Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Sidhani kama wcb wanaweza kumjibu mkuu.

Hata hivo jamaa hajawasa wao tu, kawasema watu kibao nje na ndani ya wcb kua ni watu waliomkunjia sana.

Na jamaa aliemuattack sana kwenye maelezo yake ni diamond, mwanzo nilidhani labda waliomzunguka mondi ndio wabaya wake kumbe jambazi mkuu ni mondi mwenyewe😂😂. Sema mwamba alichokosea ni kutumia silaha zake zote aisee kwa sasa akae kwa kutulia tu asubiri huruma ya wananchi.
Yes..hapo ame play his last cards na hatokuwa na kitu chochote against WCB after this. Na kwa ninavyowajua wa Tz...udaku huwa wa moto ila after sometime utapoa nguvu yake.

Anawachafua his opponents while seeking public sympathy at the same time. Anasahau kuwa ni pesa na assets alizozipata akiwa WCB ndizo zilimfanya aweze kulipa asilimia kubwa ya 600M.

Hii pia inamfanya asiwe trusted na some investors ambao pengine walitaka kufanya nae some business...eg alipoanza kusema issue za kina Kusaga na Wasafi.
 
Na kwanini tusimuonee huruma yule ambaye amedhulumiwa kukifikia kipaji chake kikuu kama vile tunavyomwonea huruma kilema?
 
Siujui na siupendi muziki wa bongo fleva ila ngoja niongelee muziki wa bongo fleva.

40% ni standard ya mgawo. 60% ya management ndiyo itatumika kwenye promotion, video na audio production, gharama za safari na maladhi. Ukikokotoa utagundua mwenye 40% anabaki na pesa nyingi kumzidi wa 60%

Uzi umejaa maoni zaidi kuliko facts.
Kumbuka hiyo 40% ni nyimbo mbil8 tu kwa mwaka. Na nauli na vitu vingine vyote unalipq mwenyewe ikiwemo fines
 
Kumbuka hiyo 40% ni nyimbo mbil8 tu kwa mwaka. Na nauli na vitu vingine vyote unalipq mwenyewe ikiwemo fines
Nyimbo mbili kwa mwaka na unajigaramia vitu vingine...so na wewe ukaamini aliyosema mmakonde ni ya kweli?

Yaani mtu aliyekuja label hana kitu.....aliwezaje kujigharamia mambo mengine...?
 
Nyimbo mbili kwa mwaka na unajigaramia vitu vingine...so na wewe ukaamini aliyosema mmakonde ni ya kweli?

Yaani mtu aliyekuja label hana kitu.....aliwezaje kujigharamia mambo mengine...?
Kuna watu walishaamuaga kumchukia diamond kwa lolote km Mange. Anachotaka kusema huyo jamaa hata kwny aiyola alijilipia nauli ya south, tena kwenye ile video konde aliharibu pikipiki ya watu management ikalipa.
 
Kalipa fadhila kwa Hawa Nitalejea, kwa kumpeleka India kwa matibabu, Bob Junior na clouds fm, na baba mlezi bado kulipwa fadhira, hipo siku yao watakumbukwa kikubwa uzima tu.
Juma lokole tunajua bila mondi hupati hata pesa ya bando
 
Sasa unasema suala la kulipa 600M linatokea wapi wakati haujausoma mkataba wake? Sheria ya mikataba ndiyo inaratibu mkataba wake alipokuwa WCB.

Aliingia WCB akiwa hana kitu...kampuni ikawekeza milions of money...akakua na kuwa almost msanii wa pili kwa ukubwa nchi hii.

Anapovunja mkataba..lazima mrudi kwenye ule ule mkataba..unasemaje pale upande mmoja unapotaka kuvunja mkataba?

Yeye msanii pale kwenye label alikuwa anafanyiwa kila kitu..kazi yake ni kurekodi nyimbo na video chini ya gharama za label. Promotions zote inafanya label...

Videos na audio zote, jina lake la kisanii, account za YouTube zote ni mali ya label. So anapotoka na akataka kutumia hivyo vitu..ni lazima anunue rights ziwe zake.

