Siku ya Kimataifa ya Wanawake tarehe 8 Machi, ni muhimu katika kutambua jitihada, harakati na mchango wa Wanawake Duniani kote
Tunasherekea mafanikio ya Wanawake katika nyanja mbalimbali za Maisha kama vile mafanikio binafsi, kihistoria, kiuchumi, kisayansi, kisiasa na kiutamaduni, pamoja na kuhamasisha juhudi za kuleta usawa wa kijinsia Duniani kote
Kauli Mbiu Siku Ya Wanawake 2024 inalenga Kuchochea Ushirikishwaji wa wanawake katika jamii ili kuongeza kasi ya maendeleo
Nia ya kaulimbiu hii ni kumpa mwanamke thamani ili kuchochea maendeleo na kuihamasisha jamii kumshirikisha mwanamke katika maendeleo.
Je una ujumbe gani kwa Wanawake unaowafahamu (Mama, Mke, Mpenzi, Rafiki na Mtoto wa Kike)?