Harakati za kusaka wadhamini zinakiuka sheria ya uchaguzi chapter 343

Harakati za kusaka wadhamini zinakiuka sheria ya uchaguzi chapter 343

eddy

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2007
Posts
17,079
Reaction score
12,312
Kitendo cha kukodi gari la matangazo kupita mitaani kuhamasisha watu, kuandaa jukwaa na kuhutubia kwa zaidi ya saa nzima huku ukijitapa namna serikali yako itakavyokuwa na kujaribu kukosoa serikali iliyopo madarakani kwangu hiyo ni kampeni, unaposema serikali yangu mtakayoichagua wakati ukijua wazi haujateuliwa kuwa mgombea urais kwa mujibu huo ni ukiukwaji wa kifungu namba 31 cha sheria ya uchaguzi chapter 343, ila nimejaribu kuangalia adhabu inayomstahili mtu aliyejitangaza mwenyewe kuwa mgombea urais sijaiona

Hivyo ipo haja ya kupitia upya kanuni za maadili ya uchaguzi, ili kuwepo na uwanja sawa wa ushindani kisiasa. Haingii akilini mtu anatafuta wadhani huku akiwa amekodi ngoma ya ritungu akipita sokoni na midundo ya muziki hii sio sawa. Tunawasihi wanasiasa katika shughuli zao wasibugudhi shughuli za kijamii na kiuchumi, ukitaka kuhutubia nenda kwenye uwanja jenga jukwaa lako hutubia na sio kwenda sokoni vituo vya mabasi kandokando mwa barabara na kuanza kukusanya watu na kutatiza shughuli za kiuchumi.

Nimemsikia mheshimiwa akihamasisha watu wanapokwenda kuchukua form za ubunge na udiwani waende na misururu ili wasijeporwe form, huku ni kuhamasisha uvunjifu wa amani na mikusanyiko haramu, kama mtu anawasiwasi wa kuporwa form basi aombe escort ya polisi na sio kuhamasisha vurugu, nimeona mitandaoni watu wakiandamana kwenda kuchukua form ili sio jambo la kupuuza ikitokea bahati mbaya form akaikosa basi panaweza tokea vurugu. nasikia kuna mtu alipigwa kwa kudhaniwa anataka kupora form ya udiwani, hii inaweza chagizwa na kauli za majukwaani za hawa wasaka udhamini wa urais, kama ulipata wadhamini wa chama kimyakimya tena ukiwa ulaya sasa kinachokufanya uanze kuzurura na ngoma ya ritungu ni nini kama sio kutaka shari?
 
Kwani mlipo mpiga Risasi Tundu Lissu ndio ulikuwa utawala wa Sheria? Na mlipo muua Alphonce Mawazo, Azori, Ben Saanane mlikuwa mnafuata Katiba?

Au mlipo waengua wagombea wote wa upinzani ktk serikali za mitaa mlikuwa mnafuata sheria?Au mlipo muwekea SUMU Mangula mlikuwa mnafuata sheria?

Mataga tulieni tuu msumari hutolewa pale pale ulipo ingilia.
 
Kwani mlipo mpiga Risasi Tundu Lissu ndio ulikuwa utawala wa Sheria? Na mlipo muda Mawazo, Azori, Ben Saanane mlikuwa mkafuata Katiba?

Au mlipo waengua wagombea wote wa upinzani ktk serikali za mitaa mlikuwa mnafuata sheria?Au mlipo muweka SUMU Mangula mlikuwa mnafuata sheria?
Hizo Ni porojo wananchi wanataka maji barabara umeme,
 
Nauliza tu!!rais wa JMT kwa sasa ni nani according to our constitution? Tuanzie hapo ndipo wanaotukana waje na hoja
 
Mkuu Eddy, wenzio huwa wanaweka kabisa na namba zao za simu ili kuweka kumbukumbu sawa kwa siku za baadaye. Lakini pia huwa wananogesha kidogo mada kwa kuweka lugha za matusi na zisizokuwa na staha kwa yule ambaye ni tishio kwao ili wapate kongole zaidi.
 
Ukiona mtu anaandika topic kwa kirefu namna hii, basi ujue huyo ni CCM anataka kulazimisha kueleweka na kupinda maneno. Points ni short and clear
Maccm hayana akili kabisa......

Leo rais alikua kanisani TAG anapiga kampeni lkn hili hawasemi kabisaaa.......
 
Sheria ipi inazuia kusindikizwa kwenda kuchukua form za uchaguzi/uteuzi?
 
Kwa hiyo kupiga risasi na uchunguzi usifanyike ndio sheria. Very hopeless.
 
Tatizo unaosema watoe escort hawaaminiki,ndio maana leo Sugu wamemkamata Mbeya.
Wewe angalau ungesema wajilinde wenyewe pamoja na fomu zao.
 
Back
Top Bottom