So justification ya 600M inakuja baada ya kupiga hesabu za uwekezaji aliofanyiwa toka ameanza kurekodi wimbo wa kwanza. Pia gharama za kununua haki za kazi zake zote ambazo zilikuwa zinamilikiwa na label. Mwisho ni brand kama brand...aliingia kwenye label akiwa pangu pakavu sasa anatoka jina lake likiwa ni brand kubwa...lina value.

Utagundua kuwa 600M ni kama vile WCB wamemfanyia fair...hasa ukizingatia ameruhusiwa kutumia kazi zake, na social media platform kwa majina yake ya kisanii ambayo bado yanazidi kuingiza pesa. Fikiria kama angekatazwa kutumia jina lake na kazi zake...but those guys walimruhusu.

When a contract comes to an end..parties are restored to their original position as if they have never contracted at first place.

So Harmo alipoondoka..ilikuwa ni sawa kulipa gharama hizo maana the other side wali spend zaidi kwake kumkuza na kum brand...angeondoka bila kulipa ingekuwa ni unjust enrichment.

Sasa hivi anaiona hiyo 40% kuwa ilikuwa ni ndogo na alikuwa ananyonywa...wakati anaingia label alikuja na nini? He was broke na diamond took a leap of faith kwa kuwekeza kwake. Imeanza kuonekana ni ndogo once things turned out better.

Pia awe makini...asijepigwa defamation suit maana ametaja majina ya watu clearly na mambo mengi aliyosema hawezi kuyathibitisha endapo atapelekwa mahakamani......na pia kitendo cha kuvujisha mazungumzo yake na Vanny boy publicly kinaweza kuja kum haunt kama wenzake wakiamua kupita route ya jinai.

hujanielewa.

shida yangu au ya harmonize sio kulipa 600 au 800 what ever,mkataba ndio unaamua,ndio maana aliwalipa bila kushitaki au kulalamika popote,ishu ni mwenye leble kutotambua kwamba alikuwa anafanya biashara na harmonize sio hisani au charity alikuwa anafanya.

defamation suit huwa anafungua aliyeona kachafuliwa,kama kuna anayeona kaonewa aende polisi then mahakamani watakutana huko.
 
Hilo nalifahamu fika...

Tangu enzi Harmonize yupo Wasafi, nilikuwa namkubali Rayvann mara 100 kumlinganisha na Harmonize

Na kilichokuwa kinanikera zaidi kuhusu Harmonize ni ile kuiga kila kitu toka kwa Diamond.... yaani alikuwa Clone ya Diamond; hakuwa unique kama Rayvann ambae hata kama umepiga mtungi na kuzima, ukisikia ngoma mpya ya Rayvann utajua tu huyo ni Rayvann!!
Ila siku hizi ukiachana na Kick, konde amepunguza kumkopi Abdul

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Umesema tusiweke utim we mbona umeweka utim? Uyo harmonize anaimba nini tangu atoke wasafi?
Basi sema unakuja saa ngapi ama kwenu umeshakatazwa
Said kichwa nitamueka wapi na mkongo nimeshampakaza
Iyo mitungi ndo usiseme utakunywa utasaza
Kama pesa ndo zipo nyingi kuzigawa nimeshaanza

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kama wewe ni shabiki wa domo sikushangai, midomo yenu ni myepesi kutamka maovu.
Basi sema unakuja saa ngapi ama kwenu umeshakatazwa
Said kichwa nitamueka wapi na mkongo nimeshampakaza
Iyo mitungi ndo usiseme utakunywa utasaza
Kama pesa ndo zipo nyingi kuzigawa nimeshaanza

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Sioni mwenye anajadili facts humu zaidi ya utimu na mahaba. Inamaana hamjamsikia Harmo aliposema kuwa ni video shooting 9 kati ya production 59 alizofanya? Ndizo alizofanyiwa na Wasafi?
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] mkuu kweli kaimba hivii, wengine hatujasikiliza ngoma yake yoyote
nyau)
Basi sema unakuja saa ngapi ama kwenu umeshakatazwa
Said kichwa nitamueka wapi na mkongo nimeshampakaza
Iyo mitungi ndo usiseme utakunywa utasaza
Kama pesa ndo zipo nyingi kuzigawa nimeshaanza

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
1.Pesa ya kuvunja mkataba ilitolewa na sayona CRDB bank na jembe ni jembe sio kama tulivyoaminishwa kuwa sarah alihusika.

