Miaka ya nyuma ipi mkuu, unataka turudi nyuma?
Haya twende taratibu, miaka ya nyuma unakumbuka elimu haikuwa kipaumbele? Unakumbuka mabinti walikuwa wanaolewa na miaka mingapi?
Miaka ya nyuma unayoisemea binti alikuwa akishavunja ungo, anapelekwa unyagoni kisha anatafutiwa mume anaolewa?
Vijana wa kiume nao ivoivo, walikuwa wakishabalehe, wanapelekwa jandoni, wakirudi wanakuwa tayari kuoa.
Siku hizi elimu inawafanya mabinti na vijana wafikishe miaka 23, 24, 25, 26 wakiwa hawana mbele wala nyuma. Meanwhile wameshabalehe na kuvunja ungo, unatagemea wataacha kufanya kisa hawajaoa au kuolewa?