Harakati za Daudi kuwania Ufalme zinatupa Somo gani katika Siasa na namna ya kuepa Kuuawa?

Yeyeto aliyemuua Mdude, hana akili hata kidogo au niseme ni mpumbavu wa wapumbavu. Mdude hakuwa tishio kwa utawala hata kidogo. Mdude kwanza siyo wale watu waliokuwa na ushawishi au kuwavuta watu wengi. Kama laana zipo kweli basi muuaji wa Mdude ametafuta laana za bure.
Bado najiuliza na sipati jibu 😳🙄
Hivi hizi conspiracy theories ni za kweli au au ni mambo ya kusadikika tu ??!!
Najiuliza tena Why and How tumeweza kufika hapa kama ni kweli ??! 😳🙄
 
Kwanza tuliandaliwa kuto kuhoji na tatizo la kuhoji linaanzia kwenye ngazi ya familia kuna vitu ukihoji utaambiwa kama umekua uondoke

Tabia ya kukataa kuhojiwa imebebwa kwenye ngazi zote za maisha ndiyo maana wadau waliojaribu kuhoji kuhusu tozo za kwenye simu waliambiwa kama hawataki kulipa tozo waende burundi

Tunaishi kwenye jamii ya kanyanga twende jamii ambayo unaweza kuisafisha ubongo ikafikiri unavyotaka wewe jamii ambayo watu wengi hawawezi kuchakata fikra chanya na hasi

Unyumbu wa kisiasa ni mfumo kandamizi ambao unatumika na CCM ambao unaruhusi wanaopewa dhamamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza ama kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi na uoga wa kuigiza kwa viongozi wao, (unafiki)

Wanyama nyumbu huongozana kwenye msafara wa kundi lao bila kuangalia hatari watakayo kutana nayo nyumbu hupita kwenye makolongo na mito yenye mamba wakali tena wenye njaa bila kupanga jinsi watakavyo kabiliana na mamba, (no SMART goals settings)

Nyumbu wakifika kwenye hiyo mito huona hatari, huwaona mamba lakini huamua kwenda tu, (kujizima data), atakaye jeruhiwa ama kuliwa shauri yake, (ndiyo mtizamo wa CCM)
 
Che Guevara alisemaga “ it’s better to die standing than to live kneeling “
🤣🤣🤣 hapo alimaanisha nini ??!! 😳🤣🤣 !
Kila mtu na falsafa yake mukichwa 🙌🤷‍♂️ !

Hakunaga kufa kishujaa.
Shujaa lazima uhakikishe unabaki hai. Hiyo ni kanuni ambayo Master aliyebobea lazima akufundishe.
 
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Ni kweli kabisa Hakuna ufalme au utawala usiotoka kwa Mungu. Huo utawala haupo.
Hata watawala wenyewe wanajua Jambo Hilo kutokana na maisha Yao walikotoka na walipo hivi Leo.

Niliwahi msikiliza Magufuli na pia Rais Samia mwenyewe alishawahi kukiri kuwa hakuwa na uhakika kwamba siku moja angekuja kuwa Rais wa nchi.
Jambo moja ambalo linajirudiarudia kwenye utawala ni kuwa kila mtawala mpya anapoingia watu huachwa midomo wazi na kutoamini kuwa Fulani kweli amekuwa Rais au Mfalme.
Hii ni kiashiria kuwa utawala wa mwanadamu unatoka kwa Mungu mwenyewe.

Kikawaida Mungu huwainua wale ambao wengi huwaona hawana sifa za kimwili kuwa katika nafasi Fulani kubwa na kuwanyima wale wanaoonekana wanasifa za kimwili machoni pawatu.

Ni watu wangapi unawajua wanaakili na sifa Bora kabisa lakini wanazidiwa na kuongozwa na wale unaowaona hawana sifa za kuongoza au watawala?

