M-mbabe
JF-Expert Member
- Oct 29, 2009
- 13,203
- 23,027
Mtu anapotunza na kuneemesha (kusomesha, nk) familia yake au ukoo wake huwaga anapewa sifa kedekede na jamii kuwa ni mtu mwenye busara na muwajibikaji.Ndio basi tena his legacy will live forever.
Ni kwamba eti
Hasara itokee isitokee
Mambo aliyofanya Magufuli katika kipindi chake kifupi hata vipofu wameyaona. Vipofu nao wanasimulia Mambo aliyofanya. Mabubu nao pia wanasimulia.
Ndio hivyo ndugu zangu.
Kama unaumia
Nenda kabomoe Ubungo na Tazara interchange.
Ukiona haitoshi kabomoe hosipitali zilizojengwa kila kijiji.
Ukiona haitoshi kabomoe lile bwawa letu la umeme.
Ukiona haitoshi kabomoe ikulu yetu pale Dodoma.
Ukiona haitoshi kabomoe barabara zilizojengwa huko.
Ukiona haitoshi kabomoe reli yetu ya standard gauge.
Ukiona haitoshi kabomoe na reli yetu ya umeme.
Ukishindwa kachukue kamba ujinyonge tu.
Itoshe tu kusema his legacy will live forever.
Sasa, mimi hapa ni jambazi. Wakati wa uporaji nishaua mwanao na wana wa rafiki zako, ndugu zako, jirani zako, washikaji zako ili nineemeshe ukoo wangu
Kama unaumia..
Kanyang'anye degrees za Havard za mtoto wangu aliyesomeshwa na hela yangu ya wizi
Kanyang'anye degrees za Havard za mdogo wangu aliyesomeshwa na hela yangu ya wizi
Kanyang'anye degrees za Havard za mke wangu aliyesomeshwa na hela yangu ya wizi
Kanyang'anye degrees za Havard za binamu yangu aliyesomeshwa na hela yangu ya wizi
Kanyang'anye degrees za Havard za mjukuu wangu aliyesomeshwa na hela yangu ya wizi
Kanyang'anye u CEO wa mkwe wangu ambaye hela yangu ya wizi ilitumika kumpa cheo hicho.
Niongeze volume labda?