Umenisoma.vzr sana mkuu..
Jana kuna binti nilikuwa naongea naye, ana 21 yrs, ameshamaliza diploma, yuko tu nyumbani. Amelelewa kimayaimayai, ajira hataki kuapply, lipolipo tu. Imagine jitu zima la miaka 21 limemaliza chuo ila kufuata vyeti lilisindikizwa na mama yake.
Sasa tukawa tunaongea mambo ya mahusiano, nikamuambia ukipata kijana anataka kuoa, basi olewa, muda ndo huu. Eti kananijbu muda bado, ngoja kwanza nifikishe miaka 25 hivi, ili nami nijipange angalau hata niwe nimesimama nina cha kwangu.
So, unaona kabisa mabinti wameshaharibiwa mentality, wanachojua wao kuolewa na miaka 20,21,22,23 ni mapema sana, wakati ndiyo muda sahihi wa binti kuzaa watoto wenye afya..
Wanashindwa kujua kwamba wao kwa sasa wana miaka 20 huku mama zao wakiwa na miaka 40+, ina maana mama zao waliolewa na mapema na miaka 19 na kuendelea.