Nirudi kwenye hoja. Kama wewe ni mwanasiasa mchanga na unandoto kubwa basi itakupasa uanze kufuatilia Kisa cha Daudi kwa Ukaribu Sana.

Wasifu wa Daudi kwa ufupi ni kama ifuatavyo;

1. Lastborn kwenye Familia ya Yese Babaake mwenye watoto nane.

2. Mwenye umbo dogo, mwenye Sura nzuri, na rangi nyekundu.

3. Kazi yake ilikuwa uchungaji wa mifugo ya Babaake.

4. Vipaji; Alikuwa mwanamuziki(muimbaji, mtunzi wa ushairi, na mpigaji kinubi)

5. Ujuzi wa ziada, alikuwa mpiganaji lakini ambaye hakuwa na sifa za kujiunga na jeshi.

6. Alitoka kwenye Familia ya kipato cha kawaida. Alipenda kujiita Mtoto wa Maskini.

7. Sifa za ndani. Alikuwa na AKILI, HEKIMA NA BUSARA Sana.
8. Alikuwa mpole na Mchamungu.

Hizo ni sifa za Daudi kabla hajawa Mfalme.

Harakati zake za Kisiasa kuwania utawala na kuwa Mfalme;

1. Daudi anapakwa mafuta Kisiri na Nabii Samweli.
Alipakwa Mafuta ili awe Mfalme ilhali tayari alikuwepo Mfalme anayetawala. Yaani ni sawa sasa hivi Rais Samia yupo Madarakani alafu atawazwe kisiri Rais mwingine.
Ukisoma kisa hiki utaona Nabii Samweli ndiye huyohuyo aliyempaka mafuta Mfalme Sauli aliyepo madarakani.

Wakati Mungu anamtuma Nabii Samweli Kumpaka mafuta Daudi ili awe mfalme badala ya Mfalme Sauli. Samweli anaogopa kuuawa na Mfalme Sauli.
Kuogopa ni sifa ya kibinadamu ambayo hat manabii wanayo.
Nabii Samweli anamwambia Mungu, ni kweli umenituma nikampake Daudi mafuta awe Mfalme lakini naogopa kuuawa na Mfalme Sauli atakapoipata habari hii.

Mungu anampa maarifa na mbinu ya kwenda kumpaka mafuta Daudi bila Sauli kujua kwa haraka.
Hapa tunajifunza kuwa kuwa MTU wa Mungu, hata kwa kiwango cha Nabii haimaanishi usitumie Akili kujilinda na kujihami.
Na Mungu anataka utumie akili alizokupa kulinda baraka ya Uhai aliokupa.
Fikiria Nabii Samweli ametumwa na Mungu, lakini anaogopa mfalme sauli aliyempaka Mafuta yeye mwenyewe.
Ingekuwa ni Mtu mpumbavu angesema naenda hivyohivyo, siogopi kima kwani nimetumwa na Mungu.
Kutumwa na Mungu sio kisingizio cha kutotumia akili.

Daudi anatawazwa kuwa Mfalme Kisiri.

2. Daudi licha ya kutawazwa lakini anakuwa na subira ya kusubiri wakati wa Mungu kuwa Mfalme. Hakumsumbua Mfalme Sauli.
Kisa kinaonyesha Daudi tangu amepakwa mafuta awe mfalme amekaa uraiani zaidi ya miaka na miaka.
Hakuwa na haraka, subira.

Huenda ingekuwa mwenzangu na miye hapa tayari nimeshapakwa mafuta na ninajua ninaenda kuwa mfalme/Rais tayari ungeniona naanza kusumbuana na utawala wa Samia. Lakini Daudi kimya. Kama sio yeye.

Mpaka anakuja kumpiga Goliathi mwaka mmoja baadaye. Kapiga Goliathi na bado akasota zaidi ya Miaka na miaka bila kuwa Mfalme.

