Happy Father's Day kwa akina baba wote JF na Dunia kwa ujumla. Una ujumbe gani kwa Baba yako leo?

Ahsante sana mkuu kwa niaba ya wababa watarajiwa
 
Nampenda baba yangu japo ni mkali🥰
Bila malezi yake Bora akishirikiana na mama yangu kipenzi, sidhani kama ningekuwa na mafanikio au Hali niliyonayo Sasa.
Licha ya uchumi WA baba yangu kuwa mzuri, lakini hakunijengea tabia ya kuuwaza na kuutegemea kwa maisha yangu ya baadae

Alinijengea tabia ya ku hustle kivyangu Mimi pamoja na ndungu zangu tunajivunia kuwa na baba Bora

Kuelekea ndoa yangu baba kaniahidi mambo mazuri

Nakupenda baba nyamwi♥️♥️♥️♥️
 
Asante sana Cute Wife 🤝
 
Kama keyboad uliyoitumia kuandika hapa ni ya mzungu, unachoongea hakina maana
 
Namkumbuka kwa kunipa kipondo kizito kila nilipogoma kwenda shule na leo naona faida niliyopata kwa kipigo kile simchukii kabisa nafikiri asingenipa kipondo ingekuwaje leo?
 
Duh! Na wewe umeshakuwa baba?
 
Kina baba ni mihimili muhimu sana ya familia.
Nguzo ya familia ni baba.
Mlinzi wa familia ni baba.
Shifu/master wa familia kujifunza na kuwa imara ni baba.
Namshukuru baba yangu kwa mambo matatu;
1)Amenipambania mpaka sasa na hachoki kunipambania licha kuwa nimekua ila anatamani anilee mpaka nikifa.
2)Alinivumilia licha ya makosa mengi na akanipa nafasi tena na tena mpaka nikawa imara.
3)Amenifunza mengi kimaisha japo kwa njia ngumu nyingine za kutokwa na machozi,ila alikua akinijenga na kweli nimejengeka.
ALLAH AMPE STAHIKI BORA BABANGU KWA JINSI ALIVYOTUKUZA VYEMA.
 
Yaani Baada ya siku ya akinamama duniani kushika hatamu, watu wameona waje na siku ya wanaume! Sisi wanaume hatuhitaji haya mambo!! Ili iweje kwa mfano?? Tuacheni tuishi maisha yetu ya kawaida siku zote ni sawa na tuwajibika kila kukicha!!
Umemaliza kaka.
Tuishi humo.
 
Mhhh!

Hivi waafrika ni lini tutaacha kuwalaumu wazungu hata kwa vitu visivyoeleweka? Hasa uvivu wa akili zetu. Watu wenyewe kila siku na mabakuli yetu tunawafuata kwao kuwasumbua, tukiwategemea hadi kwa kondomu, na neti!

Wao wakianzisha hizo siku kwa malengo ya kibiashara mbona ni mawazo mazuri ya kukuza uchumi. Na si kwamba maadhimisho na biashara hizo hufanyika Afrika pekee, hata kwao pia. Zaidi, hizo biashara za kuuziana vyakula na maua na zawadi nyinginezo sisi hatuzuiwi kufanya, maana hawasafiri na bidhaa zao kuja kuuza wenyewe. Kwa kiasi kikubwa tunauziana wenyewe huku hivyo hawatupangii vya kuuziana, hata tukiamua tuuziane gongo na wanzuki hawatuzuii. Badala tushukuru wametupa fursa za biashara akili zetu zilikuwa zimeganda zinawaza uzinzi, uchawi na siasa chafu, tunawalaani tena! Kweli shukrani ya punda ni mateke.
 
Namuomba Mwenyezi Mungu amfanyie wepesi Baba yangu aliyetangulia mbele za haki, amuondolee adhabu kaburi, amsamehe madhambi yake na amjalie Pepo InshaAllah.
 
Nimesoma vizuri sana. Ila katika kusoma ndio nikabaini wewe ni mwanaume.

Ndio maana nikakuuliza mwanaume mwenzetu, umeshakuwa baba? Au bado bachela kama Nay wa mitego?
Bachelor km Bob risky [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
”Happy fathers day” ndiyo kitu gani hicho?

Hivi vi-wishes vya ajabu ajabu ndiyo vinasababisha wanaume wa Kiafrika kujisahau na kuanza kulia lia kutunzwa na wake zao,hayo ni mambo ya wazungu hayatuhusu waafrika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…