Hasara itokee isitokee mambo aliyofanya Magufuli hata vipofu wameyaona

Mtu anapotunza na kuneemesha (kusomesha, nk) familia yake au ukoo wake huwaga anapewa sifa kedekede na jamii kuwa ni mtu mwenye busara na muwajibikaji.

Sasa, mimi hapa ni jambazi. Wakati wa uporaji nishaua mwanao na wana wa rafiki zako, ndugu zako, jirani zako, washikaji zako ili nineemeshe ukoo wangu

Kama unaumia..
Kanyang'anye degrees za Havard za mtoto wangu aliyesomeshwa na hela yangu ya wizi
Kanyang'anye degrees za Havard za mdogo wangu aliyesomeshwa na hela yangu ya wizi
Kanyang'anye degrees za Havard za mke wangu aliyesomeshwa na hela yangu ya wizi
Kanyang'anye degrees za Havard za binamu yangu aliyesomeshwa na hela yangu ya wizi
Kanyang'anye degrees za Havard za mjukuu wangu aliyesomeshwa na hela yangu ya wizi
Kanyang'anye u CEO wa mkwe wangu ambaye hela yangu ya wizi ilitumika kumpa cheo hicho.

Niongeze volume labda?
 
Avatar yako tu inapicha ya zombie, hiyo inadhihirisha jinsi mindset yako ilivyo ya kishetani
A ha ha ha ha kijana pole

Na pia wape pole walimu wako waliokufunza shule ya iman ya kuwa sura ya shetan na jamii yake ipo kama hicho kitu umekiita zombi
 
Uwe mfuatiliaji, tatizo maendeleo na watu kukosa haki zao kwa wakati si sawa, ni heri kupunguza baadhi ya mambo watu wapate stahili zao, waangalie wastaafu hadi miaka miwili hawajapata chochote, wafanyakazi muda unaenda madaraja hayapandi hivyo wanakosa mishahara stahiki, mambo mengi hayapo sawa, tuendelee kuomboleza kwa amani!
 
Hayo ni maombolezo ya kuzishusha tu bendera nusu mlingoti kutokana na hadhi ya marehemu! Ila kwa sisi wanyonge, tunaendelea na maisha yetu kama kawaida! Kula maisha wewe! 😇
Mimi Nasubiri 40 💇‍♀️
 
Asiwepo wa kukupinga. Kama mtu hakuyaona basi hata kipofu alisikia mlio huko DODOMA. Uko sahihi.
 
NIMEONA WATU MMEANZA KUFOKA NA SIO KUELEZA, KWA KAWAIDA MWIZI HAPENDI ITWA MWIZI ,MALAYA HAPENDI ITWA MALAYA NA MUUAJI HAPENDI ITWA HIVYO KADHALIKA KWA FISADI ATAJITAHIDI AJIPATIE WATU MAKUNDI MAKUNDI AKIWALIPA FEDHA ILI WAZITUMIE KUMSAFISHA MWIZI
KWAKO NDG KAMA HUKUWA MNUFAIKA WA FEDHA HIZO ACHA KELELE ZA KUMBAGAZA MH,RAIS AFANYE KAZI YAKE.
KWA MTU MWENYE UADILIFU HUJIFUNZA TOKA KWA WAZAZI WAKE TABIA NA MWENYE DO MWEMA,KAMA ULIVYO MAKUAMINI,MWACHE MAMA AFANYE KAZI, VIVA MH,RAIS VIVA TANZANIA.
 
Tunarudi kule kule kwa Jakaya, '…hata kama wameiba kazi yao tumeziona…' sio tena Wizi na ubadhirifu umekomeshwa
 
Ongeza na majengo ya chato
 
Hata aliyofanya JK, Mkapa,Mwinyi na Nyerere yalioonekana.
 
Huu ujinga wa kujivisha upofu wa mambo yanayo ongekewa na kuonekana wazi ndio unaoitafuna CCM kwa sasa. Na mkiendelea hivyo mtakuja kutuletea balaa katika hii nchi.

Ogopa sana mtu ambaye ananyima uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa mijadara huru ya jamii kujadiri mienendo ya serikali yao, Mtu ambae anaamin katika mawazo yake pekeee, mtu ambae anawachukia wote wenye mtazamo tofauti na yeye. Mtu huyu hawezi kua na mapenzi mema na hii nchi.

Hatuwezi kua taifa tunacheza ngoma ya mtu mmoja, ni upumbavu wa hali ya juu sana.

#DumuTanzania.

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
Hivyo vyote kavikuta mezani jk alishapitisha vifanywe sema ni mda ulimtupa mkono .
Magu yeye labda ni hilo bwawa la umeme ndio alichoweza kufanya tuu .
Najua utabisha siko tayari kubisha naomba niishie hapo
 
Waimba mapambio wanamalizia malizia sifa zao za kipumbavu😅😅😅😅
 
Hii ni vita ya kiuchumi sasa kama ATCL imepata hasara solution ni nini? kuziuza au kuangalia namna bora ya kuziendesha kwa faida?
wapo wasiotakia mema hili taifa wanatamani ndege hizi zisiwepo, ili ziletwe za vibaraka wao na ndio hao wanaopiga kelele sasa wakishangilia hasara bila kuzungumzia faida zake kiuchuma siku za usoni.
 
Mbona kijiji changu hakina Hospital.

Au unaongelea vijiji cha chato?
Meko keshakufa. Mataga huamini?
SHIRIKA la Ndege Kenya liimepata hasara ya Sh bilioni 36.2 mwaka jana ambayo ni hasara kubwa katika historia ya shirika hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…