3. Kutenda kwa Akili na Busara.
Siasa zinahitaji akili nyingi na busara za kutosha. Hasa ukiwa underdog. Daudi kwenye huu mtanange alikuwa underdog wakati anatakiwa kumtoa Mfalme aliyeko madarakani.
Embu fikiria hapo wewe unawezaje kumshinda Rais Samia umtoe ili wewe uwe Raia badala yake.
Wakati wewe ni maskini usiye na kitu Rais anakila kitu. Anajeshi, anapesa, na vyombo vyote vya dola vilivyopo kisheria na vile ambavyo visivyo kisheria ambavyo huvijui vyote vipo chini yake. Unamshindaje?
Kimsingi haiwezekani kumshinda.

Daudi tayari anakura ya Mungu lakini kumbuka hata Mfalme Sauli aliyepo madarakani alikuwa na hiyohiyo Kura ya Mungu. Sema baada ya Mfalme Sauli kukoseakosea ndipo Mungu akahamisha Kura kwa Daudi.

Licha ya Mungu kuhamishia Kura kwa Daudi lakini Kisa kinaeleza kuwa Daudi alitenda kwa akili na busara mambo yake siku zote.
Hiyo inatufundisha sisi hasa wale wanasiasa wenye ndoto ya kuwa watawala kuwa hata uwe na kura ya Mungu na sifa zingine za ziada ni lazima ujue kutenda kwa akili mingi na Busara. Ingawaje usiache HAKI.

4. Usipambane na Utawala.
Acha utawala upambane na wewe kutokana na kazi zako njema. Lakini usifanye intentionally kupambana na serikali.
Hakuna aliyewahi kupambana na serikali akashinda isipokuwa Nabii Musa, tena katika mazingira maalumu.

Daudi yeye licha ya kujua yeye ni mfalme mtarajiwa hakutumia nafasi hiyo kumchallenge mfalme aliyepo madarakani.
Hakuwa na dhamiri ya kupambana na mfalme. Zaidi alikuwa akimsaidia mfalme aliyepo madarakani ili atawale vizuri.
Lakini kumbe vile anavyomsaidia mfalme sauli ndivyo anavyopata umaarufu kwa watu na jambo hilo linamfanya Mfalme sauli kupatwa na wivu.
Hiyo inapelekea Mfalme Sauli kufanya majaribio yasiyopungua matatu kutaka kumuua Daudi.

Hali hiyo ya kumsaidia mfalme imejitokeza pia kwa Yusufu ambaye baadaye alikuja kuwa Mfalme. Pia ilijitokeza kwa Musa alipokimbilia Nchi ya Kushi, naye akawa mfalme huko Kushi.
Hakuwahi kupambana na Mfalme kwa dhamiri.

Visa vyote hivyo vinatufundisha ukiwa underdog hupaswi kupambana na ufalme hasa wa taifa lako kwani uwezekano wa kushinda ni kama sifuri. Labda katika mazingira maalumu na hiyo huwaga ni exceptional Cases

4. Kuwa na Intelejensia Kali(Ujasusi).
Ukiwa smart, mwenye busara, usiyetaka kushindana, mwenye dhamiri safi, mwenye haki. Lazima watu watajua tuu. Hata kama kuna ubaya unapangwa juu yako watatokea watu kutoka hukohuko ubaya unapopangwa watakujulisha ukimbie.
Pia kwenye hivyohivyo vikao vya kukuangamiza watatokea watu watakaokutetea kwa mfalme au Mtawala kwa namna yoyote ilimradi usipatwe na madhara makubwa hasa ya kugharimu uhai wako.

Daudi anataka kuuawa na Mfalme Sauli, kwa mkono wa Mfalme mwenyewe Daudi amekoswa mara tatu. Huku Yonathani Mtoto wa Mfalme Sauli akihusika kumpa taarifa Daudi kuwa ajichunge Sana kwani Mfalme Sauli yuataka kumuua.

