Haraka sana nahitaji Mwanamke wa kwenda nae Kufunga Ndoa ya 'Kibwerere' Mkoani Arusha

Haraka sana nahitaji Mwanamke wa kwenda nae Kufunga Ndoa ya 'Kibwerere' Mkoani Arusha

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema Serikali itagharamia shughuli zote za harusi, ikiwemo kulipia ukumbi mkoani hapo lengo likiwa ni kuvutia zaidi wageni na watalii kufika Arusha na kuwa chachu ya kukuza uchumi.

Makonda amesema masharti ya ndoa hizo ni pamoja na kati ya wawili hao, mmoja wao atoke nje ya mkoa huo, ikiwezekana atoke nje ya nchi akiwa na maana kwamba wale ambao wote ni wakazi wa mkoani hapo fursa hiyo haitawahusu.

"Lengo letu sisi hatutaki kuwa na 'high season' au 'low season', tunataka kutengeneza shughuli na matukio mbalimbali kuhakikisha muda wote uchumi unakuwa na kuendelea, ili mama wa mboga, bodaboda na kila mtu anufaike na ugeni unaofika hapa Arusha," amesema.

Makonda amesema hayo leo Jumatatu Julai 8, 2024 jijini Arusha alipokutana na wadau na mashirika na asasi zisizo za kiserikali.

Chanzo: mwananchi_official

Najua Mademu wengi hapa JamiiForums mnatamani Kuolewa nami haya jitokezeni nimchague twende zetu Arusha.
 
Watu wa Arusha wana Raha sana Mkuu yaani Wewe tafuta tu Demu wako kokote kule kisha muone Makonda na Uoe.
Ukitaka kujua Wakuu wa Wilaya & Mikoa hawana kazi fuatilia harakati za Makonda na yule Bwege aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai.
 
Back
Top Bottom