2.Diamondi ni mtu mwenye roho mbaya sana rejea kauli za ommy dimpoz, belle 9, shettah rich mavoko.

3.Rayvanny anavumilia kuwa wasafi hajui pa kuanzia kutoka tena kwa yeye wanaweza sema atoe bilion 1.

4.Bila amri ya Magufuli Diamond asingesaini kuvunja mkataba kwa wakati.

5.Harmonize mwaka wa 3 anaendelea kuwepo kwa game nje ya wasafi.

6.Kuna watu huwa wanalazimishwa kumsifia na kumpost Diamond kila kukicha ama akiwa na jambo mfano jana amepostiwa na mama yake uncle shamte baba levo page ya wasafi.

7.Nyimbo zote nzuri za WCM Mondi alikuwa analazimisha aweke mistari yake ili ikitoka ionekane yeye ndio ameibeba nyimbo wakati kiukweli sio sahihi alikuwa hataki kupotea masikioni kwa watu.

8.Uchawi ni sehemu ya maisha ya Diamond.

9.Mameneja na ndugu wa Diamond walichangia ugomvi kuwa mkubwa sana.

10. Mali tunazoaminishwa za Diamond zingine hazina ukweli.
Basi sema unakuja saa ngapi ama kwenu umeshakatazwa
Said kichwa nitamueka wapi na mkongo nimeshampakaza
Iyo mitungi ndo usiseme utakunywa utasaza
Kama pesa ndo zipo nyingi kuzigawa nimeshaanza

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Mambo yanakwenda kasi sana, joto linazidi kukimbiza huku jua likichoma kishenzi. Wakati tukifikiria ni kwa namna gani tunaweza kusurvive huku maji na umeme vikiwa shida, wasanii nao wanaibuka na mambo yao, yaani ni shida juu ya shida.

Haya! Wengi mmeniambia nije na makala kuhusu jambo hilo, basi niseme ninakuja na hii makala, ila kabla ya kuendelea, weka uteam pembeni kwanza, tuzungumzie mambo halisi.

Mimi sina timu, huwa ninazungumza kitu ambacho ni cha kweli, kile kilichokuwa kwenye mtazamo wangu, kubwa zaidi, huwa si mpenzi wa miziki ya Bongo fleva, hata simu yangu, huwezi kukuta ngoma za hapa Bongo.

Lakini kwenye yote, acha nijaribu kuelezea kile nilichokiona tangu siku ya kwanza Harmonize anapoondoka WCB mpaka leo, nitajaribu kufafanua ninayoyaona, kama una yako, basi na wewe kaandae makala tuje kusoma.

MKATABA WA 40%
Nianze na suala la mkataba. Kwanza kitu cha kwanza tujue unapokuwa huna pesa, una maisha magumu, ukiletewa mkataba wowote ule ambao unaonyesha utakuwa unaingiza pesa ni lazima utausaini kwa sababu usipousaini, inamaanisha unakubaliana na maisha ya dhiki unayoishi.

Leo nikisema ninahitaji waigizaji kwenye filamu yangu, halafu nikisema bwana mimi sina hela ya kumlipa msanii, ila ukifanya kazi na mimi, utapata jina na kuitwa kwenye muvi za watu wengine, utaacha nafasi hiyo kwa sababu hutolipwa? Je, utaendelea kukaa kwenye maisha hayo na kuachana na opportunity ambayo itakufanya kujulikana?

