Harakati ya kuuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Mzanzibar ameruhusiwa kununua ardhi Tanganyika ila mtanganyika haruhusiwi kununua ardhi znz, kuna wazanzibar wanakuja Tanganyika wanakua wakuu wa mikoa/wilaya ila mtanganyika haruhusiwi kushika vyeo znz labda wale wa kwenye majeshi
 
Utanielewa tu siku hiyo Zanzibar itakapokuwa huru kwa 100%. Ila siyo sasa.
Ataelewa pale Tanganyika itakapoanza kuwakatia umeme Kwa kushindwa kuulipia, kuwauzia maji, mkaa, mchanga na vitu vingine wanavyochukua bure Huku bara, pale Tanganyika itakapoanza ajira, ardhi ni Kwa ajili ya watanganyika hayo ni Kwa uchache
 
Post zingine mnaanza kwenda mbali utakamatwa halafu uanze kulalamika wasiojulikana. Jaribuni kuwa mnaandika mambo kwa mipaka, punguzeni utoto kwenye mambo makubwa na ambayo ni serious kwa nchi
 
Tafuta clip ya Lukuvi utapata idea....
 
Siku muungano huu ukivunjika nitafanya sherehe kubwa na champagne za kumwaga zinanyweka
 
Ungefafanua ni kero zipi za Bara ambazo haziangaliwi, na ni matendo gani wanafanya kuonyesha kua hawatupendi watu wa bara?
 
Muungano uko kwenye maji ya bahari na ulinzi wa nchi. Muungano ni moyo wa Tz , ukitaka muungano ufe unaweza kuanza kufa wewe! Jitahidi sana kutumia ID feki unapoweka mada kama hizi.
 
Baada ya kuuvunja huu muungano huu uchwara, Wazanzibar mlio bara mjiandae kurudi kwenu Zanzibar au muukane uraia wa Zanzibar na muwe raia kamili wa Tanzania.
=
Your browser is not able to display this video.
 
Siku muungano huu ukivunjika nitafanya sherehe kubwa na champagne za kumwaga zinanyweka
Mkuu SAGAI GALGANO , O - Level ulisoma somo la kemia?, kuna topic ya pili baada what is chemistry ni chemical reactions na by products, yaani kuna vitu ukivichanganya unapata kitu kinachoitwa mixture, kama kuchanya maji na matope, au chumvi na maji, kunakuwa hakuna chemical reactions, hivyo vitu hivyo unaweza kuvitenganisha ukapata zile reagents za awali, lakini muungano wetu ni muungano wa chemical reaction kuunda compound mpya, hauvinjiki!.

Mimi ni mtu wa mastori mastori, kama una muda, karibu kwenye mastori, kama huna muda, just jump
Hivyo ndivyo ulivyo huu muungano wetu adhimu ni muungano wa chemical process Tanganyika imekufa, Zanzibar imekufa, Tanzania imezaliwa, huwezi kuifufua Tanganyika, au Zanzibar, Tanzania ni mtoto wa ndoa hii!. This is union for life!. Ni rahisi kwa ndugu na jamaa za Sultan Sayyid Said kurejea kwao Oman kuliko kuuvunja huu muungano wetu adhimu uliongiwa na wajukuu wa ukoo wa MwinyiMkuu ndio wenye Zanzibar yao, achana na hawa wapiga kelele wakuja!.

Wale wanaosubiri kwa hamu muungano wetu huu adhimu ufe, watasubiri sana!, ni kama fisi anavyoona binadamu akitembea anavyo tingisha mikono, anadhani imekatika inakaribia kuanguka, hivyo anaifuata kwa nyuma kuisubiria!.

Tena safari hii Tanzania tuna bahati kumpata huyu Mama ni mtenda haki sana!, kwanza ameruhusu "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
Kisha kwa vile siku zote kule Zanzibar huwa kuna mtu anashinda lakini hapewi kwa kuhofia hatma ya muungano, Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda

This time nimeisikia sauti hii Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke

Kwa vile Mama Samia ni mtu wa haki bin haki this time mshindi atapewa, hivyo acheni hizi kelele za kuutishia muungano na safari hii akanyimwa tena!.

P
 
Kuna watu mnabwabwaja na hamjui chuki hii ya kuukataa muungano inazalishwaje... ungepata nafasi ya kujua hilo hakika utaukataa muungano.. do your home work. Anza na teuzi za be tozo ndani ya bara na tabia za wateule.
Mzee Paskal nawe unarukaruka mlemle Tanganyika na Zanzibar kazaa Tanzania wakati Zanzibar inaendelea kudai kubaki yai na ihudumiwe kama yai.
 
Kimsingi Wazanzibar ndio wenye haki ya kulalamika na siyo Watanganyika.

Population yao ni ndogo sana, ni aibu kwa Mtanganyika kuwalalamikia Wazanzibar wakati power zote zipo Tanganyika.
Hii ni kweli. Zanzibar kila mtu mmoja unaweza kumpa police hapo shida iko wapi
 
Sioni tatizo lolote kuhusu Ardhi, kuttouziwa wabara. Zanzibar ni ndogo na tukiruhusiwa tutaininuwa yote na wao hawatakuwa na kitu kilichobaki. Na tukivunja muungano watafurahi sana.
 
Naombea Muungano uvunjike Fasta hata leo. Hauna manufaaa kwa sisi Watanganyika.
 
Sisi wa zanzibari tupo wachache lakini tunapinga kukandamiziwa na mkubwa yoyote
Wanaowakandamiza ni wenzenu wanaolamba asali Bara, amkeni mgawane majukumu muwadhibiti
 
Mkuu 'Mwanga Mkali', sitakudharau kama ulivyonidharau mimi kwa kudhani nina akili hafifu kuliko ulizonazo wewe.

Umejuaje kuwa "sijui chuki zinazalishwaje"?

Kwani katika maelezo yangu hapo juu umesoma nikieleza kwamba hayo yote uliyoyataja siyajui? Mbona nimeeleza kwamba ni sababu hafifu sana kwa watu wenye akili kuzitumia kama sababu za kuuvunja muungano!

Hayo uliyoyaeleza na huyo anayeyafanya ndiyo mwenye mali miliki ya muungano?
Huoni kwamba unajidhalilisha mwenyewe hapa na kudhani kuwa muungano ni mali ya huyo mtu tena asiyekuwa na uwezo kamili wa uongozi, kama ulivyoonyesha mwenyewe?

Haya mambo msiwe mnayarukia tu bila kuyaelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…