Mara zingine, Mikali binti mfalme anamtorosha Daudi kabla wauaji waliotumwa na Babake ndiye mfalme Sauli kuja kumuua Daudi.

Ni muhimu kuzipata taarifa za kintelejensia kwa usalama wako.
Lakini lazima ujue kuzipata taarifa hizo ni kazi ngumu na kama ni pesa utahitajika pesa nyingi Sana. Lakini ukiwa mwenye haki na dhamiri safi ni hakika utajikuta unapata watu wema watakaokuokoa. Au haohao wabaya watakusaidia kukuokoa.

5. KUKIMBIA KUJIOKOA NI MBINU MUHIMU IKIBIDI.
Kukimbia kujiokoa sio dhambi wala sio uoga.
Kwenye Masha yako jukumu namba moja katika maisha yako ni kulinda uhai wako kwa gharama yoyote ikibidi kuvunja Sheria. Uhai Kwanza mengine ndio yanafuata.
Usije ukawa mjinga wa kujitoa mhanga na kudhulumu maisha yako kienyeji. Fanya ufanyavyo lakini uhai ubaki nao.

Lazima ujue, mashujaa hawauawi bali shujaa huishi.
Daudi ni shujaa kwa sababu ameyaokoa maisha yake mara kadhaa kwa mbinu mbalimbali. Ikiwemo kukimbia ikibidi.
Mashujaa wengine ni kama Musa, Ibrahim, n.k.

Sio unaona maisha yako yapo hatarini badala usepe unakuwa kama mjingamjinga.
Kumbuka Mungu mwenyewe hawi radhi na wajingawajinga.

Labda itokee katika mazingira maalumu.

Kufikia hapo Taikon Master sina la ziada.

Robert Heriel
Taikon Master
Dar es salaam
Daudi hakua mtoto wa mwisho bali alikuwa mtoto wa nje mtoto wa suria
 
1 Samweli 17:13-14
[13]Nao wale wana watatu wa Yese waliokuwa wakubwa walikuwa wamefuatana na Sauli kwenda vitani, na majina ya hao wanawe watatu waliokwenda vitani ni haya, mzaliwa wa kwanza Eliabu, na wa pili wake Abinadabu, na wa tatu Shama.

[14]Naye huyo Daudi alikuwa mdogo wa wote; na hao watatu waliokuwa wakubwa wakafuatana na Sauli.
 
Kwanza tuliandaliwa kuto kuhoji na tatizo la kuhoji linaanzia kwenye ngazi ya familia kuna vitu ukihoji utaambiwa kama umekua uondoke

Tabia ya kukataa kuhojiwa imebebwa kwenye ngazi zote za maisha ndiyo maana wadau waliojaribu kuhoji kuhusu tozo za kwenye simu waliambiwa kama hawataki kulipa tozo waende burundi

Tunaishi kwenye jamii ya kanyanga twende jamii ambayo unaweza kuisafisha ubongo ikafikiri unavyotaka wewe jamii ambayo haiwezi kuchakata fikra chanya na hasi

Unyumbu wa kisiasa ni mfumo kandamizi ambao unatumika na CCM ambao unaruhusi wanaopewa dhamamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza ama kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi na uoga wa kuigiza kwa viongozi wao, (unafiki)

Wanyama nyumbu huongozana kwenye msafara wa kundi lao bila kuangalia hatari watakayo kutana nayo nyumbu hupita kwenye makolongo na mito yenye mamba wakali tena wenye njaa bila kupanga jinsi watakavyo kabiliana na mamba, (no SMART goals settings)

Nyumbu wakifika kwenye hiyo mito huona hatari, huwaona mamba lakini huamua kwenda tu, (kujizima data), atakaye jeruhiwa ama kuliwa shauri yake, (ndiyo mawazo ya CCM)
Duh 🙄 !
Hii ni kali Kwakweli !
Sasa kama hii kitu iko hivi itakwenda hivi hivi mpaka lini ??!
 
