brenda18
JF-Expert Member
- Sep 17, 2013
- 5,687
- 5,287
Nimepata ajali ya bodaboda.
Gari ya kwanza kufika eneo la tukio lilikuwa la wanangu. Wakaambiwa wabebeni majeruhi muwaacha hospital ya karibu, wakajibu wanawahi kwenye party. Wakaniaga kabisa.
Nilibebwa na nisio wajua, wakanifikisha hospital, wakanitunzia mali zangu, asubuhi wakaleta na chai kabisa. Ndipo wakanipa simu nikawasha nikatoa taarifa nyumbani. Nimekaa siku tatu hospital wale jamaa zangu hawajaja wala kupiga simu.
Walioniokota walinisalimu siku zote hospital mpaka nyumbani walifika kunijulia hali. Jamaa zangu nakutana nao mtaani wiki ya pili ndio daah pole sana zikawa nyingi. Ninatabasam tu.
Leo simpiti mwenye shida, kama siba uwezo wa kumsaidia nakaa mpaka atokee mwenye ana uwezo.
Dah pole sana hii ndio sababu sina rafiki na sitaki rafiki zaidi ya familia yangu