Kwenye hili! Kwanza tusimlaumu Harmonize kwamba kwa nini amesaini mkataba wa kulipwa asilimia 40 kwa sababu naamini hata ungekuwa wewe, kwa maisha ya dhiki, halafu unajua nikifanya kazi na Mondi, nitajulikana na kutengeneza pesa, kwa nini usikubali?

Kampuni nyingi za Tanzania zina mikataba mibovu na tunaiingia kwa sababu tuna shida ya pesa, tupo kwenye maisha ya kimasikini sana, unakubali kusaini mikataba mibovu kwa sababu unataka pesa, ama umaarufu ili baadaye utusue.

Unapoingia kwenye mikataba hiyo, unaona kabisa unanyonywa, ila huna ujanja, kuna kitu unakitafuta lakini moyo wako unasema siku moja nitaondoka tu, nikishapata pesa za kutosha nasepa.

Hilo ndilo wamekuwa wakilisema hata wajasiriamali, unapotaka kuanzisha biashara yako, kwanza anza kuajiriwa, upate pesa kisha ondoka ukaanzishe biashara yako, ndivyo ilivyokuwa kwa Harmonize.

Asingeweza kukaa WCB milele, ilikuwa ni lazima siku moja aondoke. Ukishapata pesa na umaarufu uliokuwa unautaka, sasa unasema huu ndiyo muda wa kuondoka, unaondoka zako, kuna watu wengi wamefanya hivyo, yeye si wa kwanza.

Kosa kubwa wanalofanya WCB ni aina ya mikataba wanayoingia na wasanii, msanii akiondoka, akilipia pesa, imekula kwao ila si kama lebo nyingi za Marekani.

Leo hii Drake, Nicki Minaj hawapo Young Money, ila kwenye kila pesa wanayotengeneza huko walipo, kuna asilimia inaingia kwenye lebo hiyo na maisha yanasonga.

Suala la Harmonize kuingia mkataba wa aina hiyo, simlaumu kwa sababu hata wewe unayesoma hapa, huko kazini kwako umeingia mkataba wa aina hii hii, hujilaumu wewe, unamlaumu Harmonize.

Kijana wa Kitanzania anapotaka kutafuta jina ama pesa, anakuwa tayari kufanya jambo lolote lile. Nilipokea meseji nyingi tu, mtu anakwambia “Bro! Natamani kuigiza, nitaigiza hata bure.”

Unajua anamaanisha nini? Anachohitaji ni kutafuta jina, anaamini hapo baadaye atakuja kuwa na jina na atapiga pesa tu kwani akihitaji pesa sasa hivi, anaweza asizipate na ukawa mwisho wa ndoto zake.

Sasa mtu huyu akikubali kuigiza bure ama kwa malipo madogo, siku akipata jina na kutaka kuondoka, cha kwanza tutatakiwa kupitia mkataba wake, tufanye tulichokubaliana na tuache aondoke.

Maisha popote pale.

HARMONIZE VIJEMBE KWA MONDI
Harmonize aliondoka WCB na kilichofuata ni kutoa vijembe na matatizo yaliyokuwepo hapo. Kuna wengi walisema kwa nini asingesema akiwa hapo? Kama wewe unajiuliza swali hilo, jishike kifuani na sema mimi ni mjinga sana.

Kuna wachezaji wengi wa mpira wakiwa timu fulani, hawazungumzi mbovu, ila wakiondoka ndipo utasikia ile timu mbaya sana, kocha magumashi na mengine mengi.

Ukiwa kwenye nyumba mbaya, husemi kwa watu kwamba ni mbaya, utataka uondoke halafu ndiyo useme ilikuwa nyumba mbaya.

Leo umeoa, huwaambii watu kama mkeo ni malaya, unasubiri umuache ndiyo uanze kusema yule mwanamke alikuwa malaya, halafu hajui kupika, kikojozi na kitandani gogo. Kwa nini usiseme wakati akiwa ndani?

Madhaifu ya sehemu tunayasema tukishaondoka sehemu hiyo.