Kwenye hii dunia hakuna kinachodumu.
Mwisho wa wote ni kifo.
Then baada ya kifo anayejua ni Yule mwenye nguvu injinia wa maisha
Mwenye nguvu injinia wa maisha, mwenye uwezo usiowezwa na yeyote yule 🙌🙏🙏💯✅ !

Lakini wapo wengine wenye kupenda kujizima Data Wanasemaga kwenye Siasa hakuna Mungu 😳😳🙄🙄🤷‍♂️ !
 
Kwanza tuliandaliwa kuto kuhoji na tatizo la kuhoji linaanzia kwenye ngazi ya familia kuna vitu ukihoji utaambiwa kama umekua uondoke

Tabia ya kukataa kuhojiwa imebebwa kwenye ngazi zote za maisha ndiyo maana wadau waliojaribu kuhoji kuhusu tozo za kwenye simu waliambiwa kama hawataki kulipa tozo waende burundi

Tunaishi kwenye jamii ya kanyanga twende jamii ambayo unaweza kuisafisha ubongo ikafikiri unavyotaka wewe jamii ambayo haiwezi kuchakata fikra chanya na hasi

Unyumbu wa kisiasa ni mfumo kandamizi ambao unatumika na CCM ambao unaruhusi wanaopewa dhamamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza ama kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi na uoga wa kuigiza kwa viongozi wao, (unafiki)

Wanyama nyumbu huongozana kwenye msafara wa kundi lao bila kuangalia hatari watakayo kutana nayo nyumbu hupita kwenye makolongo na mito yenye mamba wakali tena wenye njaa bila kupanga jinsi watakavyo kabiliana na mamba, (no SMART goals settings)

Nyumbu wakifika kwenye hiyo mito huona hatari, huwaona mamba lakini huamua kwenda tu, (kujizima data), atakaye jeruhiwa ama kuliwa shauri yake, (ndiyo mawazo ya CCM)
Hii Comment yako Inafikirisha sana tena sana !
Wenye Akili timamu inabidi wapate mazingatio humu ili siku moja huenda wakaja na muarobaini wa kuiponya Nchi !
Naona kama sasa tunataka kwenda Harijojo 😳 yaani tunakwenda ndiko siko 😳🙄🙌🤷‍♂️ !
 
Kujizima data
 
Duh 🙄 !
Hii ni kali Kwakweli !
Sasa kama hii kitu iko hivi itakwenda hivi hivi mpaka lini ??!
Mimi nimefuatilia sababu ni jamii kunyamaza, swali je jamii itaendelea kunyamaza hadi lini na mdharq ya jamii kunyamaza ni kusalimu amri kwa majukumu ya kijamii ama kitaifa

Silence surrenders public responsibilities
 
Mtu anaruhusiwa kufikiri lolote
Siyo kufikiri lolote bali kujizima data, yaani kuahirisha kufikiri, bakuri atakwambia ni sufuria mavi atakwambua ni ugali pia kuna kundi ambalo linafurahia watu kupata madhara ama matatizo, 'pessimistic' people

Tanzania tunaongozwa na wapumbavu

Tanzania upumbavu ni kipaji, mpumbavu ni mtu aliyebobea kwenye jambo fulani lakini halifanyi kwa weledi
 
Siyo kufikiri lolote bali kujizima data, yaani kuahirisha kufikiri, bakuri atakwambia ni sufuria mavi atakwambua ni ugali pia kuna kundi ambalo linafurahia watu kupata madhara ama matatizo, 'pessimistic' people
Duh 🙄 !
 
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Ni kweli kabisa Hakuna ufalme au utawala usiotoka kwa Mungu. Huo utawala haupo.
Hata watawala wenyewe wanajua Jambo Hilo kutokana na maisha Yao walikotoka na walipo hivi Leo.

