Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Hizo voice note Rayvanny alishaliongelea muda mrefu sana kupitia interview yake na alisema yy alikuwa upande wa Mmakonde hata mbele ya Diamond mwenyewe na ni kawaida tu ndani ofisi moja wafanyakazi kuteteana hata kama wafanyakazi ndo wamefanya makosa
Kanafiki tu Hadi kesho kanamsnitch Domo K
 
KONDE BOY ALIONDOKA NA RAMANI YA VITA WCB.
------------------------------------------------

Wakati wasafi walipomsajili baba levo asaidiane na Juma lokole kwenye mashambulizi dhidi ya Harmonize. Niligundua, Harmonize anawaumiza vichwa WCB, huenda anaonekana tishio kwao, anawakera, kuna sehemu anawakosesha usingizi na kuwanyima amani ya moyo.

Inaoekana WCB hawakutegemea kama konde angeweza kusimama kimuziki bila uwepo wa lebo ya wasafi. Na kibaya zaidi, harmonize anatumia mbinu na formation ileile wanayotumia wasafi kushinda mechi zake.

Na wasafi hawajabadili mbinu za vita hata baada ya kuvunja ndoa na Harmonize. Hivyo inakuwa rahisi Konde boy kutunishiana nao misuli. Sababu anajua uimara na udhaifu wa mbinu zao ulipo.

Muda mwingi anaotumia baba levo Instagram kurusha vijembe, mafumbo, michambo na madongo kwa Harmonize. Inakupa picha, WCB bado hawajafanikiwa kupata mbinu sahihi za kuizika career ya Harmonize kimuziki.

Wakati ndoa ya wasafi na harmonize inalala mauti. Harmonize alitozwa faini ya milion 600 kama fidia ya kuvunja mkataba. Harmonize hakuondoka kifala (WCB) aliondoka akiwa ameiba ramani ya vita.

Ramani inayompa kiburi, na jeuri ya kuwavimbia kina Babu tale, Fela, na Nasibu mwenyewe.

Na kibaya zaidi wasafi hawajabadili mbinu za vita. Kama wangekuwa wamebadili mbinu, wasingemnunua baba levo asaidiane na Jumla lokole kumshambulia Konde boy jeshi.

Vita dhidi ya WCB sio kitu rahisi. Ni vita inayohitaji mtu uwe na timu yenye msuli wa pesa, timu inayojua fitna na hila zote za muziki wa bongo fleva. Timu yenye kukusanya watu wa kutengeneza antetion na kick kila siku.

Timu yenye uwezo wa kukesha macho ikitunisha misuli inapoibuka vita ya maneno kule Instagram.

Rich mavoko aliishindwa hii vita. Na leo macho yetu yanaona kaburi la mziki wake lilivyojaa nyasi."

Harmonize anaonekana kuicheza vema vita hii. Alipoamua kuanzisha lebo yake "KONDE GANG" alikuwa anaijuza dunia kuwa ameingia kwenye vita ya muziki na lebo yoyote ile.

Alikuwa anatuma ujumbe kwamba, "amejivisha mabomu na yupo tayari kulipuka na msanii yoyote anayetaka kuuchezea ugali wake. Harmonize amefanikiwa kwenye hii vita, hivyo kujiita JESHI anastahili.

By Green Osward
 
Mmakonde ni level za zuchu,hamfikii hata marioo kwa lolote zaidi ya kujaza micheni shingoni,jana joto lote kavaa hood lazima ubongo uchemke aropoke
 

Safi kabisa wewe ni miongoni mwa free thinker, unajiuliza huyo Mond hakupewa back up?

Nongwa ni Harmo kuinuliwa na kwamba ampe heshima wakati huo huo anaetaka heshima hatoi heshima.. utopolo
 
Sasa alitegemea kuongozwa na seba ambae band zote alizoanzisha zimekufa kua atamshinda domo,mziki wako ukiwa mzuri utakua juu tu uhitaji nguvu kuwa juu
 
Huu uzi wengi wamecomment kufuatana na mahaba yao na si uhalisia na mambo. Hata kusikiliza Konde boy alichosema hawajasikiliza. Kweli mahaba yakikujaa unakua upofu
Mwambie Mmakonde mwenzako aache kulalamika na aendelee kupambana na mziki wake Coz fitna na figisu zipo kwa kila msanii hapa bongo

Na akiona ameshindwa kufanya mziki afanye kustep down tu
 
Ile "Mang'dakiwe" alipita nayo yote vilevile kaongezwa vimaneno kidogo, tayari akawa Teacher.
Halafu anasema yeye yuko juu kimziki,seba sio meneja yule anamtumia kupata pesa,heri angemchukua seven mosha kua meneja angemsaidia sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…