Suala la Harminize kumpiga vijembe Mondi ni kawaida kila kona. Bado ana hasira, labda kwa yale aliyowahi kutendewa ambayo aliona hayafai, taswira ikimjia, anakuwa na hasira na kujikuta ameropoka hili na lile.

Mtu akiondoka sehemu kwa vita, atahitaji kukaa muda mrefu mpaka akili yake kuja kukaa sawa.

HARMONIZE AMEKOSEA?
Jibu ni ndiyo! Wakati mwingine unapoondoka sehemu, achana na kila kitu, nenda kafanye mambo yako, achana na yaliyopita. Harmonize alishindwa kufanya mambo yake.

Alimkalia Diamond kooni, akaikalia WCB kooni, akawa anatoa vijembe kutwa. Nikahisi labda naye Diamond kwa kuwa amekuwa mkongwe angekaa kimya, ila cha ajabu naye akaanza kumrushia vijembe hasa kwenye nyimbo ambazo alishirikishwa, nikajua wote bado ni watoto ama kila mtu hataki kuonekana mpole kwa mwenzake.

MONDI AMEKOSEA?
Kuna msemo wa Kitanzania unasema ukigombana na mtu mmoja halafu ukasema ana matatizo, basi tunaweza kuamini kwamba kweli ana matatizo, ila ukigombana na watu watano, tutashindwa kukuelewa ukisema wana matatizo, tutakwambia kwamba wewe ndiye una matatizo.

Leo ukiniambia Mondi ana matatizo, nitakataa hilo, yeye hana matatizo bali watu waliomzunguka ndiyo wana matatizo. Namfahamu msela, nimekua naye mtaa mmoja, tangu kishuleshule mpaka alipoanza muziki japo sisi wengine tulikuwa bize na shule.

Jamaa ana uswahili kama sisi ila kuhusu roho mbaya, kwa mchizi hilo nakataa kwa kuwa tabia ni kama ngozi, huwa haijifichi, ningeliona hilo tangu kipindi kile alipokuwa akitoroka shule na kwenda kuimbaimba kila alipoona muziki ama kutafuta hela kwa kuuza nguo kwa kudandia Tandale sokoni.

Unapokuwa unakutana na watu ambao wanaweza kuibadilisha akili yako na kukupa nyingine kabisa. Ukiwapa nafasi, wanachukua maamuzi yao mabovu na kuwa yako, na wanafanya lolote lile ambalo mwisho wa siku litaonyesha taswira mbaya juu yako.

Kama ulifuatilia mwanzoni, vijembe vingi vya Harmonize havikuwa kwa Mondi moja kwa moja, alijua kabisa mchizi alikuwa mtu poa ila kuna mtu ambaye hakuwa poa, na ndiye aliyekuwa akimpiga vita sana.

Na ninadhani baada ya kuonekana hajibu kitu, ni kama akashinikizwa kujibu, naye ndipo alipoanza kujibu.

Kosa la Diamond ni kuanza kujibizana na Harmonize. Angekaa kimya tu, mtu umekwishamtoa, umemfanya kujulikana kupitia wewe, ana kitu gani cha kujimwambafai kwako? Wewe nyamaza tu, dunia itaendelea kujua kwamba bila wewe, yeye asingekuwepo hapo alipokuwa.

Kumjibu Harmonize ni jambo baya sana ambalo Diamond amelifanya, alitakiwa kuwa kimya tu, aendelee kufanya mishe zake kama kawaida kwa sababu siku zote huwezi kumfananisha yeye na Harmonize, bado ni kijana mdogo sana kwenye mafanikio ya muziki.

Kinyago umekichonga mwenyewe, kinakutishaje? Unakiogopea nini? Kama ningekuwa Mondi, nisingemjibu Harmonize ama kumpa kijembe kwenye wimbo wowote ule, ningewakataza Juma Lokole na Baba Levo kumuongelea Harmonize, yaani ningeachana naye mazima. Kumuongelea na kumtupia vijembe inaonyesha kabisa naye Mondi anatamani kusikika mitandaoni akibishana na Harmonize ambaye kiukweli ni mdogo mno kwake.