Niliwahi msikiliza Magufuli na pia Rais Samia mwenyewe alishawahi kukiri kuwa hakuwa na uhakika kwamba siku moja angekuja kuwa Rais wa nchi.
Jambo moja ambalo linajirudiarudia kwenye utawala ni kuwa kila mtawala mpya anapoingia watu huachwa midomo wazi na kutoamini kuwa Fulani kweli amekuwa Rais au Mfalme.
Hii ni kiashiria kuwa utawala wa mwanadamu unatoka kwa Mungu mwenyewe.

Kikawaida Mungu huwainua wale ambao wengi huwaona hawana sifa za kimwili kuwa katika nafasi Fulani kubwa na kuwanyima wale wanaoonekana wanasifa za kimwili machoni pawatu.

Ni watu wangapi unawajua wanaakili na sifa Bora kabisa lakini wanazidiwa na kuongozwa na wale unaowaona hawana sifa za kuongoza au watawala?

Nirudi kwenye hoja. Kama wewe ni mwanasiasa mchanga na unandoto kubwa basi itakupasa uanze kufuatilia Kisa cha Daudi kwa Ukaribu Sana.

Wasifu wa Daudi kwa ufupi ni kama ifuatavyo;

1. Lastborn kwenye Familia ya Yese Babaake mwenye watoto nane.

2. Mwenye umbo dogo, mwenye Sura nzuri, na rangi nyekundu.

3. Kazi yake ilikuwa uchungaji wa mifugo ya Babaake.

4. Vipaji; Alikuwa mwanamuziki(muimbaji, mtunzi wa ushairi, na mpigaji kinubi)

5. Ujuzi wa ziada, alikuwa mpiganaji lakini ambaye hakuwa na sifa za kujiunga na jeshi.

6. Alitoka kwenye Familia ya kipato cha kawaida. Alipenda kujiita Mtoto wa Maskini.

7. Sifa za ndani. Alikuwa na AKILI, HEKIMA NA BUSARA Sana.
8. Alikuwa mpole na Mchamungu.

Hizo ni sifa za Daudi kabla hajawa Mfalme.

Harakati zake za Kisiasa kuwania utawala na kuwa Mfalme;

1. Daudi anapakwa mafuta Kisiri na Nabii Samweli.
Alipakwa Mafuta ili awe Mfalme ilhali tayari alikuwepo Mfalme anayetawala. Yaani ni sawa sasa hivi Rais Samia yupo Madarakani alafu atawazwe kisiri Rais mwingine.
Ukisoma kisa hiki utaona Nabii Samweli ndiye huyohuyo aliyempaka mafuta Mfalme Sauli aliyepo madarakani.

Wakati Mungu anamtuma Nabii Samweli Kumpaka mafuta Daudi ili awe mfalme badala ya Mfalme Sauli. Samweli anaogopa kuuawa na Mfalme Sauli.
Kuogopa ni sifa ya kibinadamu ambayo hat manabii wanayo.
Nabii Samweli anamwambia Mungu, ni kweli umenituma nikampake Daudi mafuta awe Mfalme lakini naogopa kuuawa na Mfalme Sauli atakapoipata habari hii.

Mungu anampa maarifa na mbinu ya kwenda kumpaka mafuta Daudi bila Sauli kujua kwa haraka.
Hapa tunajifunza kuwa kuwa MTU wa Mungu, hata kwa kiwango cha Nabii haimaanishi usitumie Akili kujilinda na kujihami.
Na Mungu anataka utumie akili alizokupa kulinda baraka ya Uhai aliokupa.
Fikiria Nabii Samweli ametumwa na Mungu, lakini anaogopa mfalme sauli aliyempaka Mafuta yeye mwenyewe.
Ingekuwa ni Mtu mpumbavu angesema naenda hivyohivyo, siogopi kima kwani nimetumwa na Mungu.
Kutumwa na Mungu sio kisingizio cha kutotumia akili.

