Wakuu subirini kwanza nichomoe betri.
Ipo hivi katika maisha kila mmoja huja kwako kwa lengo la kukufikisha sehemu fulani katika maisha yako au kukufundisha kitu fulani katika maisha yako, na watu hawa wapo wale wanaoendelea kukaa katika maisha yako ili kutimiza lile kusudi la wao kuwepo na muda wao ukiisha huwa wanaondoka.
Tatizo letu sisi wanadamu huwa tunataka waendelee kuwepo tukidhani bado unawahitaji either kwasababu ya hisia zako au hali yako kwake. Hapa huwa tunakosea sana.
Kama umemsaidia mtu elewa kuwa ulikuwa ni miongoni mwa watu ambao Mungu alipanga kuwa kama baraka katika maisha yao na wewe kujifunza kitu ama kupata thawabu fulani ambayo sometimes unaweza usiione kwa macho.
Usilazimishe mtu kuwepo katika maisha yako kisa ulimsaidia mkuu, ulifanya kwa moyo na Mungu aliliona hilo hivyo huitaji kukumbukwa ili kupata faraja, hapana unapaswa kulitazama hilo katika macho ya tofauti.
Elewa siyo kila mtu anaekuja katika maisha yako atakuwepo milele, sahau hilo ndo maana hata mzazi inafikia hatua kutokana na umri wa mwanae inabidi bahadhi ya vitu anasitisha kufanya kwa mwanae. Watu wanakuwepo ili kukufanya wewe kuwa sehemu fulani kimaisha baada ya hilo usitegemee tena yeye kuendelea kuwepo, kama ikitokea kuendelea kuwepo basi jua kuna kusudi lingine la yeye kuwepo na kusudi hilo laweza kuwa zuri au baya ili kujifunza au kupata uzoefu fulani.
Kukosa uelewa wa mambo kama haya ndo chanzo cha kujengeana chuki zisizosaidia mwisho wa siku ndo mwanzo wa undugu kuvunjika na ndivyo ambavyo vizazi vinavyofuata kuendelea kutengana.
Kama lengo lako la kumsaidia mtu ni kutegemea malipo fulani either ya yeye kuendelea kuwepo katika maisha yako au malipo mengine yoyote basi jua huo msaada hautoki ndani ya moyo wako unafanya under influence.
Narudisha betri.