Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Hakuna shughuli hapo

Harmonize inabidi atoe respect kwa mtu aliyemuokota baada ya kuambiwa na BSS kuwa hajui kuimba ila Diamond akaamini kipaji chake na kumsaidia kufika alipofika leo hii

Huyo rayvanny mwenyewe alikuwa ameachwa na Madee kwenye ile label yao kwa kuambiwa hajui kitu ila Simba akamchukua na kuamini kipaji chake na leo hii yupo juu

Muangalie Mbosso khan leo hii wenzake wa kundi la Ya moto band wapo wapi na wanafanya nini kwenye industry? Aslay na yule Beka flavour

Tuje tumsuguse Zuchu right now, one of the top female artist in East and Central Africa

Ooooh!, This Dude Simba need appreciation kwa kutengeneza wasanii wakubwa ambao wanaweza kufanya competition na yy mwenyewe coz label nyingi hapa bongo wameshindwa kufanya ambacho amekifanya yy

Pia wakumbuke ile music label yake sio kwa ajili ya social charity Ila ipo for profit gain
yaani usikute kwa sababu hizi umeolewa na mwanaume mwenzio mahali, unakata vitunguu
 
Wabongo bhna naona mshakua brainwashed na Wasafi classic ni kawaida mtu alikua anatakiwa ajitengemee shida kujaribu kumshusha anapojaribu kujitegemea

Harmonize naona ameongea maeneno general sana ya tabia za ma boss wa ki Tanzania ukiachana na mtu muache endelee na maisha yake usijaribu kumuua ili aonekane alifanya mistake kutoka kwako acheni ushabiki wa kishamba sukumeni mziki uende sio unafiki
Hii komenti irudiwe mara kumi.
 
Sina timu ila nimeangalia mahojiano ya konde ana hoja ya msingi yeye amekubali kwamba D amemfanyia wema ila anachopinga D kuendelea kumuwekea vikwanzo hata kama mtu umemsaidia akishindwa kukupa shukrani ndio umtengeze zengwe la Fitina hii si sawa.
Nimemsikiliza tena Harmo sasa hivi tena kwa utulivu maana jana nilikuwa kwenye makelele!

Asee nimefuta mpaka comment yangu[emoji849][emoji849]

Domo hafai
 
Kuna kipande namsikia harmonize anasema kuwa wasafi festival mtwara huko .harmo alikuwa aimbe na mond nyimbo ya mwisho ila mond kuona shangwe kubwa hakupanda nae .wakati harmonize anashuka mkubwa fella anasema unaonaaaaa dogo atakuua huyu.!!!! Akimaanisha kuwa mond atafunikwa na harmonize au atarogwa awe chini ya Harmonize.

Mimi sio shabiki wa mziki ila hichi alichosingiziwa mmakonde kipo sana sehemu yenye riziki .pia wazee wa wcb walikuwa wakisema harmo aliwaambia mashabiki kwa kilugha kuwa wasimshangilie mond kwenye jukwaaa.mmakonde kapitia mengi.ndio maana katoka wcb kanenepa faster.
 
Sakata looteee la harmo kutoka wcb ndilo lilomzima rayvanny. Jamaa alikua anakuja juu sana ila siku hizi kapoa mno hata label yake inasua sua angeweza mae kujitoa itakua kaona yanayompata mwenzie,kaamua kujituliza hapo hapo
 
Sijasikiliza hata nyimbo zake....ndo kile kiingereza cha ago kill u??? Akankill ma self???

Sema nn hata mm albam yake inanipa ugum sana kusikiliza hivyo viingereza hapana aisee pia inaonekana hashauliki ilipaswa akae kimya tu huko mbelen tungemjua tu nan mbaya
 
Hizi zote ni kiki tu, hawa wote wanajuana na wanajua wanachofanya...
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Sema nn hata mm albam yake inanipa ugum sana kusikiliza hivyo viingereza hapana aisee pia inaonekana hashauliki ilipaswa akae kimya tu huko mbelen tungemjua tu nan mbaya
Mbeleni lini? Kijana amezungumza ukweli, kijana ana moyo hatari, ingekuwa mtu mwingine hiyo vita isingekuwa ya nchi hii, kimsingi
Tale
Mkubwa Fela
Salama
Diamond
Hawa watu ni kama wale wachungaji wanaotumia dini kumbe ni wafiraji tu, anyway if could be nimelipa 600ml wasingenichelewesha contract even a single minute..Niichojifunza huyu kijana alikuwa anafanya mambo mengi bila lawyer wa upande wake,
 
Mdogo wangu mimi ninaongea kitu ambacho nina ufahamu nacho, sasa kama mziki ni vita jamaa karusha kombora limewapata ugulieni kimya kimya, wasubirie mengine yanakuja mpaka tumalize huu mwaka huyo junk wenu anaweza kuwa korokoroni

Unamyonya mtu kisha unamchuna 600M, that's hard young bro..
Wewe hauna uelewa wowote nimegundua una ushabiki wa kijinga, nimekupuuza ulivyosema korokoroni na unyonyaji.

Unavyojiunga na kampuni yoyote unepewa mkataba Kisha unasoma matakwa yake, label ya WCB inamilikiwa na kampuni ya Wasafi limited ambayo diamond CEO kwa hiyo kama umekubali kufanya kazi maana yake uko tayari kufauata matakwa ya mkataba wako wa kazi. Unyonyaji unatoka wapi acha kuwa mjinga harmonaize alikuwa muajiriwa kwa hiyo kuchukua 40 ya 100 sio hiyo nyingine ni kwa ajiri kuendesha kampuni.

