Hata kama ameondoka, issue sio kuondoka bali ameondoka vipi! Kama ameondoka kwa makubaliano, hapana ubaya wowote kwa sababu wanaweza kuendelea kushirikana! Na itakuwa poa zaidi kama anaamini anakoenda ni bora zaidi kwa career yake! Lakini kama ni kweli ameondoka lakini ameondoka kwa kiburi cha Kwangwaru (hapa ndipo taabu ilianzia-- inawezekana Diamond alikuwa anamuonea wkivu au inawezekana Harmonize akajiona yeye ndiye yeye) kuwa na Views +50M, hilo haliwezi kuwa jambo jema kwake kwa sababu ukweli ni kwamba, Sebastian hana historia ya ku-manage wasanii successfully ikiwa hata huko ku-manage kwenyewe amewahi! Asije akafanya kosa ambalo alifanya Ruby ambalo watu tuliongea sana hapa na kuhoji historia ya Majizo na EFM yake katika ku-manage wasanii ambako Ruby ndo alikuwa amejiegesha sana!!
Na hapa tukumbushane jambo moja, inawezekana kabisa kwamba Harmonize ni bonge la mkali (binafsi simkubali kwa sababu namuona ni Clone ya Diamond) kwa sasa, tena pengine kuliko msanii yeyote yule hata barani Afrika! Pamoja na yote hayo, tasnia ya muziki ni very stupid! It's not about unajua kuimba namna gani, manake kuwa mkali wa kuimba ingekuwa ndo hoja, leo hii Diamond asingekuwa hata among top 5 kwa mafanikio hata hapa Tanzania!!
Ukweli mchungu ni kwamba, kuna advantage kubwa sana ya kuwa chini ya WCB kwa sababu, kama ni uchawi, basi huyo Mchawi wa Diamond ana karama ya aina yake! Jamaa ana nyota kali sana, kiasi naweza kuthubutu kusema ana nyota kali kuliko msanii yoyote yule nchi hii!!! Leo hii WCB ikisaini msanii ambae hafahamiki kabisa, halafu kaa wiki moja kisha ita watu 1000 at random halafu waulize wakutajie wasanii walio chini ya WCB na wale walio chini ya label kama King Music!!
Wala usishangae, majority wakapatia kutaja wasanii wote walio WCB including yule aliye kundini ndani ya wiki, lakini wengi wakashindwa kutaja akina Cheed waliopo Kings Music, ingawaje wana miezi kadha hivi sasa!!! Na wala usishangae mtu akishindwa kumtaja hata Abdul Kiba, kiasi kwamba hata ukimwongoza "ina maana humfahamu hata Abdul Kiba"? Ukakuta nae anakuuliza "Abdul Kiba? Au unamaanisha Ali Kiba?"
Na ingawaje ni kweli kuna msaada mkubwa sana wa akina Talle na Sallam, lakini mbali na hao, tangia hapo tu Diamond ana nyota ya kwake peke yake, na ndio maana tangia atusue na Nenda Kamwambie, hajawahi kushuka wakati akina Tale wote hao alikutana nao takribani miaka 3 baadae! Which means, walichukua mtu ambae tayari alikuwa na nyota yake; and it doesn't matter iwe ya kuzaliwa nayo au inayotokana na ulozi!