kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Sina mashaka na uzalendo wa Tundu Lissu kwa Taifa. Kinachomponza ni kuwaambia watu tusikombe mboga ili tushibe wote. Kuna watu hawataki kuambiwa usikombe mboga, wanachofurahia ni wao wakombe peke Yao wengine mle ugali kwa kuchovya tongue au mle bilà mboga kabisa.
Tundu Lissu aliwaonya watu kuhusu ubaya wa kuvunja mikataba bila kufuata Sheria za kuvunja mkataba uliofungwa kisheria. Lakini aliambuli kile alichokiambulia. Sasa tunaambiwa taifa limeingia hasara inayotugharimu sisi wote na akiwemo Tundu Lissu.
Nashauri deni hilo lilipwe na waliohusika kuvunja mkataba wa symbion na mikataba mingine iliyovunjwa kwa njia hizo kama wenyewe watashinda kesi. Tushikilie Mali zao popote zilipo ndani na nje ya Nchi na kuzipiga mnada kulipia gharama hizo, na deni litakalobaki basi ndio sisi wote kwa shingo upande kabisa tulilipe.
Hii ni kuonyesha kuwa CCM imeshimdwa kuisimamia serikali yake, wajitafakari.
Tuliambiwa hakuna watumishi hewa mbona CAG amesema wapo wengi TU? Tulidanganywa? Kuna watumishi hawakupandishwa vyeo Wala kuongezewa mishahara Yao kwa kisingizio kuwa wanashughulika na watumishi hewa kwanza, mbona wapo?