Harmonize umeyakanyaga kwa Mbosso, unaenda kupigwa kama ngoma!

Harmonize umeyakanyaga kwa Mbosso, unaenda kupigwa kama ngoma!

Kiukweli mbali na muziki, sijaelewa hata kimoja ulichoandika hapa. Hayo mengine ya msanii huwa sina muda wa kuyafuatilia kabisa.

same as myself
Machawa wa konde gang , lazima mjifanye hamuelewi , nyimbo mnazosema Kali Ila bado zinalag behind , ni kama kujitekenye na kucheka wenyewe .... !! Ushuhuda wa kujishuhudia mwenyewe
 
TheStoryTimeFacts [emoji310]
Habari [emoji112]
Naitwa Erry Mars ni msimuliaji wa Historia,makala na simulizi
Nathamini sana mchango wako ndugu [emoji120],Naomba support yako nisaidie ku SUBSCRIBE na kugusa KENGELE kwenye channel yangu.[emoji120]
Link Bonyeza Hapa[emoji116]

Asante sana [emoji120]

Mtafute UMUGHAKA akusaidie
 
Huyu Mbosso kwa mashairi yake utadhani anaimba taarabu. Harmonize lile jamaa linajua mziki
Mbosso yan simuelew hata anaimba nini, nikajua ni mimi peke yangu.

Harmo anaujua muziki, nyingine zinazobakia ni chuki tu.

Mbosso inabidi abadilike sana kama anataka kufika mbali, ila hii stail ya kutaja misosi hapana aisee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waswahili wanasema mwanakulitafuta mwanakulipata.

Baada ya kusikia kwamba Mbosso anaachia EP yake siku ya Ijumaa tarehe 28, October. Basi kama kawaida mzee wa kuvizia upepo ili abaki kuwa relevant Harmonize naye akaitangaza siku hiyo kuwa atatoa album na yeye.

Sasa ni wazi ameyakanyaga, mnyoosho atakaopewa na Mbosso hatokaa asahau. Mbosso anaenda kumnyoosha haswa na akibuma atarudi kwa wajinga wenzie kuilaumu WCB kama kisingizio.
Hivi mnaifahamu biashara ya muziki kweli au mnaleta ushabiki maandazi tu humu? Pesa za Ziiki inabidi zirudi kwa hiyo lazima watoe ngoma la sivyo mikataba itawabana mno.

Harmonize alipewa 1.1 billion kusaini Ziiki na WCB wasafi walipewa $5 million. Kwa hiyo inabidi pesa za watu zirudi.
 
Wewe huwezi nifundisha mimi biashara ya muziki, acha tu niishie hapo.
 
Watu hawako serious, Hamna nyimbo mule ya kufananisha na Album ya Harmo labda aloimba na mondi na ndo imebeba hyo EP yao eti kuna nyimbo kaimba na Muarabu[emoji23][emoji23][emoji23] alimradi vituko tu

Nyimbo 6 vs nyimbo 14 haya ndio matokeo mpaka sasa huko audiomack

IMG_20221101_124530.jpg
 
Waswahili wanasema mwanakulitafuta mwanakulipata.

Baada ya kusikia kwamba Mbosso anaachia EP yake siku ya Ijumaa tarehe 28, October. Basi kama kawaida mzee wa kuvizia upepo ili abaki kuwa relevant Harmonize naye akaitangaza siku hiyo kuwa atatoa album na yeye.

Sasa ni wazi ameyakanyaga, mnyoosho atakaopewa na Mbosso hatokaa asahau. Mbosso anaenda kumnyoosha haswa na akibuma atarudi kwa wajinga wenzie kuilaumu WCB kama kisingizio.
Umeloa tayari😅
 
Tumia akili za kuzaliwa usipende kufuata mkumbo kwa hiyo hapo ndo unaonesha ubora wa album, Kati ya Nyimbo 14 mpya ni ngapi? Huyo mbosso mtoto mdogo sana yaani WCB team nzima wamekaa kutunga hiyo + Promo lakini hawawezi kufikia hyo album Ep kama hufahamu halafu Jeshi one man army katoa album mwenyewe give him respect.

Huyu mnahangaika tu kumjibu,mwenzenu yuko kwenye assignement,jioni anapeleka ushahidi jinsi alicyokuwa anapambana mtandaoni kutetea brand analipwa elfu 8 anasepa.
 
[emoji23][emoji23][emoji23],Duuh hapo nimeelewa huyu kumbe ni chawa, yeye kazi yake kusifu huku na kuponda kule.
Anacho fanya yeye na unachofanya wewe ni yaleyale sema mko pande mbili tofauti, toa kwanza boriti kwenye jicho lako ndiyo utaona kibanzi kwenye jicho la mwenzako.
 
tupo tofauti kabisa ndiyo maana kwanza nilianza kusikiliza nyimbo zote za mbosso na then nkasikiliza nyimbo za harmo, na sikusema nyimbo za mbossi ni mbaya ila huwezi mvunjia heshima harmo kwa sababu ya mbosso, ukweli usemwe Album ya hamo ni kali kuliko EP ya mbosso. kama na wewe ni chawa sawa ila kama ni shabiki wa muziki utakuwa umenielewa.
Mwizi humuhisi kila mtu anaiba, mimi sijazungumzia muziki bali nimezungumzia comments zenu umeshaanza kuniita chawa, je ninge-comment kuwa nimezikubali zaidi nyimbo za Mbosso ungeeniitaje?

Diamond ndiye mtu anayeongoza kwa fan-base Tanzania lakini kuna wengi tu wanaona wanamuziki wengine wanaimba vizuri zaidi yake vivyo hivyo hata nyimbo za Harmonize na Mbosso watu watatofautiana mitazamo.
Kulazimisha kila mtu awe na mtazamo wako nadhani huo tuuite uchawa.
 
Back
Top Bottom