Daudi anatawazwa kuwa Mfalme Kisiri.

2. Daudi licha ya kutawazwa lakini anakuwa na subira ya kusubiri wakati wa Mungu kuwa Mfalme. Hakumsumbua Mfalme Sauli.
Kisa kinaonyesha Daudi tangu amepakwa mafuta awe mfalme amekaa uraiani zaidi ya miaka na miaka.
Hakuwa na haraka, subira.

Huenda ingekuwa mwenzangu na miye hapa tayari nimeshapakwa mafuta na ninajua ninaenda kuwa mfalme/Rais tayari ungeniona naanza kusumbuana na utawala wa Samia. Lakini Daudi kimya. Kama sio yeye.

Mpaka anakuja kumpiga Goliathi mwaka mmoja baadaye. Kapiga Goliathi na bado akasota zaidi ya Miaka na miaka bila kuwa Mfalme.

3. Kutenda kwa Akili na Busara.
Siasa zinahitaji akili nyingi na busara za kutosha. Hasa ukiwa underdog. Daudi kwenye huu mtanange alikuwa underdog wakati anatakiwa kumtoa Mfalme aliyeko madarakani.
Embu fikiria hapo wewe unawezaje kumshinda Rais Samia umtoe ili wewe uwe Raia badala yake.
Wakati wewe ni maskini usiye na kitu Rais anakila kitu. Anajeshi, anapesa, na vyombo vyote vya dola vilivyopo kisheria na vile ambavyo visivyo kisheria ambavyo huvijui vyote vipo chini yake. Unamshindaje?
Kimsingi haiwezekani kumshinda.

Daudi tayari anakura ya Mungu lakini kumbuka hata Mfalme Sauli aliyepo madarakani alikuwa na hiyohiyo Kura ya Mungu. Sema baada ya Mfalme Sauli kukoseakosea ndipo Mungu akahamisha Kura kwa Daudi.

Licha ya Mungu kuhamishia Kura kwa Daudi lakini Kisa kinaeleza kuwa Daudi alitenda kwa akili na busara mambo yake siku zote.
Hiyo inatufundisha sisi hasa wale wanasiasa wenye ndoto ya kuwa watawala kuwa hata uwe na kura ya Mungu na sifa zingine za ziada ni lazima ujue kutenda kwa akili mingi na Busara. Ingawaje usiache HAKI.

4. Usipambane na Utawala.
Acha utawala upambane na wewe kutokana na kazi zako njema. Lakini usifanye intentionally kupambana na serikali.
Hakuna aliyewahi kupambana na serikali akashinda isipokuwa Nabii Musa, tena katika mazingira maalumu.

Daudi yeye licha ya kujua yeye ni mfalme mtarajiwa hakutumia nafasi hiyo kumchallenge mfalme aliyepo madarakani.
Hakuwa na dhamiri ya kupambana na mfalme. Zaidi alikuwa akimsaidia mfalme aliyepo madarakani ili atawale vizuri.
Lakini kumbe vile anavyomsaidia mfalme sauli ndivyo anavyopata umaarufu kwa watu na jambo hilo linamfanya Mfalme sauli kupatwa na wivu.
Hiyo inapelekea Mfalme Sauli kufanya majaribio yasiyopungua matatu kutaka kumuua Daudi.

Hali hiyo ya kumsaidia mfalme imejitokeza pia kwa Yusufu ambaye baadaye alikuja kuwa Mfalme. Pia ilijitokeza kwa Musa alipokimbilia Nchi ya Kushi, naye akawa mfalme huko Kushi.
Hakuwahi kupambana na Mfalme kwa dhamiri.

