SABABU ZA VIJANA KUOA SINGLE MOTHERS
Najua wenye vichwa ngumu watabisha na kujifariji ila zifuatazo ndio sababu za vijana kuoa single mothers
1. Kijana kutaka mwanamke cheap
Kuzaa kabla ya ndoa huwa kunaishusha thamani ya mwanamke. Hivyo mwanamke aliyezaa mahari yake huwa ni ndogo kuliko ambaye hajazaa. Sasa vijana kwa kupenda kitonga huwa wanakimbilia huko ili wapate punguzo la mahari (kwa sababu wao ni waokoa jahazi)
2. Kuanza maisha ya pamoja kabla ya ndoa
Wanawake wengi waliozaa kabla ya ndoa kwa kutambua kuwa thamani zao zimeshuka huwa wako tayari kuanza maisha ya kinyumba kabla ya ndoa. Hivyo vijana wapenda vitonga huwa wanakubali kuanza kuishi na hawa wanawake ili waanze kufaidi matunda ya ndoa kwa gharama ndogo kabla ya ndoa yenyewe.
3. Kusaidiwa mahari ya kuolea
Mara nyingi vijana wanaooa single mothers mahari ya kuolea huwa ni tatizo kwao. Hivyo huwa wanakubali kuanza maisha na single mothers ili wasaidiane kutafuta mahari. Japo wengi huwa wanalikataa hili ila ukweli ni kwamba direct/indirect huwa wamesaidiwa na single mothers kutafuta mahari.
4. Kusaidiwa harusi
Kwasababu harusi zimekuwa ni gharama kubwa hasa kwa wakristo. Vijana wengi wapenda vitonga huwa wanakimbilia kuoa single mothers, kwasababu mara nyingi single mothers tayari wanakuwa wameingia kwenye utafutaji, wako kwenye vikundi vya kinamama na vikundi vingine vya kijamii hivyo huwa wanawasadia kuchangisha michango ya harusi na kujigharamia maandalizi ya harusi kama shera, saluni n.k. Tukumbuke harusi ni jukumu la bwana harusi na familia yake. Bibi harusi na familia yake wanapaswa kushughulikia kitchen party na send off, siyo harusi.
5. Kijana kutaka kusaidiwa maisha kwa kigezo cha mipango na uchakarikaji wa mwanamke.
Kama nilivyotangulia kusema hapo kwenye #4 mara nyingi kutoka na burden ya maisha single mothers wanalazimika kuwa wachakarikaji na mipango mingi, wakati wale ambao hawajazaa wengi huwa huwa bize na urembo na fasheni. Hivyo vijana wapenda vitonga huwa wanawaona single mothers ni fursa kwao ili wasaidiane maisha (mipango na uchakarikaji)
6. Kijana kutaka upendo na utiifu cheap
Kwasababu wanawake ni hypergamy in nature, huwa wanawapenda na kuwatii wanaume ambao wako juu yao kiumri, kiuchumi, kifikra kimaamuzi, wenye uzoefu wa n.k.
Mwanamke anapozaa kabla ya ndoa na thamani yake kushuka huwa analazimika kupunguza vigezo na demands zake kwa mwanamume. Pia ili wakubalike huwa wanaamua kuonyesha upendo na utii bandia wa kiwango Standard gauge. Hapo ndipo single mothers wanapogeuka kuwa kimbilio la vijana ili vijana wajipatie upendo na utii kwa gharama nafuu.
N.B
i. Hz sababu zote nilizozitaji single mothers huwa wanazijua, wazikubali na kuzitii japo kwa shingo upande ili wafanikishe mambo yao.
Hii inasababisha single mothers wengi waishi maisha ya vifungo na wanaume ambao hawawavutii, kuwataka wala kuwapenda. Hivyo inapotokea tu single mother akajipata kimaisha na akapata mwanaume anayemvutia na kumpenda (mara nyingi huwa ni wale waliowazalisha hapo kabla) hakuna rangi utaacha kuona. Utabaki kutulialia bila sababu.
Ukijakunililia nakuchana makavu kabla ya kukupa ushauri ama msaada.
ii. Bila kujali single mother ni mama yangu mzazi, dada yangu wa tumbo moja ama binti yangu sababu nilizozitaja zinabaki kusimama mahali pake.
HAKUNA SINGLE MOTHER ANAYEFURAHIA KIJANA WAKE AU KAKA YAKE KUOA SINGLE MOTHER