Mkuu 'Thailand',
Pamoja na kuielewa mada yako vizuri kabisa, lakini wazo tu la "kuuvunja Muungano ni la kihayawani.
Kwa nini uvunje Muungano kwa sababu hafifu kama hizo ulizotaja wewe. Utashindwaje kutatua hizo kero za kipuuzi kabisa ulizoeleza hapa!
Mbona watu wanapenda sana kukuza matatizo yanayochochewa na wapuuzi wachache, hasa walioko huko visiwani.
Wewe huoni kwamba unawafurahisha sana hawa watu wanapokuona unarukwa akili kiasi kile na michezo yao ya kijinga hii inayofanyika sasa, ikichagizwa na hao walioko madarakani sasa hivi.
Sasa nikwambie, hakuna wa kuuvunja Muungano wetu, ila kitakachofanyika ni kuwafanya waTanzania wote, bila kujali mtu katokea wapi, kuwa na fursa sawa katika Jamhuri hii.
Uwe Unguja au Makambako, utajisikia mTanzania kwanza kabla ya umakumbako wako.