Harakati ya kuuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Hapo ndy kwenye utata,,

Population yao ni ndogo lakini fungu la pesa tunagawana sawa sawa.

Huoni kama hawana cha kulalamikia muungano?
Nakubaliana nawe. Ila kumbuka wao huishi kwenye ndoto za mchana za kudhani kuwa wakiwa nje ya muungano wanaweza kuwa kama mabwana zao wa Mashariki ya Kati wanaowabagua na kuwadharau bila kuangalia Comoro wamefikia wapi
 
Zilizoungana ni nchi mbili sovereign states.

Mbinu za kuimeza Zanzibar zimefeli na Tanganyika kujificha kwenye serikali ya muungano Wazanzibar wanajuwa vizuri, Sasa wacha watunyoonye.

Mbapokaaga Dodoma kuwapangia Rais wa Zanzibar msidhani wenzeni hawaumii, Sasa tumieni mnyolewe ni zamu yao.

Yani inashangaza eti mjumbe wa Bukoba, Geita, Mwanza na kwingineko ndio anachaguwa mgombea Urais wa Zanzibar, na mgombea wanaomtaka Wazanzibar wenyewe kura hazitoshi kwa sababu akidi ya wajumbe wapo wachache, ni kwa nini msiwaache wachujane wenyewe hukohuko Zanzibar?
 
Nakubaliana nawe. Ila kumbuka wao huishi kwenye ndoto za mchana za kudhani kuwa wakiwa nje ya muungano wanaweza kuwa kama mabwana zao wa Mashariki ya Kati wanaowabagua na kuwadharau bila kuangalia Comoro wamefikia wapi
Inferiority complex, ukweli ni kwamba Tanganyika ndio inadumaza maendeleo ya Zanzibar, tunawakosesha hadi fursa hadhimu zinazopatikana OIC.

Zanzibar ndogo yalikuwa makao mkuu ya Sultan wa Oman, kimsingi Zanzibar ilikuwa ni kama sehemu ya Oman na wakiwa hhru wana Uhuru wa kuungana na Oman, tukome kuwapangia maisha ndio maana wanatuchukia sana machogo tumejaa ujuwaji wakati tuna Ardhi kubwa hata kuitumia hatujui.
 
Muungano umeshikiliwa na kipengele kimoja tu cha siasa
 
Nashukuru kuwa umekubaliana na hoja yangu kuwa bado Wazenj bado wanajiona kama waomani wasijue kwao ni watumwa wasio na thamani. Yaani, unajisifia Znz kuwa makao ya mpumbavu na mhalifu Sultan? Kweli, upumbavu ni zaidi ya mzigo. Kwanini usijivunie Uafrika wako? Kama znz ni sehemu ya Oman, kwanini Oman hawajaidai? Hata historia rahisi ya nchi yako huijui!
 
Huu ujumbe nadhani s ujumbe wangu. Sijaongelea Liberia. Umekurupuka. Umechemka na kuchemsha bure. Hilooo!
 
Huna uchungu wowote wa kuikosa Tanganyika? Hauoni au kuhisi kuna mambo yamepwa kwa Tanganyika kukosekana?
 
Huna uchungu wowote wa kuikosa Tanganyika? Hauoni au kuhisi kuna mambo yamepwa kwa Tanganyika kukosekana?
Mkuu 'Yoda', kwa kawaida huwa ninakuchukulia tofauti sana na wachangiaji wengine humu JF, kwa sababu hukuchukulia kama mtu mwenye upeo mpana kuhusu maswala mbalimbali.

Sasa unanichanganya hapa na hilo swali lako uliloniuliza hapo. Hivi kweli umenisoma na kunielewa vizuri?

Kwa nini niwe na uchungu na Tanganyika au Zanzibar na nisiwe na uchungu mkubwa zaidi juu ya Tanzania?
 
Bhangi ni kitu mbaya Sana.
 
Outside of the union there is no Tanzania. There is Tanganyika and zanzibar. There is also no president of tanzania. We will have to choose the president of tanganyika. I dont think samia or any other president will be willing to see his job relinquished like Gorbachev
 
Hakuna tanzania bara sema Tanganyika ueleweke.

#MaendeleoHayanaChama
 
Tukivunja muungano Kuna nchi moja itaona madhara ya kuwa nje ya muungano itabidi iombe Tena kuungana bila masharti yoyote
 
Wa Tanzania bara ni watu wa nchi ipi hiyo ??
 
Tukivunja muungano Kuna nchi moja itaona madhara ya kuwa nje ya muungano itabidi iombe Tena kuungana bila masharti yoyote

Kwani kwenye huu uvamizi uliopewa jina la muungano kuna nchi iliomba kuungana ??
 
Kifupi Zanzibar hawatupendi wa Tanzania bara
Kama waiita Zanzibar basi iseme Tanganyika

Kama waiita Tanzania bara basi iseme Tanzania visiwani.

Vinginevyo sema sehemu ya Jamhuri ya Muungano Tanzania baadhi ya watu wake wana jambo linalowashangaza wenzao.
 
Wewe ni vuvuzela , unataka kuvunja muungano JF
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…