wakiume, zitatengeneza ama zitaharibu maisha yao huko mbeleni.

Mabinti zenu wanatamani kusikia mkiwaambia ni wazuri, werevu, wa maana, wanaojitosheleza na wa muhimu.

Vidume vyenu, vinataka kusikia mkiwaambia namna ni werevu na wenye nguvu na uwezo wa kufanikisha chochote maishani.

Inatangulia kauli ya Muumbaji inafuata kauli ya Baba. Hizi kauli ni muhimu sana kwenye maisha ya mwanadamu yoyote mwenye moyo udundao kwa mpigo wa sekunde.

Kila mtoto mwenye uhakika wa uwepo wa baba kwenye maisha yake, anataka sana kumuona akiwajibika kama kiongozi na kama mzazi.

NOTE: Wamama ambao mmetengana na wababa wa watoto, kwa sababu yoyote isiyohusisha uhai na kifo, wapeni hao wababa nafasi ya kuwalea watoto kwa nguvu na uwezo waliojaaliwa. Vita vya mapenzi visiingilie na kuharibu maisha ya mtoto.

Kama baba yuko hai, na anaihitaji hiyo nafasi ya kuwajibika, usimnyime. Mtoto wako anamhitaji sana. Usitamani kufanyika fahari kwa kutambulishwa kama 'super women' hali ya kuwa huyo unayetamani aje akutambulishe unamharibia njia kwakumtenga na baba yake.

Malezi yanahitaji akili na kusakanya maarifa kila siku, hayataki hisia. Kumpenda mtoto tu hakutoshi, mfundishe, muelekeze, mpe sababu na wakati fulani mpe njia. Kwenye hili, Baba ni muhimu sana.

Hongera kwakuwa baba mzuri.
Hongera kwa kuwa baba bora.

MUSTAKABALI WA KIZAZI KIJACHO UNAKUHITAJI SANA BABA AMBAYE UNAIJUA NA KUIISHI NAFASI YAKO.

Heri kwenu nyote. Mtunzwe na Mungu.
 

Attachments

  • _3760d946-c225-4a7d-bf4d-986fd2f5ec65.jpeg
    _3760d946-c225-4a7d-bf4d-986fd2f5ec65.jpeg
    223.4 KB · Views: 0
Asante kwa dua zako kwetu, kumbe ndio maana naona kuna keki imefichwa hapa ndani lakini haina maandishi yeyote, nahisi walitaka wanifanyie surprise....🤣
 
Tatizo sisi Waafrika bado tunaishi kwa kutegemea fikra za mzungu kila anachokitunga na kukileta sisi ni wapokeaji na watekelezaji. Valentine Day, Women Day, Mothers Day, Fathers Day, AIDS Day. Tuishi kwa utashi wetu tumpende kila mtu na kuambiana mara kwa mara kwamba tunapendana na kuthaminiana.

Hizi siku zilitengenezwa na wazungu kwa malengo yao ya kibiashara...siku hizi ndipo wafanyabiashara wanauza sana maua, vyakula,na zawadi nyingine mbali mbali
Watu wanaiga ujinga.

Hivi hivi itakuja na siku ya mashoga duniani waunge mstari kutakiana heri,ni ujinga wa kiwango cha juu sana kujifanya kusherehekea hizi siku hasa anapokuwa mwanaume ndiye ameunga trailer.
 
Kwa niaba ya babaz wote, tumepokea wishes. Tutaendelea kuwa baba bora kabisa kwa watoto wetu na wale wote tunaowahudumia kama baba.

Lakini wakati tunatimiza majukumu yetu ya ubaba, hakikisheni na nyie kama watoto mnatimiza wajibu wenu, someni, fanyeni kazi, jiongezeni ili tuzidi kujivunia kuwa baba zenu.
 
Endelea kupumzika kwa amani mzee!

natamani unitokee ndotoni unipe mafunzo ya kuishi vizuri na mke wangu..

Baba uliwezaje kuishi na wanawake wanne katika compound moja? Mbona mimi hapa mke mmoja tu ananipa kamzozo?
 
Happy father's day nawapongeza wanaume wote tunao pambana usku na mchan Ili family zetu zile pamoja na yote tunaonekan hatuna maana tunasemwa hatuhudumii family zetu japo tuna hudumia thaman yetu hazionekan kwasababu wanawake tulio zaa nao nakuwa nao wanasema ubaya Zaid Kwa watoto wetu kulko mazuri tunayo fanya Mungu yupo pamoja na sisi tusife moyo tuendele na mapambango Zaid tusiache kumuomba Mungu
Mr chaupole
UBUNTU BOTHO
 
Happy father's day nawapongeza wanaume wote tunao pambana usku na mchan Ili family zetu zile pamoja na yote tunaonekan hatuna maana tunasemwa hatuhudumii family zetu japo tuna hudumia thaman yetu hazionekan kwasababu wanawake tulio zaa nao nakuwa nao wanasema ubaya Zaid Kwa watoto wetu kulko mazuri tunayo fanya Mungu yupo pamoja na sisi tusife moyo tuendele na mapambango Zaid tusiache kumuomba Mungu
Mr chaupole
 
R.I.P mzee Swai. Ulinifundisha kuwa Mwanaume halisi wa kimachame. Do and don't zako zimenifanya niendelee kupambana humu duniani.

Tuonane asubuhi ile, katika pambazuko lile. Katika karamu ya mwanakondoo.
Na wakwa nawe nyalemefwa ndao[emoji24]
 
Happy father's day nawapongeza wanaume wote tunao pambana usku na mchan Ili family zetu zile pamoja na yote tunaonekan hatuna maana tunasemwa hatuhudumii family zetu japo tuna hudumia thaman yetu hazionekan kwasababu wanawake tulio zaa nao nakuwa nao wanasema ubaya Zaid Kwa watoto wetu kulko mazuri tunayo fanya Mungu yupo pamoja na sisi tusife moyo tuendele na mapambango Zaid tusiache kumuomba Mungu
Mr chaupole

UBUNTU BOTHO
Mwanaume hapongezwi wala hasifiwi hayo uliyoorodhesha hapo ni majukumu yake ya lazima anayopaswa ayatekeleze kila siku awe amependa au hakupenda,wanaume tumepewa koromeo ukiona mwenzako anavyochakarika inatosha kumuwazia mema na kumkubali kimoyo moyo.

Otherwise ukimwambia unampongeza au unampenda (hata baba yako mzazi) anaweza akakuona namna gani asikuelewe vizuri.
 
Pumzika kwa amani mzee wangu!!

Ulinitengeza kuwa imara, mbunifu,.mvumilivu na kukabiliana na shida za dunia na kutokata tamaa

Hapa nilipo mafanikio, familia ni matunda ya mapambano yako

Daaaah

Pumzika kwa amani baba yangu
 
Back
Top Bottom