Harmonize umeyakanyaga kwa Mbosso, unaenda kupigwa kama ngoma!

Kiukweli mbali na muziki, sijaelewa hata kimoja ulichoandika hapa. Hayo mengine ya msanii huwa sina muda wa kuyafuatilia kabisa.

same as myself
Machawa wa konde gang , lazima mjifanye hamuelewi , nyimbo mnazosema Kali Ila bado zinalag behind , ni kama kujitekenye na kucheka wenyewe .... !! Ushuhuda wa kujishuhudia mwenyewe
 
Mtafute UMUGHAKA akusaidie
 
Huyu Mbosso kwa mashairi yake utadhani anaimba taarabu. Harmonize lile jamaa linajua mziki
Mbosso yan simuelew hata anaimba nini, nikajua ni mimi peke yangu.

Harmo anaujua muziki, nyingine zinazobakia ni chuki tu.

Mbosso inabidi abadilike sana kama anataka kufika mbali, ila hii stail ya kutaja misosi hapana aisee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mnaifahamu biashara ya muziki kweli au mnaleta ushabiki maandazi tu humu? Pesa za Ziiki inabidi zirudi kwa hiyo lazima watoe ngoma la sivyo mikataba itawabana mno.

Harmonize alipewa 1.1 billion kusaini Ziiki na WCB wasafi walipewa $5 million. Kwa hiyo inabidi pesa za watu zirudi.
 
Wewe huwezi nifundisha mimi biashara ya muziki, acha tu niishie hapo.
 
Watu hawako serious, Hamna nyimbo mule ya kufananisha na Album ya Harmo labda aloimba na mondi na ndo imebeba hyo EP yao eti kuna nyimbo kaimba na Muarabu[emoji23][emoji23][emoji23] alimradi vituko tu

Nyimbo 6 vs nyimbo 14 haya ndio matokeo mpaka sasa huko audiomack

 
Umeloa tayari😅
 

Huyu mnahangaika tu kumjibu,mwenzenu yuko kwenye assignement,jioni anapeleka ushahidi jinsi alicyokuwa anapambana mtandaoni kutetea brand analipwa elfu 8 anasepa.
 
[emoji23][emoji23][emoji23],Duuh hapo nimeelewa huyu kumbe ni chawa, yeye kazi yake kusifu huku na kuponda kule.
Anacho fanya yeye na unachofanya wewe ni yaleyale sema mko pande mbili tofauti, toa kwanza boriti kwenye jicho lako ndiyo utaona kibanzi kwenye jicho la mwenzako.
 
Mwizi humuhisi kila mtu anaiba, mimi sijazungumzia muziki bali nimezungumzia comments zenu umeshaanza kuniita chawa, je ninge-comment kuwa nimezikubali zaidi nyimbo za Mbosso ungeeniitaje?

Diamond ndiye mtu anayeongoza kwa fan-base Tanzania lakini kuna wengi tu wanaona wanamuziki wengine wanaimba vizuri zaidi yake vivyo hivyo hata nyimbo za Harmonize na Mbosso watu watatofautiana mitazamo.
Kulazimisha kila mtu awe na mtazamo wako nadhani huo tuuite uchawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…