Harusi mfungie kanisani, wali ukaliwe ukumbini, huo SI Upendo enyi watu wa Mungu!

Harusi mfungie kanisani, wali ukaliwe ukumbini, huo SI Upendo enyi watu wa Mungu!

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
25,937
Reaction score
41,161
Salaam ,Shalom!

Siku za mwisho imeandikwa Upendo wa wengi utapoa,

Yaani ufunge ndoa kanisani, tukushangilie Kisha chakula kiende kuliwa ukumbini Tena kwa kundi dog tu la watu!

Kiukwelli zamani palikuwa na upendo, likuwa Kila jumamosi au jumapiili sie watoto wa uswazi hatukukosa pilau la harusi la kugombania na watoto wenzetu.

Mungu ni yule yule habadiliki, rudisheni Upendo wa awali, mchele kilo 100 unatosha kutoa chakula kwa wahudhuriaji sherehe ya ndoa kanisani Kisha mwende kwenye mambo yenu ya giza na ulevi wa usiku.

Note: Huu uchoyo tuliocopy toka kwa wazungu ndio hasa unachangia pakubwa ndoa kukosa baraka na kuvunjika ndoa nyingi kwa sababu mbalimbali, ubinafsi ukiwemo.

Nimemaliza.

Ikiwa hujampa Yesu maisha yako, fuatisha sala hii.

EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. AMEN
 
Salaam ,Shalom!

Siku za mwisho imeandikwa Upendo wa wengi utapoa,

Yaani ufunge ndoa kanisani, tukushangilie Kisha chakula kiende kuliwa ukumbini Tena kwa kundi dog tu la watu!

Kiukwelli zamani palikuwa na upendo, likuwa Kila jumamosi au jumapiili sie watoto wa uswazi hatukukosa pilau la harusi la kugombania na watoto wenzetu.

Mungu ni yule yule habadiliki, rudisheni Upendo wa awali, mchele kilo 100 unatosha kutoa chakula kwa wahudhuriaji sherehe ya ndoa kanisani Kisha mwende kwenye mambo yenu ya giza na ulevi wa usiku.

Nimemaliza.

Ikiwa hujampa Yesu maisha yako, fuatisha sala hii.

EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. AMEN
Mdogo mdogo hadi utasema na honemoon iishie kanisani
 
Ukiwa kwenye mada za siasa unakua na akili nyingi sana , ukija za dini nahisi unampa computer /tablet au simu mkeo🤔
 
Si upendo kabisa, kila kitu kiishe kanisani
Eti kama huna kadi wali utaishia kuusikia tu,


Tumeiga tamaduni za uchoyo za kizungu,

Kwamba ukwepe Gharama ya wali maharage isozidi laki Tano, update pesa ya cattering kulipia sahani moja 12,000 na ulevi ukiwamo.

Hii ni sababu ya wengi kushindwa kuoa kwa wakati,

Ukumbi ml 5, wakati mchana kanisani nje pale hulipii ukumbi.

Shame on you christian wa mchongo msio na upendo.
 
Mimi ni yule yule,

Ingawa huwa Nina ushirika na Mungu ndani YANGU,aitwaye Roho mtakatifu

Tuvumiliane.
Sawa mpendwa rabon, sikupingi hata kidogo,kwani kumkufuru huyo roho wako mtakatifu ni kufuru mbaya mno 😊
 
Sawa mpendwa rabon, sikupingi hata kidogo,kwani kumkufuru huyo roho wako mtakatifu ni kufuru mbaya mno 😊
Kuhubiri SI kumkufuru Roho,

Uliza ufundishwe, usitokwe Bure maneno usoyajua.
 
Kumbuka hata bwana yesu tulitoka nae mbali tukishindia mizeituni hadi midomo yetu ikabaki na ukakasi lakini harusi yake kaikimbizia mbinguni.

N
 
Kumbuka hata bwana yesu tulitoka nae mbali tukishindia mizeituni hadi midomo yetu ikabaki na ukakasi lakini harusi yake kaikimbizia mbinguni.

N
Harusi ni mbinguni na wanadamu wote wamealikwa,

Na watakula Bure na kunywa,

Huo ndio Upendo sasa!
 
Kufundishwa hapana ,hakuna nisichojua kuhusu Dini zote na imani kwaujumla,.
Mimi sina dini ndio maana hunielewi.

Dini hizi za kusajiiliwa kama vikundi vya upatu, vyenye kusajiiliwa na kufutwa SI halisi ni fake.

Yesu ndiye njia pekee kweli na uzima, injili haina mipaka wala sensoring ndio maana wanasiasa nawakemea pia WEWE ukidhani NAMI ni mwanasiasa,

Mimi ni kama Yohana Mbatizaji, ni sauti ya aliaye toka nyikani ikidai matengenezo.

Yesu yuaja upesi.
 
Hata mimi mlevi na msinzi nimealikwa?
Ndio umealikwa ila uache pombe na uzinzi,

Kule hakuna malaya wala ugomvi wa kupasuliana chupa.


Sherehe ni ya watakatifu, mwamini Yesu upate ticket ya Bure.
 
Mtumishi wa mungu umenena kweli na umenikumbusha enzi hizo kweli hakuwa na maswala ya hzo kadi na michango ilokithiri. Yaani siku hizi wakubwa tu ndio wanasherehekea na unakuta muda pia ni usiku. Uchoyo uliokithiri huu
 
Back
Top Bottom