NI KWELI HARMONIZE AMEBADILIKA?
Bado najiuliza swali hilo. Nakumbuka kipindi cha nyuma wakati akiwa WCB, wakati huo nikiwa mwandishi wa habari. Hakuna kitu ambacho Harmonize anakikataa kama kumuona mtu akipiga picha na Diamond. Yaani alikuwa anakukazia ileile.

Harmonize alikuwa maana halisi ya mringaji, alijua kufanya kitu chochote kile usimfikie Diamond kwa lolote lile, hata ukiwa shabiki wake kwa namna gani, ila leo namuona si Harmonize yule, amekuwa mnyenyekevu, mpole na amekuwa na moyo wa kusaidia wengine, huwa ninajiuliza kutoka WCB kumembadilisha kuwa hivyo ama kule aliambiwa awe na maisha yale hata kuwabania watu kupiga picha na Mondi? Sijapata jibu.

KOVU LA HARMONIZE LITAMTESA MONDI MILELE
Harmonize alikuwa msanii wa Mondi, yaani yeye ndiye ambaye alimchukua yeye kama yeye, si kama hao wengine ambao ameletewa. Harmonize alikuwa kipenzi cha Mondi, aliaminiwa na kuonyeshwa chocho zote.

Kipindi kile Mondi alipokuwa akisafiri, alikuwa akiongozana na Harmonize kila kona, alimtambulisha kwa kila mtu, kwa kifupi alimwamini kwa kuwa alikuwa msanii wake, hakuletewa kama ilivyokuwa kwa hao wengine.

Ukiangalia kipindi hicho, Mondi alikuwa akisafiri sana na Harmonize kuliko hata Rayvanny, alijua kwamba huyu ni msanii wangu mimi, mrithi wangu, halafu ghafla tu, huyo mrithi akasepa zake. Kama ni kupigwa na kitu kizito kichwani, basi Harmonize amejua kumpiga nacho Mondi.

Suala la Harmonize litaendelea kumtesa, kama ni mzimu wake basi utaendelea kumtokea. Rich Mavoko ameondoka WCB lakini humsikii Mondi akimzungumzia, wengine watakuja na kuondoka, hatowazungumzia, ila kwa Harmonize, hatoweza kujishika hata kidogo.

Alitumia pesa na muda kwa ajili yake, alimwamini, akampa kila kitu ili dogo atusuea, kipindi kile akampa mpaka mademu wa kupiga nao skendo, mara katoka na Wolper, mara na huyu, yaani yote ilikuwa ni kumtengenezea jina dogo ili afuatiliwe, mwisho wa siku kilichotokea, kimemuumiza mno mno mno.

HIVI MMEMFIKIRIA RAYVANNY YUPO KWENYE HALI GANI?
Huyu amesahaulika. Jana baada ya kusikia mahojiano ya Harmonize na kuplay ile voice record, nikaanza kumfikiria Rayvanny yupo kwenye hali gani. Kuna jamaa mmoja mpenzi wa WCB aliweka video zikimuonyesha Rayvanny akiwa kwenye mahojiano kipindi cha nyuma akisema alihisi anarekodiwa na Harmonize, nikamuuliza jamaa maswali kadhaa.

Mtu ameondoka WCB kwa ugomvi mzito, leo anaongea na wewe, unajua kabisa unarekodiwa, je, ungeweza kumtemea shit bosi wako? Yaani mimi nimeondoka kwa ugomvi, halafu unaongea na mimi, unajua kabisa nakurekodi, je, ungeongea shit kwa bosi? Jibu ni hapana.

Rayvanny hakuwa akijua hilo ila baadaye akasanuka kwamba inawezekana yale mazungumzo yake na Harmonize yalikuwa yakirekodiwa, akaamua kujitetea mapema kabisa ili siku yatakapokuja kuwekwa hadharani basi tuseme jamaa alijua kama alikuwa akirekodiwa. Wakati mwingine inahitaji akili kubwa kucheza michezo ya kijanja.