Visa vyote hivyo vinatufundisha ukiwa underdog hupaswi kupambana na ufalme hasa wa taifa lako kwani uwezekano wa kushinda ni kama sifuri. Labda katika mazingira maalumu na hiyo huwaga ni exceptional Cases

4. Kuwa na Intelejensia Kali(Ujasusi).
Ukiwa smart, mwenye busara, usiyetaka kushindana, mwenye dhamiri safi, mwenye haki. Lazima watu watajua tuu. Hata kama kuna ubaya unapangwa juu yako watatokea watu kutoka hukohuko ubaya unapopangwa watakujulisha ukimbie.
Pia kwenye hivyohivyo vikao vya kukuangamiza watatokea watu watakaokutetea kwa mfalme au Mtawala kwa namna yoyote ilimradi usipatwe na madhara makubwa hasa ya kugharimu uhai wako.

Daudi anataka kuuawa na Mfalme Sauli, kwa mkono wa Mfalme mwenyewe Daudi amekoswa mara tatu. Huku Yonathani Mtoto wa Mfalme Sauli akihusika kumpa taarifa Daudi kuwa ajichunge Sana kwani Mfalme Sauli yuataka kumuua.

Mara zingine, Mikali binti mfalme anamtorosha Daudi kabla wauaji waliotumwa na Babake ndiye mfalme Sauli kuja kumuua Daudi.

Ni muhimu kuzipata taarifa za kintelejensia kwa usalama wako.
Lakini lazima ujue kuzipata taarifa hizo ni kazi ngumu na kama ni pesa utahitajika pesa nyingi Sana. Lakini ukiwa mwenye haki na dhamiri safi ni hakika utajikuta unapata watu wema watakaokuokoa. Au haohao wabaya watakusaidia kukuokoa.

5. KUKIMBIA KUJIOKOA NI MBINU MUHIMU IKIBIDI.
Kukimbia kujiokoa sio dhambi wala sio uoga.
Kwenye Masha yako jukumu namba moja katika maisha yako ni kulinda uhai wako kwa gharama yoyote ikibidi kuvunja Sheria. Uhai Kwanza mengine ndio yanafuata.
Usije ukawa mjinga wa kujitoa mhanga na kudhulumu maisha yako kienyeji. Fanya ufanyavyo lakini uhai ubaki nao.

Lazima ujue, mashujaa hawauawi bali shujaa huishi.
Daudi ni shujaa kwa sababu ameyaokoa maisha yake mara kadhaa kwa mbinu mbalimbali. Ikiwemo kukimbia ikibidi.
Mashujaa wengine ni kama Musa, Ibrahim, n.k.

Sio unaona maisha yako yapo hatarini badala usepe unakuwa kama mjingamjinga.
Kumbuka Mungu mwenyewe hawi radhi na wajingawajinga.

Labda itokee katika mazingira maalumu.

Kufikia hapo Taikon Master sina la ziada.

Robert Heriel
Taikon Master
Dar es salaam
Sauli alipojua tu Huenda Daudi akawa mfalme wa Israeli alianza kusakwa.....vyombo vya dola vya Mfalme Sauli vilitumia kila mbinu.

Luck enough kumbe Mtoto wa Sauli Aitywayee Nathani alikuuwa anampenda sana Kijana mwenzie Daudi. Akawa anampenyezea taarifa kutoka Ikulu Ya mfalme pale Giboa kwa Wayebusi
 
Yeyeto aliyemuua Mdude, hana akili hata kidogo au niseme ni mpumbavu wa wapumbavu. Mdude hakuwa tishio kwa utawala hata kidogo. Mdude kwanza siyo wale watu waliokuwa na ushawishi au kuwavuta watu wengi. Kama laana zipo kweli basi muuaji wa Mdude ametafuta laana za bure.
Kauawa?
 
Ni kweli utawala wa CCM umekwisha fitinika kwa sasa wako madarakani kwa muda wa kuazima tu, kinachotakiwa kwa mujibu wa mleta mada ni kwenda kwa timing tu kama kumchinja kobe.
 
Back
Top Bottom