Kwa mawazo ya wengi humu nimegundua risk taking is not our thing,Diamond asingekua na mawazo kama ya Harmonize angebaki kwa Ruge
Man, huyu Ruge watu wanampa tu credit kwa sababu tumeaminishwa Ruge ndie mastermind wa kila kitu kwenye tasnia ya muziki hapa bongo! Diamond alianza na Chifu Kiumbe, na ndie naweza kusema mwenye mchango mkubwa!! Baadae Chifu Kiumbe akaamua kuachana na masuala ya burudani na kumrudia Mungu wake!! Kuona hivyo, Diamond akaenda kwa Tale kuomba amsimamie labda kwavile alikuwa anayaona mafanikio ya Tip Top Connection! Tale kwa kuona Diamond ni mkubwa sana (kwa sababu alienda kwa Tale wakati tayari yupo juu), nae akamuomba Fella washirikiane, kwa sababu Tale mwenyewe amekiri mara kadhaa kwamba role model wake yeye ni Said Fella!!
Enzi hizo, Sallam issues zake ilikuwa ni kuleta wasanii kupiga shows Bongo, na ali-base sana Nigeria! Na kwa kipindi hicho, alikuwa anam-manage Mr. Nice lakini hawakufika mbali! Kwa kuona connection za Sallam na Nigeria, ndipo Diamond akaomba amkutanishe na Davido (kama utakumbuka, Ommy Dimpoz alishawahi kuzungumzia suala la Diamond kumletea figisu kwa Davido), na hapo ikazaliwa Number One Remix!! Lakini kwavile Sallam alishaanza kum-manage Mr. Nice na hawakufika mbali, connection yake kwa Davido ikazaa u-manager, huku Diamond akitaka kutumia fursa aliyonayo Sallam kwa Nigerians!!
So, sikatai kwamba Ruge ametoa mchango wa hapa na pale, lakini mchango mkubwa kabisa kwa Diamond umeanzia kwa Chifu Kiumbe ambae ndie alilipia albamu mzima, kisha akina Sallam, Tale, na Fella bila kumsahau Bob Junior ambae alimrekodia Nenda Kamwambie for free!!!
Diamond wakati ana-hustle, aliwahi kwenda pale THT, lakini "akatolewa nduki" kwa kigezo kwamba hajui kuimba!! Hapa tukumbushane kwamba, THT ilikuwa chini ya Ruge huyo huyo tunayeambiwa kwamba kama si yeye, Diamond asingefika pale alipo!!! Mchango wowote wa Ruge ulikuja baada ya kuwa Diamond ameshatengenezwa na kuwa mkubwa Tanzania. Inawezekana sana ukaribu wa Sallam (enzi hizo) na Clouds ndio ulifanikisha Diamond kuwa na Sallam! Lakini kama ndivyo, je lile suala la Mr. Nice na Sallam na lenyewe lililetwa na Clouds?!
Kwa historia ya THT, ni Barnaba ndie alibebwa na mbeleko ya Ruge kwa sababu na yenyewe alitolewa nduki live lakini Ruge akawaambia nafasi nyingine! Ni kutokana na hilo, ndio maana Barnaba alilia sana kwenye msimba wa Ruge!!