Hard times will always reveal true friends

Hard times will always reveal true friends

Nimepata ajali ya bodaboda.
Gari ya kwanza kufika eneo la tukio lilikuwa la wanangu. Wakaambiwa wabebeni majeruhi muwaacha hospital ya karibu, wakajibu wanawahi kwenye party. Wakaniaga kabisa.

Nilibebwa na nisio wajua, wakanifikisha hospital, wakanitunzia mali zangu, asubuhi wakaleta na chai kabisa. Ndipo wakanipa simu nikawasha nikatoa taarifa nyumbani. Nimekaa siku tatu hospital wale jamaa zangu hawajaja wala kupiga simu.

Walioniokota walinisalimu siku zote hospital mpaka nyumbani walifika kunijulia hali. Jamaa zangu nakutana nao mtaani wiki ya pili ndio daah pole sana zikawa nyingi. Ninatabasam tu.

Leo simpiti mwenye shida, kama siba uwezo wa kumsaidia nakaa mpaka atokee mwenye ana uwezo.

Dah pole sana hii ndio sababu sina rafiki na sitaki rafiki zaidi ya familia yangu
 
Nimekuwa mtu marafiki Sana ...kidogo simu mwana uko wapi ...tupo sehemu flani...fresh unatimba ... Mnapiga vitu stories nini ... Kila mmoja kwake. Mambo mengi yani kwenye magroup huko mara huyu kafiwa mchange sijui harusi...wengine birthday mradi kupigana tafu ...Nikumbushe tu nilikuwa mnywaji mnywaji haswa wa pombe lakini sio MLEVI. Basi sasa nimepumzika almost 3 months ila vijiweni naenda club naenda nakunywa zangu baltika ama Alvaro Redbull ama any energy drink .... Na nikiwa nao masela fresh tu unawazungushia kidogo ... Ila kifupi ni kwamba wamekuwa sio wana tena Kama zamani. Unona kabisa kwenye macho ... Nikiangalia matumizi niliyokuwa nafanya nao utakuta mmekaa meza watu sita saba atazungusha mmoja au wawili ila Mimi naweza kuzungusha hata mara tatu au nne kabisa peke yangu wao storiii mafegiii bia hapana. Ila siku nkasema ngoja nifanye kupumzika hata miezi 6 au mwaka kabisa nione ntakaakaaje yaaani wana Kama vile wamechukia Mimi kupumzika kunywa pombe sijasema nimeacha Bali nimepumzika Kuna malengo nimejiwekea nikikamilisha ntarudi dimbani. Simu kupigiwa yaani ni shidaaaa

Hao si marafiki
Hata ukirudi tena dimbani watch out
 
I love my friends, ninao watatu tu hivyo nawathamini sana.
 
Back
Top Bottom