Acha urofa basi mwanangu usiegemee upande mmoja
 
Wewe hauna uelewa wowote nimegundua una ushabiki wa kijinga, nimekupuuza ulivyosema korokoroni na unyonyaji. Unavyojiunga na kampuni yoyote unepewa mkataba Kisha unasoma matakwa yake, label ya WCB inamilikiwa na kampuni ya Wasafi limited ambayo diamond CEO kwa hiyo kama umekubali kufanya kazi maana yake uko tayari kufauata matakwa ya mkataba wako wa kazi. Unyonyaji unatoka wapi acha kuwa mjinga harmonaize alikuwa muajiriwa kwa hiyo kuchukua 40 ya 100 sio hiyo nyingine ni kwa ajiri kuendesha kampuni. Acha urofa basi mwanangu usiegemee upande mmoja
Umesikiliza hiyo interview ya Harmonize ??

Hiki kizazi kwanini kina vijana mataahira sana ???!!
 
Umesikiliza hiyo interview ya Harmonize ??

Hiki kizazi kwanini kina vijana mataahira sana ???!!
Acha kujitapa mjuaji kumbe fala tu, una welevu gani kuita wenzako matahira wakati akili yako hainonekani iko wapi, unazidi wengine nini? Mimi nimeangalia na kusukiliza kila kitu wala simpi credit yote aliongea fitina, husda na roho mbaya ya diamond ni vitu vya kawaida na ndio hulka za kibinadamu.


Ila hoja yangu ipo kwenye approach anayotumia kurudisha mashambulizi na yeye kulialia kuhusu kulipa deni kama fidia ya uwekezaji uliomfanya kuwa biashara
 
Huyu mziki ushamshinda,album inafanya vibaya.

Sasa Diamond kama angetaka kila siku kuwa yy.

Kaanzisha lebo ambayo imemtoa yy.
Kampeleka nje kufanya video kubwa.
Kamkutanisha na wasanii wakubwa Africa.
Kamtoa Rayvanny mpaka kufikia hatua ya Colabo na Maluma na kuchukua BET,Tz hii Rayvanny ndiye mwenye nyimbo yenye streams nyingi, kapiga show jukwaa la essence, mafanikio ambayo Diamond hajawahi kuya fikia.

Angeamua kuto kuanzisha label tusinge mjua na Diamond ni mfanyabiashara, always ana angalia faida na label zote duniani zina angalia faida, hata yy na JembeniJembe wanaangalia faida.

Yeye mwenyewe kuimba aliambiwa hajui, Diamond kakaa nae zaidi ya miaka mitatu, akimfundisha na kumpika kimuziki na kuna watu walimwambia hajui kuimba ila Mondi hakukata nae tamaa, kula,kuvaa na kulala kwa Diamond.

Anadai WCB walikuwa wana muogopa yy, haya leo zaidi ya miaka miwili nje ya WCB, yupo yy peke yake,free habanwi je kafika wapi,kampita Diamond?Anapata airtime ktk media zote kubwa zilizo kuwa hazipigi nyimbo zake.

Halafu haja tuambia wasanii wake wanapata kiasi gani, mikataba yao miaka mingapi,wana miaka miwili hawa heleweki wanafanya nini.
team domo mmeanza kazi
 
Diamond alimchukua Harmonize akaishi nae nyumbani kwake,
Alienda kushoot nyimbo yake AIYOLA South Africa kwa hela za WCB,
Diamond akafanya kolabo nae free kabisaa ya BADO akaenda kimataifa,
malazi alilipiwa na WCB,
Leo anasema alikuwa ananyonywa alitaka zile gharama zirudije?
kati ya nyimbo 59 za konde ni nyimbo tisa tuu wasafi ndo walitoa gharama zao
 
Nimesikiliza intavyuu yote kwa umakini kabisa ila nlichogundua ni kuwa "MFA MAJI HACHOKI KUTAPATAPA"
Watu wamehadaika na hii interview sehemu ndogo sana kuwa "hakuna mtu anayeweza kujichafua mwenyewe wakati wa kujitetea"

Harmo kashindwa kumove on kabisa... Lebo yake inasustain kwa vile imeelekeza nguvu kubwa mashambulizi kwa wasafi

Kama anapigwa matukio ni vile naye kila kukicha haishi kuelekeza mipasho kwa wasafi. Hamna anayependa kuchafuliwa
 
Swala la Harmonize kujilinganisha na Mond iwe kwa pesa&investment, mafanikio kimziki, fanbase, Exposure na mambo mengine ni ujinga usio na kikomo, ambao umetamalaki kwake mpaka kwa mashabiki zake maana ukweli unafahamika kuwa hafiki hâta 50% ya Mond kwa chochote kile.

Kimziki ameshafeli, hakuna hâta ngoma yake ambayo imeenda mbali tangu atoke WCB, tofauti na KWANGWARU ambayo ilibebwa na uwepo wa huyo anaemtukana leo, ni ngoma gani nyingine kubwa aliyowahi kufanya??
kwenye interview sijaona akijilinganisha na mondi zaidi kasema yeye kwa mondi bado mdogo.

alikuwa anaeleza jinsi alivyofanyiwa fitna hadi akaamua kuondoka wcb
 
Back
Top Bottom