CHUKI, HOFU VIMETAWALA BONGO
Kitu ambacho nakataa na nitaendelea kukataa ni pale mtu akiniambia kuna siku muziki wetu utasikika duniani kama ulivyo muziki wa Nigeria, hicho kitu sahau bro!

Sisi tumejaza chuki mioyoni mwetu, Watanzania hatupendani, unaweza kuzungumza na mtu vizuri, kumbe anakuchukia na hujui, anaziba baraka zako na hujui kabisa.

Wanamuziki wanachukiana wao kwa wao, mbaya zaidi kwa sasa wapo kimakundi, yaani kuna Team Mondi, Team Harmonize na Team Kiba, kwa staili hiyo tutafika vipi huko mbele? Hatuwezi.

Leo tutawaona wasanii wakigombea tuzo, bila aibu, nampigia kura msanii wa nje na kumuacha wa ndani, hiki ni kitu ambacho Wanigeria hawakifanyi, wanapoamua kusapotiana, wanasapotiana kwa asilimia mia moja.

Leo Burna Boy anakwenda Marekani kuperform, anawachukua maunderground wake anapaa nao kwenda huko, anawatambulisha jukwaani na ngoma zao zinapigwa, na hata kuperform, wanatangazana tu baadate tunasema huyu Burna Boy na Mondi, Mondi mkongwe, ila leo ukiuliza nani mwanamuziki mkubwa, utasema Burna ni mkubwa mara kumi ya Mondi.

Hatuwezi kufika mbele bila kusapotiana. Kwa kitendo cha Mondi kwenda Marekani bila kuwa na msanii yeyote yule ni kosa, analeta ubinafsi lakini simlaumu sana kwa kuwa yamekwishamtokea puani kwa Harmonize, alimuonyesha njia mwisho wa siku akaachwa kwenye mataa, wakati mwingine bora uonekane mbinafsi kuliko mjinga.

Kwa maelezo ya Harmo kipindi cha nyuma alisema kwamba ukienda Nigeria, ni vigumu sana kusikia klabu wakipiga ngoma za Tanzania, ila cha ajabu, sisi tunaongoza kupiga ngoma zao.

Niwaambie tu, ili muziki wetu ufike mbali, tusubiri hizi zama za Mondi, Kiba na Harmonize zipite, waje wengine wenye kiu ya kuwainua wengine kimataifa, kidogo tutaweza kusogea.

JPM ALIWEKEWA WAKATI MGUMU
Hayati JPM alikuwa kwenye wakati mgumu sana. Mondi na Harmonize walikuwa vijana wake, aliwapenda na kuwapamba wote wawili, mwisho wa siku akapokea simu kutoka kwa Harmonize na kuombwa msaada wa kitu ambacho Mondi hakuwa akikitaka bila shaka.

Kama mzazi, lazima utakuwa na wakati mgumu, hapo ni lazima umfurahishe mmoja na kumliza mmoja, ila alichokiangalia na kukifanya, ni hekima kama mtu mzima, simu yake moja kwa Waziri Mwakyembe ikamuweka Harmonize huru. Pongezi sana kwake kwa hekima zake.

Kuna kila sababu ya Harmonize kulia sana msibani mpaka kuchora tattoo ya Hayati JPM. Alimfanyia mambo mazuri likiwemo hilo, na kwa kile alichomfanyia, tattoo hiyo haitakiwi kufutwa mwilini mwake mpaka kifo chake. Bila yeye, inawezekana asingekuwa huru mpaka leo.

NB: Kweli Konde Jeshi, yaani amekaa na haya yote kwa miaka mitatu na wakati Manara alishindwa kukaa nayo hata kwa wiki moja tu.
Basi sema unakuja saa ngapi ama kwenu umeshakatazwa
Said kichwa nitamueka wapi na mkongo nimeshampakaza
Iyo mitungi ndo usiseme utakunywa utasaza
Kama pesa ndo zipo nyingi kuzigawa nimeshaanza

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom